Kwa hiyo unajaribu kusema aache ustaarabu na amewasaliti?Lini wapinzani wa Bongo wamewahi kulipwa kwa siasa za kistaarabu?Huyu Lema kesho na keshokutwa atapigwa virungu kama sio mabomu ya machozi na nyie wafuasi wa CCM mnaomsifia leo hii ndio mtakuwa wa kwanza kumkejeli na kumdhihaki na hata huyo anaemtetea leo hii nae hatamsaidia kwa lolote.
Very true .Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.
Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?
Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Kwani kijana amehukumiwa na sheria au Rais?Sheria ya mtando iko wazi ndio uliyo nshikisha adabu!KIJANA ALIKOSEA KWELI AJIFUNZE KUJENGA HOJA ZA KISIASA
KWA UPANDE WA PILI ANGESAMEHEWA INGELETA PICHA YENYE KUVUTIA ZAIDI KULIKO IYO ADHABU YA KUWAFANYA WAOGOPE KUMZUNGUMZIA RAISI KWA MAMBO AMBAYO ANAKOSEA
.....
Rais yeye ana haki ya kuwaita watoto wa wenzie '******' eh?
Kijana hakuchangiwa pesa eti sababu kafanya vema kumtukana mkuu (japo yeye aliwahi kuitwa mpumbavu na lofa). Alichangiwa pesa ili asiende jela kwa miaka mi3 na aendelee kushiriki vema shughuli za maendeleo katika jamii.Kemea kwanza tendo linalofanywa na vijana na madiwani wenu. Kitendo cha kumchangia fedha mtuhumiwa kinatoa taswira mbaya kwa chama chenu japo wengine wanaona ni kitendo cha kishujaa lakini huwezi kuenzi ushujaa katika mambo ya kijinga.
Unajua tofauti kati ya kutukana na kukosoa?Rais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Mmh! Huyu ni wewe Mh Lemma? There some thing wrong here.Lakini kamanda pia ulipaswa kusema ni vipi huyu kijana alitakiwa kukanywa.Nahisi kina tatizo kati kati yako na diwani Nanyoro na Malissa si bure." Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko , Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu .
Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono , lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara "
Godbless Lema (Mp)
Umeona wapi div 4 akawa na sifa ya kujiunga university!Asiye na adabu wala chembe za busara ni huyo Magufuli anayeita watoto wa wenzi villaza.
May be anaongezeka umri.Tangu nmeanza kukufatilia post zako na hotuba zako leo ninadiriki kusema kuwa UMEPEVUKA kisiasa,Big up Mbunge wa Arusha
Halafu wengi wanafikiri wanafikiri huyo kijana fine aliyo pewa ilitoka mdomoni tuu kumbe hipo kwenye sheria ya mitandao!Hii ni taswira ya kushuka kwa maadili ya vijana wetu...wakichekewa wataota mapembe...wapelekwe mahakamani tu...
Watumie mitandao responsibly...
Si utamaduni wetu kutukana wakubwa...awe rais au jirani...washikishwe adabu...hakuna namna...
Iko hivi: "Jiheshimu utaeshimiwa"Kwa hiyo unajaribu kusema aache ustaarabu na amewasaliti?
Nafkiri hilo linaweza kuwa sahihi kwasababu nilitegemea angekosoa kitendo cha huyo dogo kuwekwa ndani kwa kosa hilo.May be anaongezeka umri.
Ukitukanwa mahakama ipo...Kwani ni rahisi tu anayetukanwa nchi hii?? Kumwambia mtu amejinyea jukwaani sio tusi?? Wapinzani wanatukanwa mara ngapi nchi hii tena na wanasiasa wakubwa wa ccm,wananchi wanatukanwa mara ngapi nchi hii?? Hivi ****** na bwege utofauti wake ni nini?? Kumtukana rais wala mtu yoyote yule siyo vyema,ila tuache unafki SIO KWA RAIS LIWE TUSI ILA KWA MWANANCHI,NA VIONGOZI WENGINE SIO TUSI.......