Wakongwe karibuni,GENZ msichangie tafadhali

Wakongwe karibuni,GENZ msichangie tafadhali

Sakwe

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2022
Posts
245
Reaction score
879
Wakuu habari ya majukumu!
Leo katika harakati zangu nimepata bahati ya kusikiliza nyimbo mbali mbali za enzi hizo maarufu kama zilipendwa.
Kwanza nilianza na kibao cha Amigo chao les wanyika,nikagundua amigo hakuwa na makosa maana tuhuma alipewa amigo peke yake mbona hatukusikia upande wake nini kili msibu kufikia hali ya kukosa chakula na mavazi mpaka mke wake kumkimbia 😄

Malebo yake Munishi.
Wala malebo hakuwa na haja ta kuokoka alichagua maisha yake kwanini munishi ampangie maisha malebo ,tena akafikia hatua ya kuacha kuimbia na kuanza kulia makosa makubwa haya ukisikiliza utagundua mwenye shida alikuwa ni mtumishi munishi na wala sio malebo.

Merimera Yake uncle konaya
Ukisikiliza vizuri utagundua zilikuwa chuki tuu za uncle kwa binti merimela,uncle alitumia dk 5 kasoro kumchabua merimela na hata madhaifu ya binti mbona yalikuwa ya kawaida kwa kizazi chake lakini lawama alitupiwa merimela hii ilikuwa chuki ya wazi ya Uncle kwa merimela.

Karibu wakongwe mnipe na nyinyi dondoo zenu kuhusu hizi nyimbo zenye mahadhi ya zilipendwa.
Wenu Sakwe bin sakwe
Binadamu mashaka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom