Sitta na kamati yake hoi Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta na kamati yake hoi Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Nov 21, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by Mrfroasty (Ufundi) // 20/11/2011 // Makala/Tahariri // 8 Comments

  “Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano”.
  • Wajumbe wa Baraza wamchachafya
  • Atakiwa alete Katiba ya Tanganyika
  • Wengine wakerwa na “Uwaziri wa Rais”
  Na Waandishi wetu, Zanzibar
  Katika hali ambayo haikutarajiwa, Kamati ya Marekebisho ya Katiba ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekutana na mazingira magumu ya pingamizi juu ya Muswada inayousimamia.
  Muswada huo ni ule wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011 uliowasilishwa wiki hii katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mjini Dodoma, na Waziri Celina Kombani, na pia kujadiliwa katika vikao mbali mbali vya kitaifa na vya kijamii.
  Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Waziri wa Afrika ya Mashariki, Bw. Samwel Sitta, ilikutana na mazingira hayo katika Semina Maalumu ya Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar, iliyofanyika mwanzoni kabisa mwa wiki, ndani ya Ukumbi wa Zamani wa Baraza la Wawakilishi, Mnazi Mmoja mjini hapa.
  “Hakuna Sheria yoyote itakayopitishwa na Bunge la Muungano ambayo itatumika Zanzibar mpaka sheria hiyo iwe ni kwa ajili ya mambo ya Muungano tu na ipitishwe kulingana na maelekezo yaliyo chini ya vifungu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano”.
  Ni Kifungu cha 132 (1) cha Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Toleo la mwaka 1995 ambacho takriban Viongozi wote wa Serikali na wa Kisiasa waliochangia katika Semina hiyo walikinukuu usoni mwa Kamati ya Mhe. Sitta.
  Wawakilishi walikitumia pia Kifungu hicho cha 132 (2) kinachotamka “sheria kama hiyo lazima ipelekwe mbele ya Baraza la Wawakilishi na Waziri anayehusika”.
  Wawakilishi walitumia Vifungu hivyo vya Katiba wakisisitiza msimamo uliochukua sura ya kushikamana miongoni mwa pande zote za kisiasa, pamoja na wenye nyadhifa za juu za Serikali, kueleza kile umma wa Wazanzibari wanachohitaji sasa.
  Miongoni mwa waliolitumia jukwaa la semina hiyo ni pamoja na Waziri wa Kilimo Bw. Mansour Yussuf Himid, ambaye kwa maneno ya mkato alisema, kuja kwa muswada huo wa Mabadiliko ya Katiba ya Nchi kunaambatana na maamuzi halali ya iwapo wenye mamlaka ya kuitetea Zanzibar sasa watafanya hivyo au wataitelekeza kwa kushindwa kuinasua na ili ije kuwa lawama kwa vizazi vijavyo.
  Waziri wa Nchi, Mstaafu, wa Afisi ya Waziri Kiongozi wa Zanzibar ambaye pia ni Muwakilishi wa Jimbo la Kwamtipura Mjini Unguja, Bw. Hamza Hassan Juma, akitumia vifungu hivyo vya Katiba, alisema, iwe iwavyo kwa mujibu wa heshima ya kisheria, na kwamba licha ya juhudi za kuuimarisha muswada huo, kwa mashirikiano baina ya Serikali mbili, lazima ieleweke kwamba upande wa Visiwani utakuwa na maamuzi yake.
  Alisema kwa minhaji hiyo hapatakuwa na nafasi ya kuburazana tena wala kuudhoofisha upande huru wa Jamhuri ya Muungano kama ilivyokuwa hapo kabla, yaani upande wa Zanzibar.
  Naye Mwakilishi wa Mji Mkongwe wa Zanzibar, Bw. Ismail Jussa Ladhu alisema, pamoja na ulazima wa kuurejesha Muswada huo ili Wazanzibari nao wachukue maamuzi yao ijapokuwa kwa utaratibu wa thuluthi mbili za Wajumbe wa Baraza hilo, lakini pia wao kama Wawakilishi wa wananchi wanawasilisha hoja na matakwa ya msingi ya watu wa Visiwa vya Unguja na Pemba juu ya Muswada huo.
  Miongoni mwa hoja hizo ni pamoja na kuitaka Kamati ya Bw. Sitta na mamlaka zake kwanza kuitafuta Katiba ya Tanganyika ili kuweka mazingira fasaha ya kujadili Muungano wautakao sasa wananchi wa Zanzibar na huenda Tanzania kwa ujumla.
  Waliochangia na kusisitiza hoja hizo ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar , Bw. Ali Mzee Ali, na pia Katibu wa sasa wa Baraza hilo , Mwanasheria Ibrahim Mzee.
  Pamoja na hayo katika hoja iliyoleta hisia za aina yake ni pale kwa masikitiko na hali ya kusononeka alipoibuka Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Kuteuliwa na Rais wa Zanzibar , Bi. Asha Bakar Makame.
  Mwakilishi huyo ambaye aliwahi kushika Wadhifa wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Vijana wa Awamu ya Tano ya Serikali ya Zanzibar, alisema ni jambo la kuhuzunisha na ambalo si rahisi kuzituliza nyoyo za umma wa Wazanzibari, kumuona Rais wa Nchi huru ya Zanzibar akiapishwa kushika cheo cha uwaziri tena hata usio na wizara maalumu ya Jamhuri ya Muungano, alisema “hili linauma sana”.
  Kwa ujumla kuwapo kwa hoja hizi na namna Viongozi na Watendaji mbali mbali wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa, walivyosimama juu ya msimamo mmoja wa kujali haki na utaifa wao, ni kama kwamba kulipelekea Mhe. Sitta na Kamati yake kuondoka na nyoyo zilizosinyaa, huku wakiamini kuwa sasa Wazanzibari hawatanii katika kuidai nchi yao.
  Annuur
   

