Sizitaki mbichi hizi

RICH OIL SHEIKH

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
883
167
Sizitaki mbichi hizi.jpg

Mnaikumbuka hii wakuu - enzi hizo either English medium schools zilikuwa chache sana au hakuna kabisa; ilikuwa lazima uipitie hadithi ya sungura mjanja.
 
Kama sijakose kuna thread ya namna hii hii. Kwa nini usichangie tu katika thread ya mwanzo ndugu ROS?
 
Lool umenikumbusha mbali ...Sungura mjanja.... ni darasa la nne kama sikosei

Singura tena karuka mtini akarukia
mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia
Kwenye mti akatoka pembeni akasogea


Jamani story ya manenge na mandawa ya uji, kuna mtu anaikumbuka lol
 
zisitaki mbichi hizi, sungura akagumia
naona nafanya kazi, bila faida kujua,
yakamtoka machozi, matunda akalilia
 
Kitambo sana mkuu. Kuna na ile safari ya kuelekea dar kwa mjomba kipindi cha likizo kiongozi.

Siku hizi hawasomi hivyo.
 
hivi watoto wa leo bado wanasoma hii hadithi maana kuna mtoto wa ndugu yangu nilimwambia anipigie hadithi za shuleni kwao akaanza hadithi hadithi,nikasema hadith njoo,akaendelea,hapo zamani za kale palitokea padre na shehe walikua wanasafiri ktk basi moja walipofika sehemu ya chakula padre akaagiza kitimoto akamkaribisha shehe,shehe akasema sisi hatutumii hio,padre akamwambia kweli hujui utamu unaoukosa.Mtoto akaendelea kunihadithia eti,walipomaliza kula basi likaendelea na safari na walipofika mwisho wa safari wakaagana kisha shehe akamwambia padre,haya bwana msalimie mkeo,padre akajibu sisi hatuoi,shehe akamwambia kweli hamjui utamu mnaoukosa.

Kisha mtoto akaniuliza,hadithi hii inatufundisha nini,nikamwambia inatufundisha kuwa tanzania ni nchi ambayo waislam na wakristo wake wanapendana.Akacheka akasema umekosea,nikwambie jibu ,ikabidi nimtume kwa kuhofia jibu ambalo angeweza kunipatia.
 
Back
Top Bottom