Nakuunga mkono Mkuu. Sitta pamoja na unafiki wake na ufisadi lakini kwa kauli hii aliyoitoa ya kutetea maslahi ya Tanzania hastahili kabisa kulaumiwa. Imenishangaza sana kuona watu wanavyomshambulia Sitta kwa kauli dhidi ya malipo fisadi yanayotaka kufanywa kwa Dowans. Cha kushangaza wale ambao wamekaa kimya ndani ya CCM/Serikali kuhusu malipo haya hawashambuliwi hata kidogo. Watu kama kina Pinda, Membe, Magufuli, Hussein Mwinyi, Asha Migiro wamekaa kimya kabisa bila kutoa kauli zao ili Watanzania tufahamu wanasimama upande gani katika ufisadi huu lakini huyu aliyekuwa mstari wa mbele kusimama kuhakikisha malipo fisasi hayo hayafanyaki kabisa ndiye anaandamwa. Kwa maana nyingine wanamtaka anyamaze ili kurahisisha malipo hayo yafanywe haraka iwezekanavyo bila kuwepo pingamizi lolote lile. Tukumbuke malipo haya yalitaka kufanywa tangu January 2011 lakini kwa kelele za Watanzania mafisadi wakaogopa kuyalipa na sasa tuko October na mimi naamini kabisa kama Watanzania popote pale walipo pamoja na hukumu hii iliyotolewa bado tunaweza kabisa kuyasimamisha malipo fisadi haya yasifanyike na hivyo kuokoa mabilioni ya pesa za walipa kodi wa Tanzania na kuhakikisha pesa hii inatumika kwa maendeleo ya nchi badala ya kuingia mifukoni mwa mafisadi.
Hivi ni nani aliyeweka sheria kwamba ili kuipinga CCM na kuweza kufanikiwa ni lazima uwe nje ya CCM? Mwacheni Sitta apambane humo humo ndani ya CCM na kama wakitaka kumfukuza basi wamfukuze kama wanataka kuuwafukuza mapacha watatu inakuwaje wanashindwa kumfukuza Sitta ambaye amekuwa mstari wa mbele kutoa kauli ambazo mafisadi wengi ndani ya CCM hawataki kuzisikia. Tuacheni unafiki wa kumshambulia Sitta, inawezekana kabisa huyu Sitta naye ana mabaya yake mengi tu, lakini kwa kauli hii ya kupinga malipo fisadi kwa Dowans hastahili kulaumiwa kwa namna yoyote ile na Watanzania ambao wameweka mbele maslahi ya nchi ila sitashangaa kama akilaumiwa na kushambuliwa na wote wale ambao watanufaika kwa namna moja na malipo hayo ya shilingi bilioni 13 akiwemo Rostam, Al Adawi, Lowassa na wengine wote ndani ya CCM au Serikali ambao wanasubiri mgao wao baada ya malipo hayo kufanyika.
Tanzania inakizungumkuti chake cha kuwa na aina ya watu ambao wako tayri kumshambulia mtu bali kwa sababu ya kuwa yuko CDM na mwingine yuko CCM,au kumshambulia alie CCM kwa kua yeye yuko CDM.Na mchezo huu unaweza kuona kwenye timu ya TAIFA ambako kukiwa na wachezaji wa timu mbili za SIMBA na YANGA.Huwa kunaibuka uchafuzi wa wachezaji wa timu hizi mbili kuwa na maneno ya uchokonozi toka pande mbili kwa wachezaji kulushiwa madongo toka kila pande dhidi ya upande mwingine.
Kwa kiwango fulani TANZANIA limekuwa ni TAIFA kwa baadhi ya raia kupenda UNAFIKI na ujinga wa kushabikia madudu ya aina hii ya TAIFA la watu kuwa na ujanja ujanja wa kuliibia TAIFA na bado kuonekana kwenye jamii kama watu wnaostahiki pongezi kuwa walitumia akili nzuri na maarifa katika kufanikiwa kimaisha kumbe ni WIZI MTUPU.
Ebu angalia mtaani kwako mwanajamii ambae analitumikika TAIFA kwa uaminifu jinsi anavyopata shida kwa kumwagia kila aina ya matusi toka kwa wanafamilia wake na jamii kwa ujumla kuwa anachezea nafasi yake na yule mwingine aliye MWIZI kwenye shirika la umma ama chombo cha umma kuonekana ni bora na wakupigiwa mfano kuwa ndiye bora na ikibidi kuombwa na wanajamii kugombea nafasi ya uongozi kwenye ngazi ya jamii.
Hivyo swala la baadhi ya Wanajf kumwagia matusi na lawama kadha wa kadha SITA ni mzigo wa aina ya wale wale wanajamaii wanaowasifia wezi wetu kwenye jamii na kuwapa madaraka ili wawaongoze na kuwaondoa wale wote wenye kutenda haki.\
Siokuwa SITa hana mapungufu yake bali,tunaangalia mema ni yapi na mabaya yake yana ukubwa upi katika kipimo cha kumuona dhidi ya hoja zake katika kulipigigania TAIFA.
Yote ya yote uzuri wa Nchi hiii na Mama wa Nchi ni kuwa hatimae wezi wa TAIFA hili mwisho wake hata wao Uwa wanastaajabu jinsi wanavyoumbuka hakika uwa hawaamini imekuwaje kuwa kumbe wakati wanaiba au wakati wa matendo yao kullikuwa na watu wenye nguviu wa kuwaumbua lakini hawakufanya hivyo.Ukibahatika kukutana na mafisadi nina hakika ndani ya mioyo yao wanatamani WANGELUDI KUWA KAMA WATOTO WADOGO.Wanajaka moyo lisilo kwisha kwa kuwa ugeuka kuwa waigizaji wenye dukuduku kila siku na kuchezeshwa gwalide wasilolitaka,moja ya matokeo ya jaka moyo angalia wale waliokimbilia kwenye sura za makanisa au misikitini.Jaka moyo hilo ni kuanza kutafuta uwepo wa ufahamu wa UBINADAMU ambao hapo awari muhusika hakuwa nao.
Matendo ya KIFISADI ni zao la watu ambao kwa imani zao za ndani awari wakati wa matendo ya KIFISADI watendaji walikuwa hawana Moyo wala HAWAAMNI KAMA KUNA MUNGU,kwa kuwa wamekuwa na mamlaka ya kumilki mali na watu wanaowatumikia kiasi kuwa wanakufulu, na hawajitambui kuwa ni sehemu ya viumbe wa MUNGU kama wengine.
Inapofika kwenye hatua hii,basi kuna wale ambao taaratibu wanafunguka na kuona kuwa mengine pamoja na matamanio ya kumiliki mali bali kuna ubinadamu.HATIMAE WENGINE UFUNGUKA NA KUONA WATANGULIZE KIPI KATI YA HAY MAWILI KUWATUMIKA WATU [BINADAMU] NA SIO MALI AU WATUMIKIE MALI NA SIO KUWATUMIKIA BINADAMU.
Yote ya yote nae SITA atudhibitishie kwa kuweka msimamo wa dhati kuwa wakilipwa dowans anatoka CCM?