OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,191
- 103,715
Tanzania ni moja kati ya nchi ambayo haina mfumo wa "kuzaa,kukuza na kulea" watu wanaotegemewa kuwa viongozi huko mbeleni. Uongozi Tanzania ni zali na ukiacha ngazi za juu,hapa ngazi za katikati itategemea unaweza kujipendekeza kwa kiwango gani.
Kwa mfumo huu wenye nguvu hutumia ujinga wa Mtanzania kujipatia vyeo vya kisiasa,huku wakiwa wachafu,wanafiki,waliojaa visasi,waroho na makatili.
Ikumbukwe kwamba kuelekea uchaguzi wa 2010 kilianzishwa chama cha CCJ Chama cha Jamii,ambacho ilidhihirika kwamba ni cha waasi wa CCM. Pamoja na kuwa Ndugu Mpendazowe alitangulizwa lakini ikaja kubainika kwamba waasisi wa chama walikuwa ni Marehemu Samuel Sitta(RIP), Dr.Mwakyembe, Nnape Nauye na kijana Paul Makonda
Katika kipindi hiki cha kuanikana ndipo nimepata fursa ya kuwafahamu vizuri watu hawa na malengo halisi waliyokuwa nayo.
Fikiria jambo dogo tu,walianzisha chama kumkomboa Mtanzania au ni kutafuta fursa?Kama ni kumkomboa Mtanzania mbona walighairi baada ya kuahidiwa fursa????Yale madhira yaliyokuwa yanampata Mtanzania yalikwisha?
Mengi kuhusu Dr.Mwakyembe na Kijana Makonda sihitaji kuyarudia rudia,pia kwa bahati nzuri Mpendazoe ni mwanachama humu tunajua namna anavyojinadi kwa awamu ya tano,kiasi cha njano kuita nyeusi.
Je,fikiria kama chama hiki cha Sitta,Mwakyembe,Nape, Makonda na Mpendazoe kingeaminiwa na kushika madaraka tungekuwa tunaongozwa na watu wa namna gani
Watanzania muwe na utamaduni wa kuwafahamu vyema watu mnaotaka kuwapa uongozi,sio kufuata mikumbo tu.
MTAKUJA KUCHAGUA**********