mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,152
Tamaa? Nina tamaa ya nini?Muadhama anapaswa kuangalia maslahi ya taifa sio yawatu wachache wenye tamaa kama wewe
Tamaa? Nina tamaa ya nini?Muadhama anapaswa kuangalia maslahi ya taifa sio yawatu wachache wenye tamaa kama wewe
Kosa kafanya mwenyewe kinyume na kanunu walizojitungia kwamba!; aanze kufungua ile hadhara JK kisha Jaji Warioba aje amalizie Sauti ya Wenye nchi! Hao hawatamsaidia bali anaendeleza uzoefu wake wa kukosea! Ni heri angepata ushauri wa Mtikila!Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba,Samuel Sitta Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, leo anatarajiwa kukutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, jijini Dar es Salaam. Kadhalika, Sitta atakutana na Mufti wa Tanzania, Sheikh Shaaban bin Simba, makao makuu ya Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata), yaliyopo Kinondoni. Tangazo fupi lililotolewa kwa vyombo vya habari na Idara ya Habari (Maelezo), jana lilisema kuwa kiongozi huyo wa Bunge atakutana na Kardinali Pengo leo saa 3:00 asubuhi na kisha atakutana na Mufti Simba saa 6:00 mchana. Tangazo hilo fupi halikufafanua nia hasa ya kiongozi huyo kukutana na viongozi hao wa dini. "Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba anatarajia kukutana na Kardinali Pengo saa 3:OO asubuhi St. Joseph na baadaye saa 6:00 mchana Kinondoni kukutana na Mufti bin Simba. Mikutano itafanyika jijini Dar es salaam," lilieleza tango hilo fupi. Hata hivyo, pamoja na kwamba tangazo hilo halikuweka bayana nia ya Sitta kukutana na Mufti pamoja na Kardinali Pengo; wadadisi wa masuala ya kisiasa wameeleza kuwa mwenendo wa Bunge la Katiba hasa mivutano isiyokwisha inayoendelea kwenye vikao bungeni itakuwa ajenda kuu ya kuwafuata viongozi hao. Tangu kuanza kwa Bunge Maalum la Katiba, kumekuwa na mivutano isiyokwisha kuanzia ile ya kura ya siri au ya wazi, iliyoibuka wakati wa kupitisha Kanuni za Bunge hilo kiasi cha kuafikiana kwamba kura zote mbili zitumike wakati wa upitishaji wa vifungu mbalimbali vya rasimu ya Katiba. Kadhalika, suala la kupitisha kifungu cha rasimu kwa theluthi mbili ya kura za wajumbe kutoka Zanzibar na Tanganyika pamoja na muundo wa serikali; ni masuala ambayo bado yanaleta mvutano mkubwa bungeni. Mivutano hiyo imezaa makundi ndani ya Bunge; kundi moja likiundwa kama Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambalo linatetea muundo wa serikali tatu kwenye Katiba ijayo na lingine likijiita Tanzania Kwanza, linalotetea muundo wa serikali mbili. Kundi la Ukawa linaundwa na wajumbe wa upinzani na kundi la Tanzania Kwanza linaundwa na wajumbe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM); na yamekuwa yakilumbana ndani na nje ya Bunge, kiasi cha kuyumbisha kiti cha Mwenyekiti. CHANZO: NIPASHE![]()
Wakatoliki sio wapumbavu kama wewe unaezani kutotoa dhaka na sadaka ni kumkomoa Pengo. kwa uandishi huu nakuomba sana ukatubu ndugu yangu la sivyo unaweza kupata matatizo makubwa au mtafute mchungaji wako akushauri juu ya ujumbe huu wa kujiandaa kukwamisha injili.
Ndiyo raha ya JF. Wewe kweli ni wa kumwambia Moshi hana akili? Unamfahamu?! Kwenye maandishi yake, ni kipi kinachokushawishi kwamba hana akili!Mungu kakupa mwili lakini kakunyima akili! kama pengo sio mwanasiasa mbona anakubali kuburuzwa na wanasiasa?
Malizia story, BAKWATA walichukua hatua gani baada ya Mkapa kupongeza?Amri zilitolewa kuwalenga shabaha walokusudiwa kwa kauli zilizosikikika Piga Yule, Piga shaba, yule piga shaba (rejea mkanda wa mauaji ya mwembechai wa ITV).
Silaha za moto zikarindima, Waislamu wanne (4) wakauawa pale pale na maiti zao zikaburuzwa na kutupiwa ndani ya gari la Polisi kama mizoga.
Mamia ya Waislamu wakiwemo wanawake zaidi ya mia mbili walijeruhiwa na kuwekwa mahabusu.
