Siyo Siri CHADEMA Imepata Jeraha

Siyo Siri CHADEMA Imepata Jeraha

Chadema kama taasisi imepata jeraha kubwa. Jeraha hili linahitaji tiba madhubuti ili lisikigharimu chama. Maana viongozi waliopo ACT wanajua siri zote za chadema. Walikuwa wanashiriki vikao vya ndani kabisa vya chama. Ni sawa na kuachana na mke/mume. Hakuna wa kujivuna. Bali akili lazima itulie ili kuendelea na maisha mapya. Na usipo kaa vema utaishia kunywa pombe au kufanya ukahaba kwa kuchanganyikiwa.

Na ndiyo maana kwa mnaofuatilia kinachoendelea ukumbi wa Diamond Jubilee. Kuna mwanadada muigizaji alipotupa dogo linaloilenga chadema ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe. Nitanikuu "kumpiga chura teke ni kumpunguzia safari".

Sasa kama wanajua sili nyingi mbona hawakutoka paka walipotimliwa?hao wasaliti hawafiki popote?
 
Duuh hii kali - "Kumpiga chura teke ni kumpunguzia safari"
 
Ni kweli ndio maana wanaipeleka puta ccm angalia na chadema wasipelekwe puta na ACT maana hali ilivyo vyama vya upinzani bada la ya kuwa marafiki sasa ni maadui

vyama vya upinzani mbona tayari ni marafiki na wana umoja unaitwa ukawa?hivyo vingine sio vyama vya upinzani na matawi ya ccm
 
Ati wanajidai wako makini!
Hawajui siasa ni kuvumiliana kwa lengo kubwa zaidi, CCM pamoja na madudu ya Lowassa inaishia kutoa natamko tu lakini hawawezi kumtimua.
Hiyo ndo siasa.
Siyo siri, wamejeruhiwa.

Na ndomaana Hata huko Serikalini Pia wanalindana Na Kukwapua Mabilioni ya Hela Bila ya Hatua zozote. Chadema ni chama cha Kuwatetea Wanyonge,Unapoonekana Msaliti kwa Wananchi na Mwizi huna Budi Kuondoka. Hatufugi wezi,Mafisadi,Wala Rushwa,Majangili na Wauza Sembe na ndo maana Tunawachomoa mapema ili wasije kulisaliti Taifa Wakati tumeichukua Dola October. Upo?
 
Kila uchwao Chadema Ina Wanachama Wapya 20 Hivyo Ukitoka wewe sio Pengo tu! Hakuna Hata Mwanya mkuu Na Chadema Inazidi kuneemeka Napia nikama Unaamka Asubuh na Kufanya Usaf ndani Zile Takataka ndo nyinyi Wasaliti Tunaenda Kuwamwaga Jalalani.... Jalala nadhani unalijua nalenyewe likijaa zinahamishiwa Jalala Kuuu Hilo Pia Unalijua.

chadema mnajua kujifariji mpaka raha maana kumeza ukweli ni ngumu.
 
Huyu chura wala hata hafai aende zake tu hana maana
 
ukosefu wa nidhamu na matusi na jazba ni tatizo chadema

naangalia bunge hapa lema anapita mbele ya spika kama anaenda sokoni kilombero mpaka spika anamwambia vipi mbona unamkata spika?
huyu jamaa yupo vizuri kichwani hivi au anapuliza?
 
Ni mchubuko siyo jeraha, hakuna siri katika chama zaidi ya yale yaliyomo kwenye katiba ambayo kila mtu husoma, huwezi ukawazuia bendera fuata upepo kutoka ndani ya chama kwenda chama kingine wakifuata maslahi yao, kila siku tunatangaziwa watu wanarudisha kadi za CHADEMA lakini chama kinazidi kukua. Ilikuwa ni wakati muafaka kwa ZZK kufukuzwa ndani ya Chama kuondoka kwake ni siyo jeraha bali ni kamchubuko tuuu

mambo haya yakutane na wenye akili, lakini wenye upeo mdogo ni shida. mpaka sasa CHADEMA hakijui kina wanachama wangapi.ACT-WAZALENDO, hakipo kupunguza chamachochote bali kuleta tumaini jipya kwa watanzania.
 
mambo haya yakutane na wenye akili, lakini wenye upeo mdogo ni shida. mpaka sasa CHADEMA hakijui kina wanachama wangapi.ACT-WAZALENDO, hakipo kupunguza chamachochote bali kuleta tumaini jipya kwa watanzania.

