SITTA: Sijisafishi kanisani!

Hivi Siita aliwahi kutoa maelezo kwa nini anaendelea kukaa nyumba ya Spika wakati ana bonge la ghorofa masaki na nyumba zingine binafsi? mali za umma ni tamu bwana asikuambie mtu. Hivi sasa serikali inaingia gharama kubwa ya kumlipia Anne Makinda kwa sababu tu Sitta amegoma kumpisha Makinda kwenye nyumba hiyo ya bure kwa spika yeyote atakayechaguliwa

Duuuh! Thibitisha mzee.
 
Kwani kanisa ndicho kioo cha kupata Rais huko Tz?

Je Sita alipata kuonana na askofu Laizer?
 
Nimeshangaa kumsikia bwana Sitta akisema eti yeye hajisafishi kupitia kanisani kama wengine huku akisema eti"Wanchi mnatujua vizuri sana,wachafu mnawajua na wasafi mnatujua"Hivi msafi anajitangaza mwenyewe madhabahuni?Hata viongozi wa kanisa wawe makini na kauli zao juu ya wana siasa kwani kuna mmoja alidiriki kusema wazi kwamba Sitta ni msafi,je ana uhakika?
Lowassa anawatumia vibaya sana kinyume na maumbile yenu,maana akili zenu zote sasa mmemkabidhi yeye awafikirie kwa kitumia akili zake,wachafu wapo na wao wanjua kwamba ni wachafu na wengine walidiriki kumuomba mpaka mt nyerere eti aende munduli kuwasafisha!!!!!wakamtumia mzee kawawa maskini lakini mwallimu akaishia kumwambia kawawa asiwe mjinga kama lowassa yeye mtu mzima kukubali lowassa amtumie kinyeme cha maumbile yake ya akili!
 
tatizo la kimsingi la nchi yetu ni ufisadi unaotupotezea mali yetu ya taifa na kugharimu uchumi wetu kwa kutotoa tija wala ari kiuzalishaji. Lowassa ni mmoja wa wanaufaika wakubwa wa ufisadi katika CCM...mnaotaka kumpa urais eti ni mchapa kazi, nafikiri mtanufaika binafsi kwa njia moja au nyingine na Urais wake..Tz na wananchi wake hawataki Rais ajaye awe na taswira na dhamira ya mkuu wa genge la uhalifu...sitta anaweza kua mnafiki kama mwanasiasa yeyote hapa tz, lakini hajajilimbikizia mali kibinafsi kama fisadi na mnafiki Lowassa...juzi juzi anajidai eti vijana ni bomu linalongojea kulipuka, eti wafanyakazi waongezewe mishahara maisha yamepanda yeye binafsi alimuingiza kikwete akiwa anajua hana uwezo wa kuongoza na alimpangia baraza la mawaziri wasiokua na uwezo ili iwe ngazi yake ya kua Rais kiulaini baada ya Jk. Hakujali haya ya wafanyakazi wala vijana sasa yuko nje ya cabinet anaona matatizo kama siyo UNAFIKI wa hali ya juu ni nini hiki....

Hapa tupo pamoja kabisa tatizo ni misuse of public funds
na si kingine kabisa hapa .
 
Wiki iliyopita ilikuwa EL wiki hii SITTA ebu acheni hizi turudi kwenye katiba jamani tufanye nini wakati jamaa wameshahodhi mchakato
 
Sitta atueleze kwa nini aliizima dowans?
kwa nini aliunga posho??
kwa nini alijenga ofisi za spika kwao kama vile yeye ni spika wa maisha???
kwa nini alianzisha chama ndani ya chama???

sita naye ni walewale wanyonya wanaichi
mnahangaika sana aisee na huyu mgonjwa wenu wa kansa na stroke...!leo mmemuacha membe tena mmehamia kwa sitta nyie mshindani wenu ni membe sio sitta,sitta alishasema hatagombea urais,ondoeni shaka!
 
sitta hakigombea urais nachana kadi yangu ya ccm,na kujiunga chadema.jitu alina mvuto kabisa linachojua nikujiita lisafi.pumbavu
 
Kwi1kwi!kwi!sura lake na matendo yake kinafiki havitoutiani sasa ana weka bifu na mwandishi nmwana harakati wa gazeti letu jema la mwanahalisi,SAID KUBENEA,kweli 6 mabangi inamzingua sasa,
 
A pipe dream. Lowassa? Nchi gani?

Kwani hujui walamba ****** ya Lowasa wamejaa humu JF, tena wanagombea kulamba... Waache waote mchana hao.

Sitta Moto huohuo, mpango mzima ni kuchafua kisima asinywe mtu maji... maana Lowassa kishashikisha wengi ukuta.
 
