Kayenga jr
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 443
- 348
mbona umekazia hapo kwenye katerero una maanisha nini?Siku ya gulio KETERERO
mbona umekazia hapo kwenye katerero una maanisha nini?Siku ya gulio KETERERO
Dah nimekumbuka enzi zile za mashairiHadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Subgura nakuambia.
Sizitaki mbichi hizi Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
mbona umekazia hapo kwenye katerero una maanisha nini?
Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Siku ile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungura karukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karuka tena karuka, matunda akarukia,
Mwisho wake akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.
Sizitaki mbichi hizi Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Sio kama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi
Ili ni shairi tu, lilisomwa na watoto wa shule za msingi darasa la nne kama kumbukumbu zangu zipo sahihi, lakini ukiwa mtu makini mwenye kutafakari uwezi kukosa kugundua hazina iliyo jificha ndani ya ili shairi.
Tafakari kisha chukuwa hatua.
Shangazi kumbe upo! Nikafikiri ya Corona yameshakukuta!Duuh nimekumbuka mbali aisee
Hahha kumbe una roho mbaya hivyo mjomba mpk unaniombea janga linipate nipoShangazi kumbe upo! Nikafikiri ya Corona yameshakukuta!