Slaa, Jaji Werema wavutana bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa, Jaji Werema wavutana bungeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Apr 15, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Apr 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Frederick Katulanda na Israel Mgussi, Dodoma

  BUNGE limepitisha Muswada wa Sheria ya watu wenye ulemavu wa 2010, huku Mbunge wa Karatu Dk Willibrod Slaa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema wakivutana kuhusu masuala ya wenye ulemavu kushughulikiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  Mvutano huo ulizuka jana wakati bunge likiwa limekaa kama kamati kwa ajili ya kuupitisha muswada huo.


  Dk Slaa alitaka muswada huo ubainishe katika kifungu cha 16 kuwa masuala ya watu wenye ulemavu yatakuwa chini ya ofisi ya waziri mkuu badala ya sasa ambapo inaelekezwa kuwa yatakuwa chini ya wizara katika idara ya maendeleo ya jamii.


  Kutokana na hoja hiyo ya Dk Slaa, Werema alisimama na kulieleza bunge kuwa kifungu hicho hakina shaka kwa vile kinaposema itakuwa chini ya waziri anayehusika na masuala ya maendeleo ya jamii, kinamaanisha pia kuwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.


  Majibu hayo hayakumridhisha Dk Slaa ambaye alisimama tena na kusisitiza kuwa muswada huo unapaswa kutamka wazi kwa vile dhana ya maendeleo ya jamii ni pana hivyo kutokana na umuhimu wa masuala hayo, jambo hilo liwekwe wazi na siyo kwa kificho.


  "Katika nchi nyingine walemavu wanawekwa katika ofisi ya Rais ama ofisi ya waziri mkuu, sasa tungependa waziri mkuu atoe tamko lake hapa ama itamke wazi kwa vile ikiachiwa hivyo inaonyesha kuwa inaweza kuwa na tatizo katika utekelezaji," alizidi kufafanua Dk Slaa.


  Baada ya mvutano wa muda mrefu, Werema alikubaliana naye hivyo kuuhitimisha mjadala huo na kifungu hicho kubadilishwa.

  Wakati wa upitishaji muswada huo kwa kutamka ndiyo ama siyo wakiwa katika ibara ya 37, wabunge walikaa kimya kwa muda hatua ambayo Spika Sitta aliamua kuwaeleza wabunge kuwa wanapaswa kuchangia licha ya kuwa mawazo yao kuwa majimboni kwa sasa.


  "Waheshimiwa wabunge, muswada upo mbele yetu, naelewa kuwa kwa sasa mawazo yetu yapo majimboni, lakini tunapaswa kuwa makini katika kuupitisha muswada huu," alieleza Spika.


  Akihitimisha katika muswada huo Spika Samwel Sitta naye alirejea kuiomba serikali kuhakikisha kanuni zinapitishwa mapema ili muswada huo uanze kutumika.


  Aliasa serikali kuhakikisha inashughulikia mabadiliko ambayo yametolea na mbunge wa Karatu ili kuboresha muswada huo na hasa kwa kuzingatia katika kumbukumbu za bunge, badiliko hilo limezingatiwa.

  Awali wakati wabunge wakijadili muswada huo, waliomba baada ya muswada huo kupitishwa usainiwe mapema na kanuni zake ziandaliwe kama ilivyokuwa kwa muswada wa sheria wa fedha za uchaguzi ambao baada ya kupitishwa na bunge ulisainiwa haraka kwa mbwembwe na Rais Jakaya Kikwete na kanuni zake kuandaliwa haraka.


  Baadhi ya wabunge waliiomba serikali kuhakikisha kanuni za muswada huo zinaandaliwa haraka ili baada ya kusainiwa na rais iweze kutumika na kuwasaidia watu wenye ulemavu.


  Aliyeanza kuomba kanuni za muswada huo kuandalia mapema alikuwa ni mbunge wa viti maalum Magreth Mkanga ambaye alisema haoni tatizo katika muswada huo.