Nimeshangaa kumsikia bwana Sitta akisema eti yeye hajisafishi kupitia kanisani kama wengine huku akisema eti"Wanchi mnatujua vizuri sana,wachafu mnawajua na wasafi mnatujua"Hivi msafi anajitangaza mwenyewe madhabahuni?Hata viongozi wa kanisa wawe makini na kauli zao juu ya wana siasa kwani kuna mmoja alidiriki kusema wazi kwamba Sitta ni msafi,je ana uhakika?
Tatizo huyu Mzee wetu anamchanganya Mungu na Siasa,hivi anajiona amesimama kiasi gani hata aseme kuwa yeye sio kama wengine,akumbuke sala ya yule kuhani Yesu aliyoisemea,akimlinganisha na mtoza ushuru,Nani kamwambia kuwa kanisa lina mamlaka ya kusafisha watu,Mungu wetu sio mwanasias na kamwe asiwahukumu wenzake,ni Mungu peke yake anajua siri zilizomo ndani ya huyu mzee,hata kama anataka kuaminisha umma kuwa nani mchafu,Halafu,kanisa la sasa pia limekua Babeli,Pango la wanasiasa wa staili ya huyu mzee,haiwezekani ukaseme mbele za madhabahu kwamba wewe ni mwema kuliko fulani halafu madhabau na viongozi wake waone sawa tuu
 
Eti Sitta nae anaamini atakuwa President, ni heri kuongozwa na EL laigwanan mchapakazi kuliko Sitta Mnafiki.

sitta mbona anawatesa watu wa lowassa wakati alishaweka wazi hatagombea urais ila anahamu vijana ndio wachukue nafasi hiyo ya juu kabisa nchini,sasa leo nawang'ata sikio kwa kuwa mimi ni mtu wa kiintelijensia zaidi,sikia hii,LZARO NYARANDU NDIO ATAKAEHANGAIKA NA LOWASSA KWENYE URAIS NA MZEE SITTA NDIO MRATIBU WA MCHAKATO MZIMA AMBAO INASEMEKANA UNA BARKA ZA JK!MKUMBUKE LAZARO NYARANDU NI MKATOLIKI NA ANUNGWA MKONO NA WAKUU WA HUKO JIKONI,HII HAFLA YA JUZI NI MOJA YA STRATEGY TU,SITTA FITNA ANAIIWEZA,LOWASSA ANJUA HILO SI WALIKUA PAMOJA KUMUWEKA KIKWETE HAPO NA SITTA NDIO ALIKUA MWENYEKITI LOWASSA MAKAMU WAKE!HII NIMEWANG'TA SIKIO TU NYIE WATU WA LOWASSA NAONA MPAKA SASA INTELIJENSIA YENU IMESHINDWA KUWAONYESHA ADUI YENU WA KWELI NDIO MAANA MNAPARAMIA WATU OVYO MARA SITTA MARA SIJUI MEMBE.......MNANNDANGANYA SANA MZEE WANGU HUYO
 
Hivi hatuna uwezo wa kupanua mawazo yetu na kuona watu wengine zaidi ya hawa? Lakini nadhani kikubwa tunachipaswa kuzingatia ni sifa za mtu anayefaa kuwa rais wetu. Tukishazuijua hizo ndio tuangalie nani anazo. Hili la kujadili majina kila siku tunapotea njia
Huo ndiyo ukweli kabisa kabiisaaaaaa..!
 
Kama kufikiria kuhama chama kinachonyemelewa kutekwa na mafisadi ni unafiki, basi unafiki ambao kila mtanzania angeupenda maana hauna madhara kwa hazina wala rasilimali zao kuliko mijitu inayojifanya ni mitiifu kwa chama lakini motivation pekee ya kubaki ndani ya hicho chama ni kuendeleza mirija yao ya unyonyaji kwa wananchi. Ni bora kuwa na Sita 1,000 kuliko kuwa na Lowassa 1 katika nchi.

Unafiki wa Sitta si kutaka kuhama chama tu. Unafiki wake ni kuwa yeye naye ni mmoja wa wanamtandao walioshiriki ufisadi mkubwa uliochangia kumweka mkulu ikulu halafu kwa sababu ya migongano ya kimaslahi baadae akamgeuka Lowassa na kujitangaza yeye ni safi. Kama yeye ni msafi kwa nini alizima mjadala bungeni wa ufisadi huo huo anaomtuhumu Lowassa?

Halafu nimenotice una unhealthy obsession na Lowassa. Kila mjadala unaomhusu Lowassa umo. Either uko very scared kwamba Lowassa akipata rungu (japo siombi hivyo na wala sidhani kama atapata hilo rungu) unahisi atakunyonga tu maana wewe ni mmoja wa washirika wa siasa za kifisadi na kugeukana kulikoasisiwa na wanamtandao, au upo kundi fulani hasimu na Lowassa kwenye mbio zenu za 2015 hivyo unatetea maslahi yako. Either way siasa zenu hazina mashiko, awe Lowassa, Sitta au Membe. Lowassa ni fisadi aliyekubuhu, Sitta ni mnafiki wa kutupwa na Membe hana tofauti yoyote na Jk maana hana historia yoyote ya kuonyesha kwa watanzania kama ni presidential material.
 
Back
Top Bottom