Siwapendi watu wa aina hii.

Siwapendi watu wa aina hii.

Aine

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
1,603
Reaction score
489
1. Watu wanaopenda kutema mate sehemu isiyostahili hata kati kati ya barabara ya lami
2. watu wanaopenga kamasi wakati wenzao wanakula
3. watu wanaotema makohozi popote pale bila kufukia na mchanga
4. watu wanaosukutua maji mdomoni sehemu za kula tena hadharani
5.watu wanaotema mate kwenye sink au kupenga kamasi hotelini au restaurant halafu anaacha hivyo hivyo kana kwamba hatatumia tena hilo sink
6.watu wanaokwenda chooni halafu hawaflash

hivi watu hawa wanafikiria nini kufanya hivyo! ebu tubadilike jamani, kweli inakera sana
 
Wanaopiga chafya bila kujizuia kwa kitambaa ama hata mkono ikibidi.
hali ya hewa hubadilika kwa muda.
 
Kuna madereva ambao wanaendesha gari mjini wakiwa wamewasha taa FULL yani wanaboa sana,wanawasha taa full utafikiri wanapita mikumi?
 
na wanaokojoa popote pale hasa wanaume, hata nyuma ya gari yaani mtu anakojoa tu jamani unaondoa utu wako kiasi hicho, hatuna ustaarabu!!!!
 
Nafikili ulipaswa usizipende tabia na si mtu.
Kwani tabia ni matendo
na mtu ni mwili.
Kutokumpenda mtuu ni dhambi.
I hope umemaanisha huzipendi hizo tabia.

Mungu atusaidie.
 
Nafikili ulipaswa usizipende tabia na si mtu.
Kwani tabia ni matendo
na mtu ni mwili.
Kutokumpenda mtuu ni dhambi.
I hope umemaanisha huzipendi hizo tabia.

Mungu atusaidie.
simpendi mtu mwenye tabia hizo, ushawahi kuona tabia zikajitokeza bila mtu kuwepo, anayefanya hivyo ni mtu na wala tabia hazikai juu ya mti, ni mtu anaamua ngoja niteme mate, kwa hiyo wewe una maanisha mtu akikojoa barabarani utampenda ila utachukia tabia zake(kivipi hapo?)
 
Umesahau watu wanaongea hk mate yawatoka na kujaa sehemu za pembeni mwa midomo yao
 
Back
Top Bottom