Slaa: Jakaya Kikwete ana mkono EPA

Slaa: Jakaya Kikwete ana mkono EPA

Mr Dhaifu katenda,tujipange kwa katiba mpya kupunguza madaraka ya rais
 
Nimekumbuka ule usemi wa binadamu wote ni sawa ila wengine ni sawa zaidi kuliko,yaani mtu anakwapua mapesa yote hayo afu anapewa msamaha na rais?Kweli jela ni kwaajili ya maskini.
 
SIKU chache baada ya Jeshi la Magereza nchini kukiri mfanyabiashara, Ajay Somai, aliyetupwa jela miaka miwili kwa kosa la kukwapua sh bilioni 3.8 kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), amepata msamaha wa Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa Rais Kikwete ana mkono na EPA.

Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana katika mikutano ya hadhara iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika eneo la Ifunda, Kijiji cha Mawambala katika Jimbo la Kilolo na Iringa Mjini, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya Operesheni inayoendelea nchi nzima, iliyopewa jina la ‘M4C- Operesheni Pamoja Daima’.
Huku akisikilizwa kwa makini na maelfu ya wananchi wa maeneo hayo, Dk. Slaa alisema ni jambo la kushangaza kwa rais kuwaacha watuhumiwa wadogo kama wale wa wizi wa kuku, lakini ameamua kutoa msamaha kwa wezi wakubwa wa fedha za EPA.

“Hii ni kashfa kwa Rais Kikwete, haiwezekani ukatoa msamaha kwa wezi wakubwa walioiba mabilioni ya fedha halafu ukawaacha watuhumiwa wa makosa madogo, tena wengine wa kubambikiwa kesi na polisi wakiendelea kusota gerezani. Hapa lazima kuna mkono wa Kikwete,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye amepata kuwa mgombea urais wa CHADEMA, alisema kuwa mfungwa huyo wa EPA ambaye yuko nje kwa msamaha wa rais wakati wa kampeni za mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), alikodi ndege kwa ajili ya kampeni za mgombea huyo.

Mbali ya Somai, wezi wengine wa EPA waliopata msamaha huo ni wafungwa namba 24/2011, Farijala Shabani anayetumikia kifungo cha miaka 11 na mfungwa namba 345/2011, Rajabu Maranda anayetumikia kifungo cha miaka kumi, ambao nao wamenufaika na msamaha huo wa rais uliotolewa Desemba 9, mwaka jana.

Kwa mujibu wa Dk. Slaa,
CHADEMA ikiingia madarakani wezi hao watakamatwa na kurudishwa gerezani na zaidi ya yote, watalipa fedha walizoziiba.

Mbali na suala la kuachiwa kwa wafungwa wa EPA, Dk. Slaa alisema deni la taifa limezidi kuongezeka ambapo hadi sasa kila Mtanzania hata yule anayezaliwa leo, ana deni la sh 500,000.

Mbowe azidi kulia na Katiba mpya

Wakati Dk. Slaa akirusha kombora kwa Rais Kikwete, Mwenyekiti wake wa taifa, Freeman Mbowe, amesema kuwa Katiba Mpya na bora ni ile itakayopata uhalali kutokana na mchakato wake kuhusisha maoni ya watu badala ya masilahi ya chama tawala.

Alisema Katiba ya aina hii ndiyo itasaidia taifa kuponya majeraha na kuondoa makovu ambayo wananchi wameumizwa kwa muda mrefu.

Alisema CHADEMA haitawaangusha Watanzania katika kupigania na kusimamia masuala ya msingi likiwemo suala la Katiba Mpya, huku akiwataka waiunge mkono wakati wa Bunge Maalumu la Katiba.

Mbowe alisema CHADEMA inatambua umuhimu wa Katiba mpya kwa mustakabali wa Watanzania na jinsi wananchi walivyo na matumaini makubwa kuwa itasaidia kuweka mazingira ya fursa za maendeleo kwa mtu, makundi katika jamii na taifa zima kwa jumla, hivyo watasimama kidete kwa niaba ya Watanzania.

Alisema hayo jana alipokuwa akihutubia mikutano ya hadhara maeneo ya Muleba, Biharamulo, Chato, Nyang’hwale na Geita, ikiwa ni sehemu ya mfululizo wa mikutano ya operesheni inayoendelea nchi nzima, ikiwa imepewa jina la ‘M4C-Operesheni Pamoja Daima’.

Mbowe ambaye aliingia rasmi kwenye operesheni hiyo tangu Jumamosi wilayani Ngara, alisema kuwa chama chake kwa kuunganisha nguvu za pamoja kwa kushirikiana na kila Mtanzania, makundi mbalimbali katika jamii na vyama vingine vya siasa vilivyo tayari kusimamia mchakato wa Katiba kwa niaba ya Watanzania, kitahakikisha uhai wa Tanzania unapewa kipaumbele kabla ya masilahi ya vyama vya siasa.