Kwa utafiti gani unaokuonesha CHADEMA haijui ina wafuasi au Wanachama wangapi?
 
Kwa vyovyote vile chadema wamepoteza kura nyingi sana maana watu wengi wanaojiunga ACT wanatoka chadema.
Kwa taarifa yako wanaojiunga cdm ni wengi kuliko wanaotoka cdm.watz wote wanaojitambua wanakimbilia cdm+ ukawa
 
chadema mnajua kujifariji mpaka raha maana kumeza ukweli ni ngumu.

Kwa act uongo ndio ukweli na ukweli ni uongo. Hapo ndipo tunapoconclude kuwa ninyi ni ccm n not otherwise!
 
ACT fanyeni juhudi za kuichukua Kigoma YOTE. CDM maeneo yao yatatwaliwa na mgawanyiko huo. CDM ni chama cha Wachaga pekee. Ni chama cha Kikanda hasa Kaskazini. Maeneo kama Iringa Mjini na Mbeya ni kwa makosa waliyofanya CCM wakati huo. Nao wamejua walijikwaa wapi.

UKAWA sasa kwisha habari yao. Cake yao sasa imemegwa na kwenda ACT. Hiyo pekee itatengeneza njia kwa CCM kujihakikishia ushidi Oktoba na ACT kuambulia maeneo kadhaa. Nakitahilia ACT viti 15 vya Ubungo ifikapo Uchaguzi Mkuu.

Kama wanaakili nzuri,CDM wajipe miaka 5 mbeleni ya kujiandaa na kujipanga. Kwa sasa bado ni wachanga na nchi haitachukuliwa kirahisi kwa uroho wa Madaraka.

Wanawatumia Wafanyabiashara eti wakidhani ni mkakati kumbe ni kunyesa tu Mwenyekiti wao,MCHAGA,MWANA CDM,MINJA!

CDM watakula jeuri yao mwaka huu!

Uwatake radhi wa tz kwa kuwaita wachaga maana cdm inapatikana kila kona ya nchi hii kwa makabila yote .
 
CHADEMA wanafanya kazi kwa kuongozwa na hisia sana. Kwa nchi zilizoendelea hata kama mwanasiasa amethibitika anakihujumu chama, ila as long as ana impact ndani na nje ya chama, sometimes its normal to work with the devil!
Hawana uvumilivu kwa wasaliti kama vile wewe usivyokua na uvumilivu kwa kila kitu unaendeshwa na hisia Kama jina lako unavyojiita " patient zero"
 
CHADEMA wanafanya kazi kwa kuongozwa na hisia sana. Kwa nchi zilizoendelea hata kama mwanasiasa amethibitika anakihujumu chama, ila as long as ana impact ndani na nje ya chama, sometimes its normal to work with the devil!
Unaweza kutuwekea fact za impact ya Zitto ndani ya CHADEMA na tuanzie kwenye jimbo lake na mkoa wa Kigoma.
 
kweli act chama chawasiojielewa nn tafsiri ya msemo huu?"kumpiga teke chura ni kumpunguzia safari" poor zzk
 
vyama vya upinzani mbona tayari ni marafiki na wana umoja unaitwa ukawa?hivyo vingine sio vyama vya upinzani na matawi ya ccm

Inamaana ukielewana na cdm mpinzani lakini kama uelewani nao unageuka kuwa shoga au ccm b?
 
Back
Top Bottom