Hadithi inayokuja, ni ya Sungura sikia,
Hadithi uliyongoja, leo ninakuletea,
Alitoka siku moja, njaa aliposikia,
Njaa aliposikia, Sungura nakuambia
Sikuile akaenda, Porini kutembelea,
Akayaona matunda, mtini yameenea,
Sungura akayapenda, mtini akasogea,
Mtini akasogea, Sungura nakuambia.
Sungurakarukaruka, lakini hakufikia,
Matunda hakuyashika, mikononi hakutia,
Hakika alisumbuka, nguvuze zikapungua,
Nguvuze zikapungua Sungura nakuambia.
Mtazame hapo juu Sungura amelegea,
Mtazame na miguu, matunda anarukia,
Atafanya sikukuu, matunda akifikia,
Matunda akifikia, Sungura nakuambia.
Karukatena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.
Sizitakimbichi hizi Sungura akagumia,
Naona nafanya kazi, bila faida kujua,
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Siokama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Hadithi nimemaliza, nimekwisha simulia,
Jambo moja sikiliza, rafiki yangu sikta,
Usikose kujikaza, mazuri kukazania,
Utamshinda Sungura, utapata mbivu hizi.
Kutongoza ni Fani na Kipaji:
Source ODM.
Karukatena karuka, matunda akarukia,
Mwisho Wave akachoka, kachoka hata mkia,
Penye mti akatoka, pembeni akasogea,
Pembeni akasogea, Sungura nakuambia.
"Sizitakimbichi hizi" Sungura akagumia,
"Naona nafanya kazi, bila faida kujua",
Yakamtoka machozi matunda akalilia,
Matunda akalilia, Sungura nakuambia.
Siokama hakutaka, sasa nakupasulia,
Matunda aliyataka, ndiyo kisa akalia
Tunajua hakufika, alichoka kurukia,
Alichoka kurukia, Sungura nakuambia.
Wale wanao tongozea wenzao wanaitwaje hivi!!!!!!!!!:A S embarassed:
WanITWA "Makuwadi", Babu yangu alinisimulia eti zamani alikuwa hodari wa kuwaandikia wavulana wenzie barua za kutongozea kisha wanampa ujira wa pesa mbili au tatu
Hizi beti tatu, zimenifanya nicheke, hivi kweli vijana wa siku hizi wanaweza kweli kuwa kama Sungura!? ukimzungusha siku mbili tu, kesho humuoni tena!
Weshaanza, mwenzio nishazichoka PM zao!Haikufundishi wewe bali tule tuvijana tunavyokutongoza afu unavipiga chini? Ushatongozwa na wangapi hapa JF? Kama vipi nijibu kwa PM!
Hahahaha..... kulaaaleki, ndo ile ya kizuri kula na nduguyo siyo?Mi ndo naifanya hapa mujini lakini nakula kwanza mimi ndo namkabidhi jamaa aendelee
Ngoja hii post nimforwardie MwanajamiiOne. Nikisemaga mie ananiita mzushi!!Unajua siku hizi idadi ya wanaume ni wachache kuliko wanawake, ukijifanya kulinga mwenzio anajiuliza nitampataje
Haaaa haaa haaa,my babu habari yako binafsi kwanza!
Naona leo unadili na vijana wako,ungeongeza ubeti mmoja wa kuwatia moyo kuwa wasijali wakajipange upya na kuweka vina na mizani lol!
Siku hizi watu wanamalizana kwa sms tu na km ni kibuti ni humo humo wala hakuna kurusha ngumi!
Babu hii kitu mie niliimba sana enzi hizo darasa la tatu km sikosei na mwalimu wangu mpendwa Foibe!
Nakutakia wikend njema Babu!
Kumbe na wewe kakongwe?Haaaa haaa haaa,my babu habari yako binafsi kwanza!
Naona leo unadili na vijana wako,ungeongeza ubeti mmoja wa kuwatia moyo kuwa wasijali wakajipange upya na kuweka vina na mizani lol!
Siku hizi watu wanamalizana kwa sms tu na km ni kibuti ni humo humo wala hakuna kurusha ngumi!
Babu hii kitu mie niliimba sana enzi hizo darasa la tatu km sikosei na mwalimu wangu mpendwa Foibe!
Nakutakia wikend njema Babu!