“Ndugu zangu wananchi wa Biharamulo juzi nikiwa Ngara nimezungumzia masuala ya Katiba na daftari la wapiga kura, leo pia sina jinsi, nawiwa kuzungumzia suala hili nyeti la Katiba kwenu. Nimesema na nitarudia kusema tena na tena na tena, kwamba suala la Katiba ni uhai wa taifa.

“Kutokana na ukweli huo, kwetu sisi CHADEMA na watu wengine wenye mapenzi mema na nchi yetu vikiwemo vyama vya siasa vilivyo tayari kushirikiana kwa ajili ya jambo hili kubwa linalozidi tofauti zetu zote tunazoweza kuwanazo, tunalichukulia kuwa ni suala la Katiba mpya iliyo bora na inayozingatia matakwa ya Watanzania, ni suala la kufa na kupona.

“Kuna vyama vya siasa vinafikiri katiba zao zinaweza kuwa kubwa kuliko Katiba ya nchi. Tunawataka wafikirie mara mbili sana. Katiba za vyama ni kwa ajili ya vyama hivyo lakini Katiba ya nchi ni kwa ajili ya Watanzania wote nchi nzima. Kuchezea maoni ya watu kwa ajili ya kulinda masilahi ya chama fulani cha siasa ni dharau inayovuka mipaka ya kiburi cha utawala,” alisema Mbowe na kuongeza:

“Tunataka Katiba mpya hii iende kuponya majeraha na kuondoa makovu ya muda mrefu yaliyoko ndani ya jamii yetu ya Watanzania…wote tumeumizwa kwa namna moja ama nyingine, majeraha na makovu hayo yanaweza kupunguzwa au kumalizwa kabisa na Katiba mpya na bora itakayopata uhalali kutoka kwenu.”

Tanzania Daima – Slaa: JK ana mkono EPA

Ni hao wezi wa EPA ndio wafadhili wakubwa wa CHADEMA tena lakusikitisha kabisa wakati pesa hizo wanazitoa kama msaada mwenyekiti yeye anakikopesha chama.
 
kwahiyo wewe unaona sawa tu hapo waliochiwa na kuib ahayo mabilioni? kama ww sio ndugu au ulifaidika basi utakuwa ni moja kati ya mambumbumbu yasiyojitambua na yaliyolewa ushabiki

Mkuu mbumbumbu wewe na jinsi ulivyotamalakiwa na Slaa na Mbowe kiasi cha kupokea kila uchafu na takataka kama septic tank! Hujui kuchambua uongo na ukweli bora kasema Babu! Funguka usiwe mtumwa wa binadamu wewe! Ndio maana mungu kakupa kichwa, ubongo,macho na masikio uvitumie kutafakari na usisukumwe na mihemko. Ni kweli watu wanahitaji maendeleo tena sana lakini,sio kwa kudanganya umma! Mi nimesema atatumia procedure gani kuwafunga tena? Mbona swali rahisi! Au ataamua kuwa dikteta sasa kila anayemtamani kumshika basi anakamata na kuweka kusikkojulikana!
 
Kweli kibabu ni kimechanganyikiwa! Hivi unadai utawakamata watu waliosamehewa magereza na kuwafunga tena! Acha uongo na kutafuta cheap popularity! We utawarudisha kwa sheria ipi? Unajua maana ya Autrofois aquit na autrofois convict? Mbona kizee kinakuwa kiongo namna hii! Na Jk anapotangaza msamaha,kuna kamati na parole body ambayo ndio inachambua kwa ngazi ya wilaya hadi kata kulingana na matatizo aliyonayo mfungwa, hapo Jk anahusikaje? Jamani ndio maana upadri umekushinda we mzee kwa uongo!
Povu la nini? Hebu jadili hoja kuliko kutoa matusi kwa mleta hoja. Au wewe ni nyumba ndogo ya Kikwete?!!
 
Tubishane kwa hoja matusi ya nini?

Mkuu matusi ndio hoja ya msingi wa book 7 group. Kwenye terms of reference zao wameelekezwa wajitahidi ku-neutralize hoja za msingi zinazoletwa hapa kwa kuingiza matusi na mambo ambayo si sehemu ya hoja iliyo mezani. Wakati watu tunahoji ilikuwaje hawa wezi wa mabillioni wameachiwa baada ya muda mfupi kifungoni, wao wanakuja na kitu tofauti kabisa. Wasamehe bure kwani bila kufanya hivi, mkono utakuwa hauendi kinywani.

Tiba
 
Kweli slaa noma yaani ukiongelea jk tu watu wanaanza kumsema dr.slaa

Tunachosema sio ati akisemwa JK tunakasirika no! Tunataka reasoning! Je kibabu kinachosema ndani yake kuna ukwelia au ni kuendeleza mbwembwe za kuungwa mkono! Na ndio maana tunasema Slaa anaendesha chama kwa matukio tu! Yani ni msanii msanii hivi. Kila tukio kwake ni mtaji! Kuachiwa mfungwa majuzi tayari ni mtaji ha! Mnatupeleka wapi! Je matukio yakiisha mtatuambia nini sasa kwenye mikutano! Na mi nawalaani kwa Mungu mpate kuongoza nchi hii japo kwa miezi sita tuone mtakuwa mnaongea nini mkipita vijiji na kukuta watu wanawasubiri kama mlivyowaahidi! I pray to Allah, make me healthier and stronger to witness this.
 
