Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Lusungo

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
29,489
Reaction score
42,564
Mpendwa Sizonje habari za siku, natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti.

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi, kocha mzembe na anafuga uvundo.

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo. Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha.

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe.

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora.

Sizonje usichanganyikiwe, mambo bado ndio kwanza safari inaanza. Ishike ngao na kigao kuyahimili majira.

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.
 
Back
Top Bottom