Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

EU na USA wameshatoa tamko la vikwazo Tanzania.
Poleni watanzania, poleni watumishi.


Nchi imekuwa ya hovyo kabisa.

Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana, Taifa limegawanyika kabisa.
 
Sizonje alisema kuna wapiga dili walikuwa wanalipisha kiingilio mlangoni ila hela haionekani..mashabiki wanajaa uwanjani lakini hela hazionekani.....sa sijui kama ni kweli make kocha huyu ana tabia ya uwongo.
Watu mnaona mbali eee!
 
Watumishi mpaka sasa hawajapata madaraja yao.Tatizo sijui ni kiki au ni nini.Alipokuwa Zanzibar novemba 2017 alizungumzia kupandishwa madaraja kwa watumishi wa umma.Na mawaziri wake wakazungumzia hilo pia.Lakini mpaka sasa hakuna utekelezaji.Sizonje nitamtuma swahiba wako Mpoto,akukumbushe kuhusu hilo.Inawezekana una mambo mengi!
 
Hii falsafa ya hali ya juu sana.
 


Mfikishie salamu, hata wanazi wameshatoka uwanjani kwa kukata tamaa timu imesha shindwa kabla mchezo hujesha
 
Mzeee,kila kona anayokatiza anataka kuombewa,akiulizwa tatizo nini?.inakua nongwa
 
Sizonje nguvu pekee anayoitegemea ni mpiga ramli kutoka Koromije! Ndio tegemeo lake kwani humbashiria yaliyo mazuri naye hupenda kusikia nyimbo nzuri za kumsifia kocha ingawa timu tayari inakwenda ligi daraja la nne ngazi ya Kata ya Katoro...........

Kocha wa zamani kapata timu nzuri ya kufundisha huko UN na anafanya vizuri sana timu yake inacheza Uefa champions League kila kukicha match kibao za kimataifa na anashinda.
 
mkuu Mungu akubariki sana , unajua mwanzo sikuelewa maana halisi ya uzi huu , ila sasa nimekuelewa vizuri sana !
 
Kwa kweli sizonje kwa kumpandisha yule kinda wa kolomije umeleta balaa mtaani cheki sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…