  “Mie sioni shaka ya Muswada huu kupitishwa lakini shaka yangu ipo katika uandaaji wa kanuni zake. Naomba ukishaandaliwa mapema na kanuni zake pia ziandaliwe mapema ili uanze kutumika mara moja,"alisisitiza.


  Hoja hiyo ya Mkanga iliungwa na Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi ambaye aliieleza serikali kuwa kutoandaliwa kwa kanuni za sheria mapema mara baada ya kupitishwa ni ukosefu wa utawala bora.


  Hii ni mara ya pili kwa Dk Slaa kuvutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu vifungu vya sheria. Hivi karibuni walikuwa wamevutana kuhusu kifungu namba 7(3) cha Sheria ya Gharama za Uchaguzi baada ya Dk Slaa kusema kifungu hicho kiliingizwa kinyemela.


  Source: Mwananchi
   
 2. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #2
  Apr 15, 2010
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  jamaa yupo makini sana katika kufatilia masuala ya bunge lakini wengine wote wapo after maslah
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Apr 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Dr Slaa ni zaidi ya msomi, katika maswala yanayohusu taifa anaongozwa na utaifa, anasoma huku akitafakai namna taifa linavyoweza kunufaika na kila kanuni na sheria.....Mungu mpe maisha marefu huyu jamaa
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Apr 15, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Aluta Continua ila natamani hata EL angekua hodari kwa mambo ya kitaifa kama alivyo compitent kujitajirisha. Hayo mawazo ya mimi tu
   
 5. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #5
  Apr 15, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  I wish Dr Slaa angekuwa Mbunge wangu...kumpigia kura Mbunge kama Dr Slaa inatia faraja moyoni.

  Anafanya kazi yake kwa kutumia utaratibu uliopo...pamoja na kwamba utaratibu ni corrupt uliojaa mizengwe, yeye kila siku anaupinga na kutaka utaratabu ubadilishwe lakini wakati huo halazi damu kusubiri matokeo; anaendelea kutumia nafasi aliyonayo kuwatumikia wananchi.

  Matokeo yanaonekana wazi, unaweza kufikiri huko Bungeni yuko peke yake jinsi majority walivyo mabubu.

  Haishii hapo akipata mwanya wa nafasi anakuja hapa pia kutujibu maswali yetu....what an MP. Simply Brilliant...keep it up Mzee.
   
 6. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Una uhakika ni umakini na sio MASUALA YA KURA.......

  Unaweza kutowa mantiki ya kwa nini masuala ya walemavu yawe chini ya wazii mkuu na sio wizara ya maendeleo ya jamii?

  Huyu Mzee wangu naona taratibu anajongea kutoka kuwa Mwanasiasa machachari (maverick Politician) to Populist. Thanks God ana elimu ya kutosha, otherwise tungekuwa tunashuhudia the making of another demagogue. No wonder akaishia kusupport ujanja ujanja wa kina CHENGE kurudisha mianya ya Takrima wakati wa kupitisha sheria ya matumizi ya fedha katika uchaguzi.

  Mzee Slaa I realy respect you and truly admire your perseverence, guts and commitmment. Lakini katika miezi ya hivi karibuni nimekuwa nashuhudi mambo yako mengi ambayo ya dalili zote za kuelekea walipo kina Mrema na Mtikila. Unahitaji kujipa muda wa kufanya selfcriticism/reflection.

  omarilyas
   
 7. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #7
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  We kajamaa nawe una mtatizo yaani wewe kila siku ni kulialia tu.hivi hukui jamani.Unabisha vitu usivyovijua acha kukurupuka.mantiki ya kupeleka masuala ya watu wenye ulemavu no hoja muhimu na iliombwa na wenye ulemavu wenyewe na hata waziri mkuu ameikubali.wewe ni nani hata upinge..unaboa na kukurupuka kwako.
   
Loading...