SITTA: Sijisafishi kanisani!

babad

Member
Feb 9, 2011
95
13
Nimeshangaa kumsikia bwana Sitta akisema eti yeye hajisafishi kupitia kanisani kama wengine huku akisema eti"Wanchi mnatujua vizuri sana,wachafu mnawajua na wasafi mnatujua"Hivi msafi anajitangaza mwenyewe madhabahuni?Hata viongozi wa kanisa wawe makini na kauli zao juu ya wana siasa kwani kuna mmoja alidiriki kusema wazi kwamba Sitta ni msafi,je ana uhakika?
 
Sitta atueleze kwa nini aliizima dowans?
kwa nini aliunga posho??
kwa nini alijenga ofisi za spika kwao kama vile yeye ni spika wa maisha???
kwa nini alianzisha chama ndani ya chama???

sita naye ni walewale wanyonya wanaichi

Eti Sitta nae anaamini atakuwa President, ni heri kuongozwa na EL laigwanan mchapakazi kuliko Sitta Mnafiki.
 
Sitta ndiye aliyeongeza maslahi ya wabunge madadufu na kusababisha mgogoro wa kitaifa kimaslahi. hivi vibwagizo vya mishahara mikubwa na posho kubwa kwa wabunge muasisi wake ni Sitta akasahau kabisa kwamba fedha za wabunge zinatoka katika fuko lilelile la hazina ya serikali linalotokana na walipa kodi ambao ni wananchi.
 
Sitta atueleze kwa nini aliizima dowans?
kwa nini aliunga posho??
kwa nini alijenga ofisi za spika kwao kama vile yeye ni spika wa maisha???
kwa nini alianzisha chama ndani ya chama???
sita naye ni walewale wanyonya wanaichi
Ahame kwenye nyumba ya spika anayoinga'nia kukaa, kama yeye yuko safi.
 
Siita alisahau kwamba kwa kuongeza maslahi ya wabunge alitengeneza ubinafsi wa bunge dhidi ya taasisi zingine za serikali ambazo zinategemea fedha ya serikali kwa malipo mbalimbali ikiwemo mishahara ya watumishi wa serikali.
 
Kama kufikiria kuhama chama kinachonyemelewa kutekwa na mafisadi ni unafiki, basi unafiki ambao kila mtanzania angeupenda maana hauna madhara kwa hazina wala rasilimali zao kuliko mijitu inayojifanya ni mitiifu kwa chama lakini motivation pekee ya kubaki ndani ya hicho chama ni kuendeleza mirija yao ya unyonyaji kwa wananchi. Ni bora kuwa na Sita 1,000 kuliko kuwa na Lowassa 1 katika nchi.
 
Eti Sitta nae anaamini atakuwa President, ni heri kuongozwa na EL laigwanan mchapakazi kuliko Sitta Mnafiki.
Hivi hatuna uwezo wa kupanua mawazo yetu na kuona watu wengine zaidi ya hawa? Lakini nadhani kikubwa tunachipaswa kuzingatia ni sifa za mtu anayefaa kuwa rais wetu. Tukishazuijua hizo ndio tuangalie nani anazo. Hili la kujadili majina kila siku tunapotea njia
 
Sitta ulipoongeza Maslahi makubwa kwa wabunge ulikuwa na maana moja tu kutaka wao waishi kama wako peponi wakati wananchi ni maskini sana. mkasahau kulitumia bunge hillohilo kudai maslahi zaidi ya wafanyakazi wa serikali wakati fedha za kulipa wabunge na wafanyakazi hao wa serikali zinatoka hazina ya serikalini ( wizara ya fedha). Siita akumbuke kuwa bunge halina chanzo chake cha mapato kwa mantiki hiyo bajeti ya matumizi ya bunge inatoka hazina ya serikalini. Kwa mwendo huu Bunge litapata jeuri wapi ya kuiambia na kuisimamia serikali ibane matumizi?
 
