Sitta kukutana na kardinali Pengo na Mufti Simba

Sitta kukutana na kardinali Pengo na Mufti Simba

usitegemee viongozi wa dini kufanya au kuwaza kwa namna sahihi kila siku, nao ni binadam, pili usahihi ni ule wa wengi kama kiongozi yupo upande fulan wa mawazo basi huko ndo sahihi kulingana na yeye, sasabasi kama pengo ameunga mkono serikali mbili basi hayo ndo maonao yake na yupo sahihi kama wewe unavyojiona sahihi na serikali tatu, yeye kuwa rafiki na serikali ndio kazi yake yeye ni mtu wa kila mtu na sio kwamba asiwe rafiki ya fulani kisa anatenda mabaya, UPENDO HUJENGA YOOTE hivyo urafiki ni upendo na kupitia upendo huo ataweza kuwabadirisha kama wanatend mabaya,
note: YOU HAVE TO BE THE CHANGE YOU WANT TO SEE IN THE WORLD
 
Kuna habari katika gazeti la Nipashe kwamba leo Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samweli Sita anakwenda kukutana na viongozi wa dini: Pengo na Mufti kwa nyakati tofauti.

pamoja na kwamba maudhui ya kikao chao hayajulikani bado lakini inaonekana ni kuhusu swala la serikali mbili au tatu linalolisumbua BMK.

kwanza kuna urafiki wa ghafla umeibuka kati ya Pengo na serikali na CCM. Hasa baada ya Pengo kuonesha kuunga mkono msimamo wa serikali mbili kinyume na maoni ya Baraza la maaskofu katoliki waliopendekeza serikali tatu.

Tumezoea mara zote kumuona muadhama akisimama mara nyingi upande wa wanyonge (wananchi) kuwateteta na ikafika mahali akadai anapewa vitisho ili anyamaze lakini akasema hata kama vyombo vyote vya habari ( Hat nyie wa Tumaini Media) vitakataa kuyaandika yale yalio kweli basi yeye hatanyamaza kusema. Ilifika mahali kukawa na kurushiana maneno kati ya serikali na kanisa kwa sababu ya kanisa kukemea uovu wa serikali kwa nguvu. Ilifika mahali wakaambiwa wavue majoho waingie kwenye ulingo wa siasa! Kisa kanisa kuikosoa serikali na chama chake.

lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida pengo ametengeneza urafiki mkubwa na serikali na chama tawala kiasi kwamba siku hizi hatumsikii tena akitoa yale maneno yake mazito ya kiunabii kuionya serikali. Zaidi sana ameungana na chama tawala kutetea maoni yao binafsi na kupingana na ukweli wa hali halisi na maoni ya wananchi wengi.

Kiongozi mkubwa kama pengo ndiye mtu anayetakiwa asimame kati kam arbitrattor wakati mabo yamekwenda kombo na pande mbili zinashindwa kukubaliana. lakini ameamua kuchukua upande katika yanayobishaniwa! Kwa hiyo leo hatuna tena wa kututetea wanyonge. CCM wanaweza kuamua kufanya wanavyotaka kwa sababu viongozi wa dini wanaowaogopa sana walishawaweka sawa. Hakuan asiyejua kwamba Mufti Simba ni CCM dam na analipwa na serikali.

Onyo: Sisi wkatoliki tunamtahadharisha tu kardinali Pengo kwamba kama amekubali kuungana na watawala kuwakandamiza wananchi wanyonge basi na ahakikishe anashikana nao kweli kweli kwa sababu tutaendesha kampeni kubwa katika makanisa yote ya Dar ili wagome kutoa sadaka ya mavuno ambayo ndiyo chanzo kikuu cha mapato ya kanisa. Serikali uliyoamua kuwa nayo upande mmoja basi na wakugharimie gharama za kuendesha jimbo na mapadri wako. Tunataka kanisa libaki katika nafasi yake ya kuteteta wanyinge na kusimamia haki na wala sio kukaa upande wa watawala.

Tumsifu Yesu Kristo.

Muslim hayatuhusu
 
Sidhani kama alikuwa anahaja ya kuwaona hao viongozi wa dini,alichotakiwa kufanya ni kuwatendea haki wote bila kujali itikado za vyama vyao au imani zao.

Alitakiwa kuargue kwa hoja na kuwapa nafasi hata wale wanaotaka serikali tatu kutoa mawazo yao ili mwisho wa siku tupate Katiba bora yenye maridhiano ya pande zote bila kuleta ulalamishi.
 
