Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Hii ni kwa hasara yako mwenyewe.
Hakuna aliyewahi kufunguliwa mashtaka
kwamba hajatoa sada kanisani/msikitini na ndo maana
inaitwa sadaka.Jitahidi ulipe kodi,hiyo usipolipa utakumbana
na vyombo vya dola.Ila ukumbuke serikali haina mbingu
ya kukupeleka ukiisha kufa. Wala hutakutana na mtu huko
mbele ya safari yako ukamuonyesha TIN namba yako.
ukitafakari haya utaelewa sadaka ni nini?

Si lazima kama umemuona yatima
au mjane upeleke sadaka kanisani afu ndo uwaambie wampe
unaweza kumpatia huyo mjane/yatima sadaka yako
na mbinguni ikahesabika.Saidia yatima walipie ada
wape nguo n.k na kanisani peleka sadaka kwa maendeleo
ya kanisa na kutunza watumishi. period.
 
Toa fungu la kumi wewe, utabarikiwa!!!!
Hivi fungu la 10 huwa ni lazima utoe kanisani? Huwezi kutumia hilo fungu la 10 kusaidia maskini, wajane, wazee, yatima na wengine wanaohitaji zaidi badala ya kupeleka kanisani?
 
Malaki 3:10 nakuendelea inaeleza vizuri sana. "Leteni zaka kamili gharani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo..... zaka ni fungu la kumi.
 
Sasa hivi hatuko kwenye sheria za Musa bali za Kristo.
Nioneshe sehemu iliyoandikwa maneno hayo ndugu! Yesu alimshinda shetani kwa kutumia agano la kale, na agano la kale ndo ina ahadi za parqdiso ya milele (Isaya 58-66)
 
kweli kabisa wachungaji wengi ni wasanii tu wanataka sadaka ,mimi tokea 2010 niliacha kutoa sadaka najikusanya kila wiki naenda kutoa kwawazee wasiojiweza na mayatima
Hayo unayofanya si maagizo ya Mungu (Malaki 3:8-10). tatizo ni kutojua ukweli, tafuta maarifa ya Mungu utapata neema yako, kutoa Sadaka na Zaka ni agizo la Mungu kurudi kwake aliyekupa, hutumika kulipa wachungaji (walawi kiBiblia) na kueneza injili ya Kristo na kusaidia wahitaji. karibu Seventh Day Adventist Church (the bride of Jesus Christ)
 
That's why i will remain a Roman Catholic for life!
Unamkuta pastor ana hummer complete with security detail (bodyguards) plus a helicopter wakati ata jengo la kanisa hana waumini mvua yao jua lao!
KWELI JAMANI???!!!!
soma Biblia ndugu, RC wamechakachua AMRI za Mungu, wameodhi mamlaka za Mungu (kusamehe dhambi), kubadili majira ya Mungu, kufundisha mapokeo ya wanadam badala ya neno la Mungu! RC HAWANA TOFAUTI NA WALA ZAKA NA SADAKA za wanyonge hawa wanaolalamika humu!
 
Hahaaah unanikumbusha sikumoja nilienda kwa mzee wa upakoroko ,daaaa nililojionea !!!!nikastaajabu huyu Mungu wakweli kwanini anachezewa?kwanini asimuadhibu tapeli yule?
 
Yaaani ww na umri huo ulidhani pesa hizo za sadaka anafanyia nn? Ulijua anampa mungu kwa njia gani? Endelea kumnufaisha tuu na ww baki maskini.
 
Hapa akina GWAJIMA, NDEGI, MZEE WA UPAKO, MWINGIRA, KAKOBE na NGURUMO YA UPAKO, etc Inawahusu hii!
 
Kusomewa mapato na matumizi kanisani kwako iwe rc au kwingineko hautakuwA na maaba yoyote kama hakuna Usafi na utakatifu watakusomea mapato na matumizi sawa ni vizuri he utapata nini zaidi ya kwenda motoni kwa ajili ya kuongozwa na kipofu?
 
Ur truly a great thinker
 
Wana kila mbinu ya kuhakikisha sadaka lazma utoe tu.
Kwanza kutoa kwa kila bench, ivo utaona aibu mwenyewe kukaa tu wakati wenzako wameinuka.
Pili michango ya kinanda, ujenzi wa ofisi etc
Tatu siku izi wameanzisha utaratibu wa kutunzwa madhabahuni.
Mama Rwakatale kwake fungu la kumi la mwaka mzima unatoa mwanzoni mwa mwaka, ili hata ukihama mji, hatakua na cha kupoteza etc.
 

Yesu amesema watu watangaze neno bila kutaka ujira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…