Eti Sitta nae anaamini atakuwa President, ni heri kuongozwa na EL laigwanan mchapakazi kuliko Sitta Mnafiki.


Ni heri kwenu wana monduli, kama unaona ubunge haumtoshi basi mnaweza kumfanya akawa raisi wenu wa monduli maana huko ndiko anakochapa kazi. Lakini kwa Tanzania EL hawezi kutufaa hata siku moja na hajawahi kuwa mchapakazi zaidi ya kuwa mchapakazi kwa familia yake!!
 
Hivi Siita aliwahi kutoa maelezo kwa nini anaendelea kukaa nyumba ya Spika wakati ana bonge la ghorofa masaki na nyumba zingine binafsi? mali za umma ni tamu bwana asikuambie mtu. Hivi sasa serikali inaingia gharama kubwa ya kumlipia Anne Makinda kwa sababu tu Sitta amegoma kumpisha Makinda kwenye nyumba hiyo ya bure kwa spika yeyote atakayechaguliwa
 
Bwana eeeh!!! nimechoshwa kbs na hawa watu. Neither of them is good. wote washamba tu wanawaza kuiba fedha za walipa kodi. Hii nchi apewe Mnyika ndio anaweza na ana utaifa.
 
Ni heri kwenu wana monduli, kama unaona ubunge haumtoshi basi mnaweza kumfanya akawa raisi wenu wa monduli maana huko ndiko anakochapa kazi. Lakini kwa Tanzania EL hawezi kutufaa hata siku moja na hajawahi kuwa mchapakazi zaidi ya kuwa mchapakazi kwa familia yake!!

shosti wake alipigwa mawe Mbeya, yeye atapigwa nondo kama sio kuchunwa ngozi
 
Ndani ya CCM namwamini zaidi JANUARY MAKAMBA wakuu

Matatizo ya hawa wengine hadi nikapoteza japo imani kidogo nao ni;

  • Magufuri - kitendo cha kuuza nyumba serikali hakikunibariki
  • Sitta - msimamo wake wa posho za wabunge, anapenda maisha ya ufahari siyo mwenzetu analiingiza taifa kwenye matumizi makubwa yasiyo ya lazima eg nyumba anayoishi, posho za wabunge
  • Membe - anajichanganya sana na siasa zake
  • Chenge - huyu nilisha omba atusahe Watz maana si mzalendo kabisa eg kitedo cha kuwasaidia dowans vifungu vya sheria ili wapate ushindi kilinisikitisha sana, tuhuma za radar, kujilimbikizia mali nje ya nchi
  • Makinda - yupo biased sana
 
tatizo la kimsingi la nchi yetu ni ufisadi unaotupotezea mali yetu ya taifa na kugharimu uchumi wetu kwa kutotoa tija wala ari kiuzalishaji. Lowassa ni mmoja wa wanaufaika wakubwa wa ufisadi katika CCM...mnaotaka kumpa urais eti ni mchapa kazi, nafikiri mtanufaika binafsi kwa njia moja au nyingine na Urais wake..Tz na wananchi wake hawataki Rais ajaye awe na taswira na dhamira ya mkuu wa genge la uhalifu...sitta anaweza kua mnafiki kama mwanasiasa yeyote hapa tz, lakini hajajilimbikizia mali kibinafsi kama fisadi na mnafiki Lowassa...juzi juzi anajidai eti vijana ni bomu linalongojea kulipuka, eti wafanyakazi waongezewe mishahara maisha yamepanda yeye binafsi alimuingiza kikwete akiwa anajua hana uwezo wa kuongoza na alimpangia baraza la mawaziri wasiokua na uwezo ili iwe ngazi yake ya kua Rais kiulaini baada ya Jk. Hakujali haya ya wafanyakazi wala vijana sasa yuko nje ya cabinet anaona matatizo kama siyo UNAFIKI wa hali ya juu ni nini hiki....
 
Back
Top Bottom