Sitosahau nilipopokelewa na dragon nilipokwenda kwa mganga

tutuberti

JF-Expert Member
Apr 26, 2023
403
590
Daah, unapojidanganya unaujua ulimwengu huu basi kiukweli huujui kabisa au unaijua sehemu ndogo sana

Kuna siku nilikwenda kwa mganga na jamaa yangu ili nikamtengeneze mwanamke mmoja kwenye masuala fulani fulani.

Tulikuwa tunakwenda huko Bariadi ndani ndani na ilikuwa lazima tupitie ziwani na lazima iwe usiku wa manane. Nakumbuka tunapanda mtumbwi na mwenyeji wangu ananiambia nisijali tunaelekea Bariadi.

Hatujafika mbali mtumbwi ukapinduka juu chini, wote tukapoteza vitu kwakuwa vilizama, kuhamaki tunakunywa vikombe vya maji vya kufa mtu.

Nikajikuta natembea eneno nisilolijua, jioni kwa mbali naona ni kama nyumba zile za zamani sana, ghafla naona dude hilo mbele yangu bonge la dragon linapumua moto, ajabu moto ule haukuniunguza hata. Likanyosha mkono kunitaka nielekee mbele.

Nafika mbele nakuta mtoto mchanga akininyooshea kidole kuniashiria nikate kulia, jamani mambo yanatisha sana haya. Kufika mbele naona mtoto mchanga kasimama hacheki wala hatikisiki akionesha ishara nielekee kushoto.

Kufika nakaribishwa na kuelekezwa ndani ya chumba kimoja nipumzike. Asubuhi wakati wa jua kuchomoza nikajikuta nimelala kutandani mzima kabisa, nipo peke yangu na baada ya kuangalia mule ndani nikagundua palikuwa ni kwa mganga mwenyewe (jina naifadhi) na jana yake nilichoka sana.

Ajabu ni kuwa ,vitu vyangu vyote vilivyozama nilivikuta pale na nilikabidhiwa wakati wa kutaka kuondoka.

Ila nilijifunza vichache;

~ Hao watu wa ulimwengu huo wanafurahia mno baadhi ya watu wanavyodanganyana mambo haya hayapo. Wanafurahia sana na wanapenda.

~ Nakumbuka nilipewa sharti la kulala na tipwa tipwa fulani na nikapewa sharti la kutokojoa isipokua kwenye kopo maalum.

~ Njia ya kurudi ilikuwa ni ile ile na utaratibu uleule, ajabu narudi jamaa yangu namkuta mzima wa afya anacheka tu, kumbe jamaa naye ni mpana kwenye ilmu hii daaah!

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Unaendeleaje kwa sasa!? Mambo yako yalisovika?
Nasikia huwa wanasolve current problem lkn wanasababisha another problem.

For me hata iwaje kwa waganga no.!
Nitakomaa na imani yangu ya Mungu baba kupitia kwa mwanawake Yesu kristo.
 
Unaendeleaje kwa sasa!? Mambo yako yalisovika?
Nasikia huwa wanasolve current problem lkn wanasababisha another problem.

For me hata iwaje kwa waganga no.!
Nitakomaa na imani yangu ya Mungu baba kupitia kwa mwanawake Yesu kristo.
Nikiongea itaonekana naji promote mkuu.mm kifupi tu jamaa yangu alijua mchezo mzima na ishu yangu ilikua solved 100% kabisa

Sent from my SM-G800F using JamiiForums mobile app
 
Unaendeleaje kwa sasa!? Mambo yako yalisovika?
Nasikia huwa wanasolve current problem lkn wanasababisha another problem.

For me hata iwaje kwa waganga no.!
Nitakomaa na imani yangu ya Mungu baba kupitia kwa mwanawake Yesu kristo.
Kwa mganga utarnda tu kijana sema bado ujapambana na masibu ya ulimwengu vizuri. HATA mimi nilikuwa naongea na wewe ila ili niradhimu kufika kwa mganga.

Ni baada ya kaka yangu kuugua ugonjwa wa ukichaa yani mtu anakuwa chizi kabisa.Pambania mgonjwa hospital kwenye wodi ya vichaa karibu miezi kadhaa ila wapi.

Mwisho daktari mmoja akatuvuta pembeni akasema hapa mnapoteza muda kajaribu tiba za kienyeji na kweli tulienda kule na mgonjwa akapona kwa mara ya kwanza nilikanyanga kwa Mganga kusimamia show ya matibabu
 
Kwa mganga utarnda tu kijana sema bado ujapambana na masibu ya ulimwengu vizuri. HATA mimi nilikuwa naongea na wewe ila ili niradhimu kufika kwa mganga.Ni baada ya kaka yangu kuugua ugonjwa wa ukichaa yani mtu anakuwa chizi kabisa.Pambania mgonjwa hospital kwenye wodi ya vichaa karibu miezi kadhaa ila wapi.Mwisho daktari mmoja akatuvuta pembeni akasema hapa mnapoteza muda kajaribu tiba za kienyeji na kweli tulienda kule na mgonjwa akapona kwa mara ya kwanza nilikanyanga kwa Mganga kusimamia show ya matibabu
Vipi hukuulizia kuhusu ndumba za kutajirika?
 
Back
Top Bottom