Skendo: Watu watatu wakamatwa wakifanya biashara ya kusafirisha watu hai

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
[h=3][/h]
[h=3][/h]POLISI mkoani Kigoma inawashikilia watu watatu wakiwemo wafanyakazi wawili wa basi la Osaka linalofanya safari kati ya Kigoma na Dar es Salaam, wakituhumiwa kufanya biashara haramu ya kusafirisha watu hai.

Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Fraiser Kashai aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kwamba juzi saa 10 jioni askari wa upelelezi wakiwa katika doria, waliona basi la abiria katika kijiji cha Heru Juu wilayani Kasulu likikusanya watu kwa ajili ya kuwasafirisha.

Alisema katika kufuatilia hayo askari hao wa upelelezi waligundua basi hilo lilifika kijijini hapo kwa ajili ya kuwachukua abiria 44 ambao walikuwa katika mpango wa kuwasafirisha kuwapeleka Msumbiji kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za kukata mbao.

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI
 
Hivi kwa nini watu kama hawa wakikamatwa WASINYONGWE!!??. Serikali NYONGENI hivi Viumbe
 
Habari kamili ni kuwa watu hao walikuwa wanaenda nchini Msumbiji ambako, walipata kazi ya kupasua mbao na aliyekuwa anawasafirisha ni Mtanzania wa Kigoma, na ndiye aliyenunua misitu nchini Msumbiji na akarudi nyumbani kuwachukuwa wananchi wasiokuwa na ajira kwa kuwapatia ajira nchini Msumbiji, lalamiko la jeshi la polisi ni idadi kubwa ya wananchi kuchukuliwa kwa mkupuo mmoja ambao inadaiwa idadi yao inakaribia watu 40.

Sioni tatizo lolote kwa watu hao kwenda huko walikokuwa wanaenda kuanza ajira yao, nashauri jeshi la polisi liache kufanya kazi kwa kukurupuka na taarifa za kusafirisha watu wakiwa hai.
 
na geshi la polis halijui kuwa linaichafua nchi kwa kauli/shauri hili.
 
Kikubwa ni utaratibu ufuatwe, nadhani polisi wana kazi ya kuhakikisha hilo.
Sioni tatizo mtu kuwatafutia ajira wenzake.
 
Back
Top Bottom