Sitta ajitosa mgogoro wa Umeya Arusha

Yale yale yaliyotokea Ikulu last week...

Hebu tutaona ila kama wamemtumia man of God kila kitu kitaenda sawa kama hawa watu wa magamba wanamwamini Mungu
 

Hilo nalo neno
 
Hapo kwenye nyekundu jamaa kangea point!
 
Huyu jamaa amefanya miradi mingi sana ya kanisa hilo. Lakini ni kama waumini hawakumbuki. Wanachokumbuka ni kwamba yeye ni sababu ya mauaji ya ndugu zao na wale waliopata majeraha na vilema. Ndio maana hawakumshangilia.

Anyway, baba Askofu amezungumza neno angalau wakapeana mikono! Ila damu zilizomwagika ni jinamizi litakalomwandama kwa muda mrefu sana!
 
Amebana ameachia. Ccm ni chama dume.
 
anachong'ang'ania ni kipi? Si aachie ngazi tu?
 
title na ulivyoviandika havishabihiani kabisa
Hata hivyo bado tunaombea sana amani ipatikane Arusha Kama alivyosema mkuu tatizo hata yeye halijui maana aliagiza wakae walimalize lakini kuna wachache kwa masilahi yao hawataki

Wa upande gani magamba cdm?
 

nilikuwa nimenuna siku nzima lakini post yako imenivunja mbavu.
 
Hapo Lema yuko sawa, kwani ujumbe wake unasisitiza kuwa amani ya kweli ni tunda la haki. Hivyo haki ndio itakayosababisha amani katika jamii. Hata neno la Mungu katika biblia linasisitiza kuwa 'hapana amani kwao watendao maovu'.
.
 
N series nashukuru kwa kufafanua!!Umenisoma kabisa !!
Wananchi wameshamkataa,angetoka tu!!Yeye sio chaguo la Mungu!!!
 
Exegate kidogo hichi kifungu cha mandiko. Tunashindwa kuelewa kwamba ni nani hasa alifunga hapa duniani ni wana wa Arusha au ni serekali ya CCM. Iliyomteua diwani huyo kuwa meya wakitumia kivuli cha uchaguzi geresha, a.k.a usanii wa kishamba.
:juggle:Acha kung'ang'ania lugha za watu wakati hujui hata unaandika nini. Tunashindwa kuelewa kwamba hilo neno (highlighted) kwanza ni lugha gani na pili linahusiana vipi na maelezo mengine yanayofuata. Tumia kiswahili, lugha yetu ya taifa ni nzuri tu.
 
Tumemuelewa, ni typo tu hiyo.
Sio lazima utumie kiswahili kwa kila neno, usiharibu topics za watu hapa!......
Hlo tu.:mimba:
 

Hizo lugha unazoziita ni lugha za watu, kwani wewe ulikuwa unataka lugha za nyani. Ujinga mzigo!!! Usicho kijua waachie wenye kuijua!!!
 
Mimi nilikuwepo na habari ilikuwa kama ifuatavyo , Mb Arusha mjini ( Lema) alipewa mic na Mh Sitta asalimie wananchi na kuchangia harambee hiyo na Bwana Lema , alimtambua Meya feki kama Diwani wa Olorieni na siyo meya huku akisisitiza kuwa yeye hana ugomvi binafsi na Meya isipokuwa mfumo uliompata meya unamfanya meya huyo kuwa katili wa haki za binadamu na utu .

Nukuu Lema " Mh Baba Askofu na mgeni rasmi mimi kama mbunge nitakuwa mtu waq ajabu kama nitashindwa kusimamia haki mbele ya madhabau hii ya Mungu na hivyo ukweli unabaki kuwa Arusha mjini hakuna Meya na mimi mbunge simtambui meya ila natambua uwepo wa Diwani wa Kata ya Olorieni bwana Gaudensi Lyimo.

Naomba ileweke kuwa mimi sina ugomvi binafsi na Bwana Gaudensi na hata akitaka kunywa chai kwangu namkaribisha sana isipokuwa nimuombe tena Mh Sitta kama mzee wetu kwenye siasa muda mrefu awaambie wakubwa wengine hasa waziri mkuu kwamba tatizo hili si afya kwa Arusha lakini hata hivyo hatutarudi nyuma kupigania haki iliyoporwa katika uchaguzi wa umeya na kama kuna mtu anakerwa na mgogoro wowote unaotafuta hakli basi yeye aendelee kukerwa na sisi kwetu ni baraka kwani haki tutaitafuta by the ballot or the bullet.

Bwana Gaudensi alivyotaka kumjibu Lema ndipo waumini wote wakaanza kumzomea Bwana Lyimo, na Mh Sitta akahaidi kusaidia mchakato wa mazungumzo yalioanzishwa na Bwana Pinda na Mbowe kufikia tamati kabla ya 2012.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…