Baada tu ya mauaji ya Mwembechai, mkutano mkuu wa chama tawala, CCM, mwenyekiti wake akiwa Benjamini Mkapa, ambaye pia alikuwa Rais wa nchi, uliipongeza serikali kwa hatua iliyochukua Mwembechai.
Pia kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki, Polycarp Kadinali Pengo, aliunga mkono mauaji yale ya Waislamu akidai kuwa, askari wale walikuwa na haki ya kuwapiga risasi za moto kwa kuwa nao walikuwa wakiwatupia mawe.
Akajaribu kuhalalisha kwa kurejea kisa cha Nabii Daud kuwa jiwe nalo linaua kama Daud (a.s) alivyomuua mfalme Jalut kwa jiwe
Kuna habari katika gazeti la Nipashe kwamba leo Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Samweli Sita anakwenda kukutana na viongozi wa dini: Pengo na Mufti kwa nyakati tofauti.
pamoja na kwamba maudhui ya kikao chao hayajulikani bado lakini inaonekana ni kuhusu swala la serikali mbili au tatu linalolisumbua BMK.
kwanza kuna urafiki wa ghafla umeibuka kati ya Pengo na serikali na CCM. Hasa baada ya Pengo kuonesha kuunga mkono msimamo wa serikali mbili kinyume na maoni ya Baraza la maaskofu katoliki waliopendekeza serikali tatu.
Tumezoea mara zote kumuona muadhama akisimama mara nyingi upande wa wanyonge (wananchi) kuwateteta na ikafika mahali akadai anapewa vitisho ili anyamaze lakini akasema hata kama vyombo vyote vya habari ( Hat nyie wa Tumaini Media) vitakataa kuyaandika yale yalio kweli basi yeye hatanyamaza kusema. Ilifika mahali kukawa na kurushiana maneno kati ya serikali na kanisa kwa sababu ya kanisa kukemea uovu wa serikali kwa nguvu. Ilifika mahali wakaambiwa wavue majoho waingie kwenye ulingo wa siasa! Kisa kanisa kuikosoa serikali na chama chake.
lakini katika hali isiyokuwa ya kawaida pengo ametengeneza urafiki mkubwa na serikali na chama tawala kiasi kwamba siku hizi hatumsikii tena akitoa yale maneno yake mazito ya kiunabii kuionya serikali. Zaidi sana ameungana na chama tawala kutetea maoni yao binafsi na kupingana na ukweli wa hali halisi na maoni ya wananchi wengi.
Kiongozi mkubwa kama pengo ndiye mtu anayetakiwa asimame kati kam arbitrattor wakati mabo yamekwenda kombo na pande mbili zinashindwa kukubaliana. lakini ameamua kuchukua upande katika yanayobishaniwa! Kwa hiyo leo hatuna tena wa kututetea wanyonge. CCM wanaweza kuamua kufanya wanavyotaka kwa sababu viongozi wa dini wanaowaogopa sana walishawaweka sawa. Hakuan asiyejua kwamba Mufti Simba ni CCM dam na analipwa na serikali.
Onyo: Sisi wkatoliki tunamtahadharisha tu kardinali Pengo kwamba kama amekubali kuungana na watawala kuwakandamiza wananchi wanyonge basi na ahakikishe anashikana nao kweli kweli kwa sababu tutaendesha kampeni kubwa katika makanisa yote ya Dar ili wagome kutoa sadaka ya mavuno ambayo ndiyo chanzo kikuu cha mapato ya kanisa. Serikali uliyoamua kuwa nayo upande mmoja basi na wakugharimie gharama za kuendesha jimbo na mapadri wako. Tunataka kanisa libaki katika nafasi yake ya kuteteta wanyinge na kusimamia haki na wala sio kukaa upande wa watawala.
Tumsifu Yesu Kristo.
Hao viongozi wa dini wana maslahi binafsi.Hakuna hata mmoja aliyechukua maoni yetu ktk nyumba za ibada hivyo HAWANA UHALALI WA KUKUTANA NA SITTA JUU YA KATIBA
wewe na wakatoliki wapi mtagoma?? sema wewe utagoma siyo wakatoliki wote Nyerere alikuwa mkatoliki kindaki ndaki Mkapa naye hivyo hivyo Pinda na wengine kibao una uhakika wote watagoma kama wewe
Pengo asipokuwa makini Kanisa Katoliki litapasuka mapande. Katiba mpya ilijadiliwa sana kwenye Jumuiya na watu wameshatoa maoni yao. Kujaribu kugeuza mambo kipindi hiki kutazua balaa.
Naona CHADEMA hapo hujaitaja vipi yakhe? CHADEMA ndio mungu wako nini?