Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Sitta: Warioba amejitakia mwenyewe

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
 
Hizo zote ni chuki na aibu za kuumbuliwa nyie vibaraka msio jua kufikiria uwezo wenu wakufikiri ni sawa na akili za kuku tu. Mmechakachua rasimu ya katiba sababu ya pesa mmesahau kuwa hiyo katiba itakuja kuwahukumu mbeleni CCM haitotawala milele karne hii sio ile ya zama za ujima hii ni karne nyingine, Watanzania wa leo wameelewa mchezo wote mlioufanya CCM mmezoea kufoji hadi kura za marehemu mmefoji amuone haya. SHAME ON YOU
 
Maneno mengiiiii, pointi hakuna hata moja kwa uliyo ya andika.
 
Amesema hawezi kujibu hilo swali kama vile Sitti Mtemvu Miss CCM alivyojibu. Kumbe wote wanafanana.

Inapotokea mtu mwenye mawazo tofauti kuhusu katiba inayopendekezwa akatoa maoni yake, waunga mkono viongozi na vibaraka wao wanakuwa wa kwanza kusema eti wawaachie wananchi waamue wenyewe. Lakini pale wao wakiongozwa na mwenyekiti wao 'propesa' JK wanaposema katiba inayopendekezwa ni nzuri muipigie kura ya ndiyo hawaoni kama wanawalazimisha wananchi kufanya yale wanayoyataka wao. Kweli nyani haoni 'tundule'

Kauli ya Sitta inaashiria kuwa pale ambapo unaposikia mtu anaongea vitu usivyopenda kusikia umrukie umpige chupa, ngumi mateke au chochote unachoweza. Hii ni kauli ya kiongozi mkubwa kabisa katika nchi hii. Kwa aina hii ya viongozi, tuache kulalamika kuwa ni maskini maana hata dunia ingetushangaa kama tusingekuwa maskini kama watu wenyewe ndio hawa. Na kwa kauli kama hizi, nahisi wameona utajiri wa nchi wamechukua wamemaliza, sasa wanataka kuwaondolea watanzania hata amani (japo ya kimagumashi) waliyokuwa wamebaki wakiitumaini.
 
Hivi mnajua bei ya hilo daraja la ndege alilpanda ukisha jua bei yake utaweza kubaini Sitta ni Mtu wa aina gani
 
Huyu Mzee ashachanganyikiwa kabisa, laana ya viongozi wa dini ishaanza kumvuruga

Laana gani ya viongozi wa dini hivi viongozi wa dini wakizungumzia suala la kisiasa linatokana na maandiko matakatifu? Wewe ndio uliochanganyikiwa kwa maana hujui yapi ya mungu na yapi ya kidunia.tena unatisha kwa sababu kiongozi wa dini anaweza kutembea na mkeo ukaogopa kumkemea kwa sababu unaogopa laana hahahahaha
 
Sitta anajidanganya,anadhani wananchi ni mambumbu kama yeye alivyombumbu,waliofanya vurugu si wananchi,ni wanachama wa ccm wachumia tumbo wakiongozwa na Makonda,anaposema eti wananchi wengi wanaunga mikono hiyo katiba haram ni uongo,hajui tu,aingie mtaani ajionee,siyo akae tu ofisini.Na kwakuwa ameunga mkono hizo vurugu,basi yeye ndiye mfadhili.
 
Naona ccm sasa hai hubiri amani tena wanafurahia waziri mkuu mstaafu kupigwa.Sitta wananchi wataamuaje bila kuchambua kilichoandikwa na genge lako la kihuni dodoma?Umetafuna pesa zetu bure
 
Mheshimiwa Sitta yuko sahihi kabisa nami namuunga mkono kwa asilimia mia...Warioba anatakiwa awaachie watanzania wataamua wenyewe lakini huku kuhangaika kwake na kujidai yeye ndiye aliyekaa na Mwalimu kuliko watanzania wote kutamuumbua siku si nyingi
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samwel Sitta amesema kilichomkuta aliyekuwa Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya Katiba jana ni sawa na kujitakia mwenyewe.

Akihojiwa muda mfupi uliopita na Redio Voice of Tabora kuhusu maoni yake kwa vurugu kubwa iliyoongozwa na Paul Makonda jana, Mzee Sitta amesema kimsingi wananchi walio wengi wanaunga mkono Katiba pendekezwa.

Mzee Sitta amesema Jaji Warioba anapaswa kutulia kwani akiendelea anaweza kuaibishwa kuliko aliyofanyiwa jana pale Ubungo blue pearl.

Mzee Sitta amemtaka Warioba awaachie wananchi Katiba pendekezwa waamue wenyewe kwa njia ya kura.Sitta ameendelea kusema watanzania wa sasa siyo wajinga na wakikuona unawadanganya watakuvamia hapohapo.Amedai uelewa wa wananchi kwa sasa ni mkubwa kuliko wakati mwingine wowote.

Alipoulizwa swali kuhusu Uvumi kwamba yeye ndiye anamfadhili na kumtuma Paul Makonda kupambana na yeyote anayempinga Mzee Sitta amecheka na kusema hatajibu hilo swali.
 
Sidhani kama wanapewa taarifa za ukweli kwa kile kinachoendelea kwa wananchi, pita mpaka vijiweni kwa wapiga debe (Watu wa kawaida kabisa) wanazungumzia kilichotokea jana, tafsiri yake ni nini? ni kweli kama anavyosema mzee sita watanzania wa leo sio wa jana, wanaelewa kilichotokea bunge la katiba na ili ajue kuwa kweli sio wa jana, vijana hawa wanasubiri kwa hamu kujiandikisha katika daftari la wapiga kura.
 
Back
Top Bottom