Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Sitta: Nafaa kuwa Rais wa Tanzania!

Kampiga kijembe kiaina mzee wa monduli a.k.a mzee wa richmond ambaye naye alikuwa anajipigia kampeni kanisani na nyumbani kwake alikowaalika wapambe wake kumuunga mkono kwenye safari yake ya kuusaka urais
 
Akitoa salamu za mwaka mpya katika mkesha wa kuliombea Taifa amesisitiza yafuatayo;

KWAMBA, Mafisadi na Wezi wanaojipitisha kutafuta nafasi za uongozi Wasahau ndoto hizo kwani "WAMEJIANDAA" Kuipigania Nchi hii dhidi ya mbinu za watu hao

KWAMBA, Wapo tayari watu waadilifu (JOSHUA) walio tayari kulifikisha Taifa hili katika nchi ya ahadi yenye asali na maziwa mara baada ya Rais Kikwete (MUSA) kumaliza kipindi chake.

Hizi kauli zingine mbona zina vimelea vya kujinasibisha na dini!!! Mbona hakuwataja hao mafisadi?
 
Jk hatamwachia jambazi nchi

Atamwachia Joshua nchi samweli sita leo nimemkubali
 
Jk hatamwachia jambazi nchi

Atamwachia Joshua nchi samweli sita leo nimemkubali

Huyo jk mwenyewe yupo nyuma ya hii episod ya kaka wa monduli sema wengi hamjaisoma tu hiyo ishu lao moja.
 
Hivi Watanzania wanahitaji kuambiwa nani muadilifu?

Motto mpya ni hatima Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania.
 
Siasa bwana hata wale wachafu wanautaka urais?
 
Hivi Watanzania wanahitaji kuambiwa nani muadilifu?

Motto mpya ni hatima Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania.
Tatizo watanzania tunarogeka kirahisi.....sijui ni laana!!!
 
lowasa for presidency! hana mpinzani Mr. six anajua hilo ni kama kujaribu kuweka speed gavana tu lakini jamaa anatisha..usifanye mchezo na pesa.
!
 
lowasa kumpa uraisi inawezekana ikawa sahihi lakini: angalieni ni sawa na kusema fisi wa kufugwa hana madhara kwa binadamu
 
Joshua yupi huyo atakayeitoa Tanzania hapa ilipo kwenda kanani. Je ni Mwakyembe, Magufuli, Mwandosya, Makamba, Mwigulu Nchemba au Nani hasa????


Hivi ndani ya ccm kuna wasafi kama Lowassa anavyotuaminisha kweli?????
 
Hawa wapenda Urais wamenichosha sana na hizo mbio zao.... kwa nini wasitumie muda mwingi kutueleza wametufanyia nini watanzania ili siku zikifika tuwe tumewafahamu vizuri na kuwachagua wao????? Kutufungulia misahafu kila siku ya nini? Imani ni wewe na Mungu wako unachoamini kinaweza kuwa sicho ninachoamini mimi katika roho na Mungu.... Give me a break...enough.
 
Hata siku moja jk hawez kuwa musa(moses) kamwe..! Musa alikuwa anamcha MUNGU wa mbinguni na sio miungu... So Mungu hadhihakiwi
 
Hakuna MOSES wala JOSHUA ndani ya CCM!Wote ni vibaka tu na wezi wa Mali za umma!!
 
Back
Top Bottom