Mkuu matusi ndio hoja ya msingi wa book 7 group. Kwenye terms of reference zao wameelekezwa wajitahidi ku-neutralize hoja za msingi zinazoletwa hapa kwa kuingiza matusi na mambo ambayo si sehemu ya hoja iliyo mezani. Wakati watu tunahoji ilikuwaje hawa wezi wa mabillioni wameachiwa baada ya muda mfupi kifungoni, wao wanakuja na kitu tofauti kabisa. Wasamehe bure kwani bila kufanya hivi, mkono utakuwa hauendi kinywani.

Tiba

Matusi gani tena! Nimesema wekeni procedure atakayotumia Kibabu kuwafunga tena watu waliokwishafungwa na kusamehewa basi! Kuna tusi hapo Kamanda!?
 
Povu la nini? Hebu jadili hoja kuliko kutoa matusi kwa mleta hoja. Au wewe ni nyumba ndogo ya Kikwete?!!

Wapi nimeweka tusi? Au kwa u div 5 wako unadhani,Autrafois convict na Autrofois aquit ni matusi sio! Leta procedure atakazotumia, au ndio ataamua kuwa Dickteta kama Idd Amini? Anyang'anye mali za watu kwa kigezo cha utaifa na EPA, au aweke watu kwenye machimbo ya kutesea maana hana atakapowapeleka!
 
Nimeamini leo kunawatu wabalipwa kwa kumtukana slaa, yaan kweli unadiliki kumtetea jk katika hili, mtu ameiba mabilioni anasamehewa lakini wezi wa mbuzi wanaozea jela?!?! Hapana lazima tuhoji je ni dini zao, ni rangi zao, makabila yao, msaada wao kwa ccm, kujuana au walitumiwa tu..... nazidi kuichukia ccm mpaka cku naingia kaburini.
 
Mkuu
Hao wanaitwa Lumumba Buku saba(LB7)!
Wasikubabaishe kabisa!Wanalipwa ili kutetea uongo,hiyo ndio kazi Yao!Kwa hiyo nakushauri uendelee kuwa positive na kusimamia ukweli!MaanaUKWELI utakuweka HURU!

Achana na hawa KENGE ambao wako tayari kuuza UKWELI kwa sababu ya njaa!

CCM HAIKUBALIKI,UNGANA NA WAZALENDO KUITOKOMEZA!
 
Wapi nimeweka tusi? Au kwa u div 5 wako unadhani,Autrafois convict na Autrofois aquit ni matusi sio! Leta procedure atakazotumia, au ndio ataamua kuwa Dickteta kama Idd Amini? Anyang'anye mali za watu kwa kigezo cha utaifa na EPA, au aweke watu kwenye machimbo ya kutesea maana hana atakapowapeleka!

AUTREFOIS ACQUIT-

A plea made by a defendant, indicted for a crime or misdemeanor, that he has formerly been tried and acquitted of the same offence.

Kwahio unamaanisha kwamba Ajay Somai aliwahi kutiwa hatiani kwa kosa hilohilo la kuhusika na wizi wa EPA kiasi cha kufungwa miaka miwili na baadae kupewa msamaha wa rais au unamaanisha nini hapo, naomba ufafanuzi.

AUTREFOIS CONVICT-

A plea made by a defendant, indicted for a crime or misdemeanor, that he has formerly been tried and convicted of the same.

Hapa inamaanisha kwamba pamoja na ushahidi kuwa hafifu bado hakukuwa na justification ya kumfunga huyu Ayi Somai kifungo cha muda mrefu sio?

Ndio maana Dr Slaa anasema kwamba (nilivyomuelewa) ataangalia zaidi jinsi convictions na sentencing zilivokwenda hadi kufunga Somayi (samaki mkubwa) miaka miwili na wale wengine(vidagaa) miaka 10 na 11.
 
Tunachosema sio ati akisemwa JK tunakasirika no! Tunataka reasoning! Je kibabu kinachosema ndani yake kuna ukwelia au ni kuendeleza mbwembwe za kuungwa mkono! Na ndio maana tunasema Slaa anaendesha chama kwa matukio tu! Yani ni msanii msanii hivi. Kila tukio kwake ni mtaji! Kuachiwa mfungwa majuzi tayari ni mtaji ha! Mnatupeleka wapi! Je matukio yakiisha mtatuambia nini sasa kwenye mikutano! Na mi nawalaani kwa Mungu mpate kuongoza nchi hii japo kwa miezi sita tuone mtakuwa mnaongea nini mkipita vijiji na kukuta watu wanawasubiri kama mlivyowaahidi! I pray to Allah, make me healthier and stronger to witness this.
Laana isiyo na sababu aimpati mtu.
 
Back
Top Bottom