  Attached Files:

 2. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 664
  Trophy Points: 280
  Duh hali sasa ni tete
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Kuna watu wanataka kuushona muungano kwa kamba za kudu, sasa wenyewe hawautaki!
  Kama Zanzibar bado ni nchi hata baada ya Muungano, Muungano unasaidia nini!?
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Nov 21, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  wazenji hawautaki,wabara hatuutaki sasa kwa nini tusiuvunjie mbali tuache kuzongana.
   
 5. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #5
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Haya masarakasi ya CCM bana huwa yananichekesha sana. Sisi yetu macho tutaona mwisho wao...
   
 6. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #6
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa wazanzibar wanachonikera ni unafiki mkubwa walionao.
  Wakija huku wanauunga mkono muungano ili kuibishia cdm, wakiwa kwao wanawaunga mkono cdm.
  Vigeugeu hawa. Kudadeki zao.
   
 7. k

  kicha JF-Expert Member

  #7
  Nov 21, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 533
  Trophy Points: 180
  asitafutwe mchawi hapa kama watanzania bara hawaoni faida na kuona wnawabeba wazenj,i na wazenji nao wameshatoa kila dalili ya kutoutaka muungano, kuanzia mawaziri wa serikali kutamka hadharani mpaka wanachi wa kawaida kuandamana, hivi muungano upo kwa manufaa ya nani, ndugu zangu sisi tumeshazaana isije kufikia tukaangukia kwenye vita mungu atunusuru, busara itumike kukidhi matakwa ya pande zote mbili aidha kuacha au kujadili aina ya muungano kutokana na matakwa ya wananchi wa pande zote mbili, si busara kila kukicha kuendelea kujengeana chuki wahusika lioneli hili kwani historia itawahukumu
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Nov 21, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Macho na Masikio yetu
   
 9. Bushloiaz

  Bushloiaz JF-Expert Member

  #9
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni viongozi wetu,wanakwepa eti muungano usivunjike mikononi mwao wakati wananchi hawautaki
   
 10. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #10
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  muungano huu ni waviongozi na sio wananchi ndio maana kila anayeupinga anaonekana mhaini
   
 11. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #11
  Nov 21, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Huwezi kukwepa harufu ya yai viza kama hulitupi vinginevyo tuvumilie unafiki wa wazanzibari.
   
 12. K

  Kifulambute JF-Expert Member

  #12
  Nov 21, 2011
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 2,509
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wazanzibari wana haki ya kuomba katiba ya Tanganyika kwanza kabla ya hiyo ya muungano.......wazanzibar wapo sawa kabisa na suala la muungano sio issue sana wavunje tu maana hakuna kitu wanachopata..
   
 13. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #13
  Nov 21, 2011
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Wakuu hii habari ni ya siku nyingi.mswada umeshapitishwa na bunge tunasubiri saini ya Rais wa JMT hili uwe sheria.
   
 14. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #14
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mashaka yangu habari hii ni mpya au imenukuliwa kutoka vynzo vya habari zilizopita?
   
 15. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #15
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Habari hii ni ya zamani sana ... as back as April 2011. Aliyeipost sijui alikuwa na makusudi gani?
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  waTanganyika acheni unafiki kuweni wawazi na wakweli. Simamieni katika ukweli mtafanikiwa.
   
 17. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #17
  Nov 21, 2011
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Inawezekana ni ya zamani, lakini Dr Shein kateuliwa liini kuwa waziri?
   
 18. e

  elly1978 Senior Member

  #18
  Nov 21, 2011
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 180
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hii ni mpya, kwa mtizamo wangu ilikuwa semina kwa baraza la wawakilishi, lakini mbona wasemacho ni sawa na Chadema?
   
 19. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #19
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180

  mwanangu nikumbushe hivi dk sheini aliapa mwezi wa nne kuingia kwenye baraza la mawazi wa JMT?
   
 20. m

  mlala Member

  #20
  Nov 21, 2011
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  habari ya lini hii mkuu?, duu sidhani kama kweli ni ya leo
   
Loading...