Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Malipo ya Dowans yamechukuwa nafasi kubwa katika habari nchini mwetu. Kuna kila sababu ya kuchukuwa hiyo nafasi kutokana na upuuzi unaofanywa na serikali inayoongozwa na Jakaya Kikwete kukimbilia kulipa DOWANS.
Wiki kadhaa zilizopita aliyekuwa spika wa bunge lililopita Mh. Sitta alitamka wazi kuwa kuwalipa Dowans ni kuhujumu uchumi. Akaenda mbali na kudai kuwa Dowans ni genge la watu 3 ambao wanajiandaa kukomba hiyo hela kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu 2015.
Huyo alikuwa kiongozi wa bunge, aliunda kamati iliyoongozwa na Mh. Mwakyembe kuchunguza kashfa ya Richmond ambayo baadaye ilirithiwa na Dowans. Na matokeo ya ile kamati kila mtu anajua, ingawa ukweli mwingine bado umefichwa kwa makusudi ya kulinda maslahi ya watu fulani.
Nakumbuka Mh. Mwakyembe aliwahi kutamka hata kwenye vyombo vya habari kuwa kuna mambo mengine walificha kwa ajili ya usalama wa Taifa, kitu ambacho mie sikubaliani nacho.
Nikirudi kwenye kiini cha hii thread:
Mh. Sitta anaelewa wazi huu uhuni wa serikali wa kutaka kulipa Dowans. Sidhani kama alikurupuka kudai kuwa Dowans ni genge la watu 3. Anaelewa wamiliki ni nani. Kama ni kiongozi asiyependa majungu, kwa nini asije mbele ya UMMA na kutueleza anachokifahamu? Kama anajua kuwa Dowans ni genge la watu 3 huku waziri Ngeleja akitaja zaidi ya watu 3, kwa nini asiwataje tuone serikali itamfanya na kusema nini.
Hata Mh. Mwakyembe na wengine ambao walikuwa kwenye ile kamati, wanajisikiaje kuona nchi inatafunwa huku wakijua ukweli? Kama hawa watu hawataki kutupa ukweli inabidi tuwalazimishe watuambie ukweli. Hakuna mtu ambaye anaweza kushindana na nguvu ya UMMA. Mfano halisi ni kile kilichotokea Arusha juzi, sasa serikali inajiumauma kuwa wanataka mazungumzo. Hawakutaka hata hayo mazungumzo at a first place lakini wameona nguvu ya umma ikitumika ndio wanajikosha kuwa ooh mazungumzo.
Waziri Sitta, Mwakyembe, Eng. Manyanya, Seleli na wengineo, tafadhali tuelezeni mnachokifahamu kuhusu Dowans kwa kulinda mali na maslahi ya Taifa letu.
Kila kiongozi wa jamii anatakiwa kusimama ahesabiwe kuhusu suala hili la WIZI wa MCHANA kulipa Dowans.