Sitta hawakutaki jiondoe mapema kwa heshima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitta hawakutaki jiondoe mapema kwa heshima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Najijua, Apr 12, 2011.

 1. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #1
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Napenda kumtahadharisha mzee wangu sitta kuwa ccm hawamtaki ni bora akijiondoa mapema kwa heshima kabla fedhea haijamkuta

  hii inathibitishwa na kutochaguliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu na wajumbe wa nec ili hali makuwadi wa mafisadi na rasilimali za taifa wakichaguliwa kwa kishindo. Mfano january makamba, zakhia meghji, abdallah kigoda na wasira.

  Waswahili wanasema baada ya dhiki ni faraja but hakuna faraja yeyote aliyoipata mzee wetu huyu hata baada ya kutoswa uspika, baada ya kutukanwa kule znz akiwa anawasilisha muswada wa katiba mpya na hata baada ya kuongoza mapambano ya muda mrefu dhidi ya mafisadi ambao leo hii chama chenye kina kiri kupoteza umaarufu kwa sababu yao

  mzee sitta karibu kambi unayostahili kulipo na wapambanaji wa ukweli na sio wasaliti kama huko ulipo
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Apr 12, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 326
  Trophy Points: 180
  Ili ubaki CCM salam lazima uwe mnafiki mkubwa na kuwalamba miguu mafisadi kilichofanyika Dodoma ni ulaji hakuna jipya
   
 3. k

  kilolambwani JF-Expert Member

  #3
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapana jamani, hapa Sitta, Mwakyembe na Gambo wameshinda vita dhidi ya ufisadi. Kelele zao zimesaidia kuwang'oa RA, EL na Chenge
   
 4. H

  Hekima Ufunuo JF-Expert Member

  #4
  Apr 12, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 220
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Si wote tuoliona kama unavyoliona wewe. Ingekuwa tunafanana kimtizamo basi Sita, Mwakyembe, Magufuli na Ole sendeka Wangechaguliwa na nec kuingis kamati kuu.
   
 5. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #5
  Apr 12, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Huoni kama ni jambo jema kwa Mzee6 kutokuwemo ndani ya kundi la wababaishaji hawa? Ikiwa JK kafanya kwa kufikiria amemtosa, kakosea kwani angelikuwemo kila anachotaka kusema ingelibidi "asubiri vikao halali". Kwenye siasa ndugu yangu, hasa za kitanzania, bora "utapike ukiwa nje kuliko ndani".

  Kuhusu kujiondoa, kila mtu na msimamo wake. Sitta anaweza mkombozi mkuu wa WaTZ hata akibakia ndani ya CCM. Yeye anauelewa ubovu na madudu ya ndani CCM kulikoni wengi wetu, kwa hivyo kubakia huko na kutoa nje matambara yao ni faida kwa WaTZ. Kwa upande huohuo, madudu hayo yakitolewa na waliomo ndani ya CCM ni hatua moja mbele kwa ukombozi wetu.

  Ni mawazo yangu, nawasilisha.
   
 6. H

  Happy mBISE Member

  #6
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Its true kabisa, bora ajiengue mapema kuliko aje kudhalilishwa , ipo siku tu
   
 7. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #7
  Apr 12, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Akufukuzae hakwambii toka. Mzee Sita jiondoe haraka ulinde heshima yako. Zanzibar umeadhirika hadharani unasubiri nini?
   
 8. Najijua

  Najijua JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 1,029
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mzee Sitta akutukanae hakuchagulii tusi, akunyimae kunde akupunguzi mashuzi
   
 9. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,497
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  Atoe aende wapi? Alikosea mwenyewe kwenye sakata la richmond; aliwaogopa na sasa wanaendelea kumsulubu.
  Hakuna tunakomuhitaji mtu mwoga. CDM inataka watu jasiri kama Slaa, Lema nk. siyo waoga kama 6!
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,271
  Trophy Points: 280
  HII NIMEIKUTA SEHEMU.

  CCM wamebadilisha sura za secretariet, wamebadili pia baadhi ya wajumbe wa kamati kuu. Hivi kumweka mkama nafasi ya makamba kunaleta nafuu gani kwa watazania? Hawa wote walikuwa ni viongozi wa CCM na Serikali yake kabla ya uteuzi wa jana. Mkama alikuwa katibu wa wizara ya afya miaka kadhaa akikumbwa na tuhuma kibao zilizohusu dawa ya ukimwi. Magazeti yaliandika sana tu. Chiligati alikuwa waziri wa ardhi. Hakufanya lolote zaidi ya kuharibu na kurudisha nyuma kazi nzuri aliyoanzisha magufuli katika wizara ile. Je, kubadili secretariet inawafaidije watanzania? Au itawasaidiaje CCM? Ina punguzaje mikataba ya feki kama IPTL. Je, itaibuka na kauli ya kutokulipa Downs? Itatoa tamko la kuridhia mabadiliko makubwa ktk mswada wa mabadiliko ya katiba yanayopigiwa kelele kila kona wakati mkiti wake ni Rais JK aliyeuleta mswada huo? Au kumtosa Fisadi mkubwa kuliko wote RA kwenye CC wakati mfanyakazi wake wa zamani/Swahiba wake ni waziri wa Nishati na Madini (Ngeleja) kwa kupigiwa debe na RA mwenyewe kunaleta jipya gani?
  HII ni danganya toto, tatizo la CCM ni la kimfumo, halibadiliswi kwa kubadili sura za watedaji.
  My take,
  Maisha bora hayawezi kuletwa na Chama kile kile, chenye sera zile zile kikiongozwa na Kikwete yule yule aliyeleta ombwe la uongozi ktk nchi yetu, eti kwa kubadili nafasi za baadhi ya viongozi na kuwa hadaa wananchi kuwa kimejivua gamba CCM kingali na sumu ile ile ya Ufisadi
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yaonekana kilichofanywa na CCM dodoma kimekuuma sana, pole mjukuu !
   
 12. L

  Lilombe JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mnyonge mpeni haki yake JK kathibitisha haya; MWANZO WA SAFARI HATUA! UKITAKA KUNG'OA MATAWI ANZA NA MIZIZI! HAO AKINA NGEREJA, SERUKAMBA, MGEJA, MAKONGORO, SOPHIA SIMBA etc. ni matawi tu, baba zao ni RA, EL na Chenge. Wewe jiulize akina Malisa na UVCCM yao wapo uvungu upi. Hivyo CCM tuwape shavu kwa kuthubutu kutoana. Nyie Watz hamna jema siku zote mlikuwa mwapiga kelele kuwa JK anawaogopa akina EL na leo kawatosa manasema hakuna jipya! Tuache ushabiki tuangalie maslahi ya nchi. ama kwa sababu mwajua kujijenga upya CCM ni threat kwa CDM???
   
 13. mamkhande

  mamkhande Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yani hawa wanatuchezea akili hakuna lolote,Jk kumuacha 6 wala hajamkomoa kwa Sera za CCM bora utapike ukiwa ndani kuliko nje utajuta
   
Loading...