Kweli viongozi wana play role kubwa sana katika utulivu wa nchi... lakini kwa sasa hawakupaswa kushirikishwa baada ya rasimu ya pili kuwasilishwa... hawa wataharibu hali ya hewa soon asipoangalia...
 
Huyo Askofu anaitwa Ngalalekumtwa,Huyo Kalekekuntwa wako sijui umemtoa wapi!
 
Only one Solution:

CCM + UKAWA = Katiba Mpya ya watanzania.

Wasipoelewana hawa watu wawili, hata tukeshe tukisali Katiba haipo
 
jamani kama nia ni kukutana na viongozi wa dini kwan viongozi wa dini ni hao tu?
 
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya upum.bavu walio nao watanzania na viongozi wao wa dini!Kuna watu hata ukiwaambia walambe kinyesi watalamba tu ili mradi liwe ni agizo la kiongozi wa dini kwa hiyo unajisumbua bure tu mkuu kutoa tahadhari

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
MH. Samweli Sitta ,M/kiti Bunge maalumu la Katiba nafarijika kuona unahusisha watu walioko nje ya Bunge kuhakikisha Katiba inapatikana kwa Amani na utulivu Hili ni jambo jema sana, lakini kumbuka kuna baadhi ya watu tayari wana Makovu ya kudhalilishwa na baadhi ya wajumbe waliomo ndani ya Bunge lako ikiwemo Ikulu ambao ni Mh. Warioba na Mchungaji kakobe ,kumbuka Mungu ni yule yule anayesikiliza maombi yetu sisi sote wakiwemo warioba na kakobe, Busara zako zitumike kwa kupitia kwa hawa wazee nao watupe Baraka zao
 
Mr. 6 ukimaliza kufanya mkutano na hao nenda kwa;

Waprotestanti

Wapentekoste,

Waanglikana ,

Walutheri,

Wasabato

Waorthodoksi

Wamormoni

Mashahidi wa Yehova

Wahindu

Wausikh

Baha'i, n.k.
 
Kardinal Pengo anazidi kuweka pengo kubwa kati yake na Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania. Pengo amekuwa mwanasiasa sasa.

Tofauti kubwa tunayoiona kati ya ayadi Mwadhama Lugambwa na huyu Mwadhama Pengo ni kubwa.

Mwenye jukumu la kutolea kauli au kulisemea kanisa ni mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania ambaye ni Askofu Ngalalekumtwa wa Iringa, lakin Pengo anavyojitia kimbelembele, ipo siku ya Vatican yatamshinda, atulize mzuka hata kama Waziri Mkuu ni wa kutoka kumoja.

Atakachokiongea Pengo leo je ni kauli iliyotoka kwenye baraza la Maaskofu katoliki Tanzania au maoni binafsi? Kwa kanisa hilo maoni binafsi kwa kiongozi wa aina yako si jambo la kawaida maana wana utamaduni wa kuwa na msemaji mmoja anayetambuliwa ambaye amechagulia kwa kuongoza chombo hicho kwa kipindi cha miaka mitatu.
 
  • Thanks
Reactions: jme
Mkuu hili la kuwawekea vikwazo vya kiuchumi watumishi sio jema. Mwacheni Pengo awe huru kwa kile anachokiamini, mpingeni kwa hoja, na kama ni kweli wananchi wengi wana msimamo tofauti litadhihirika hilo kwenye kupiga kura.

Habari ndio hiyo akijimix tu watu nao watafanya yao!!!!!!
Viongozi wa dini wanakuwa ndumi la kuwili mchana kweupe, their days are numbered!!!!
 
Muslim hayatuhusu

Hayakuhusu vipi wakati na mufti wako yupo kwenye ratiba!!!!!

Mimi muislamu lakini nasema huu msimamo wa kutotoa sadaka unatakiwa iwe kampeni ya nchi nzima bila kujali dini mpaka viongozi wa dini wakae kwa yaliyowaweka hapo sio tunachimba mifuko wao wanaleta siasa kama wanataka siasa wakatafute majimbo huko!!!!!!!
 
Sita anaona gari linaenda hari jojo...anaenda kuomba msaada
 
Mkuu hili la kuwawekea vikwazo vya kiuchumi watumishi sio jema. Mwacheni Pengo awe huru kwa kile anachokiamini, mpingeni kwa hoja, na kama ni kweli wananchi wengi wana msimamo tofauti litadhihirika hilo kwenye kupiga kura.

Tulishampinga kwa hoja tukachagua serikali tatu, yeye asitumike kuchahachua mapendekezo ya wananchi walio wengi hata kama haungani nao kimawazo.
 
Back
Top Bottom