Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Mambo ya sadaka huwa yananifadhaisha sana hasa nikikumbuka tukio moja huko nyuma nikiwa kijana mdogo sana yaani teenager around 15 hivi.

Nilienda kanisa fulani hivi la mchungaji maarufu sana hapo jijini kanisa lake lipo ubungo.

Sasa ulipofika wakati Wa kutoa sadaka nikajongea kwenye mstari .Kumbuka sikuwa na kazi wala kipato chochote na nilikuwa mwanafunzi tu Wa sekondari .

Nilikuwa Nina sh.200,tu mfukoni na sikuwa na pesa nyingine na nilidhamiria kuitoa hiyo kama sadaka tu.

Sasa kufika mbele pale kuna mzee Wa kanisa ndo kqshika mfuko ambao unatumbukiza sadaka yako.

Kama unavyojua si vizuri sadaka kila mtu aione niliificha na kwenye mkono nikafika na kutaka kuitumbukiza mule kwenye mfuko daaah

Si yule mzee akadaka mkono wangu akaufungua mkono na kuiona hiyi 200 hahhahaahhah akanifukuza tokaaa!! kwenda huko .

Nikabaki najiuliza huyu mzee vipi je alitaka niweke kiasi gani hahahhahah.

Daaah tangu siku hiyo sina hamu nao hawa akina "nabii na mtume"

Nikaja kugundua kumbe wenzetu wanawekeana minimum amount ya sadaka sio kile ulichonacho ulichopewa na MUNGU.
 
SERIKALI INAVYOKUSANYA KODI UNAJUA ZINAFANYIWA NINI?
serikali ni serikali hakuna uhusiano na mambo ya dini(makanisa),nilisema siwezi kutoa fungu la kumi ni bora nikasaidie yatima na wasiojiweza kuna mtu hapo juu ameni-quote ameniambia hizo zaka zina maana yake. nauliza tena hizo zaka zinafanyiwa nini uko makanisani????
 
Wewe ulitaka ale nani?
Kama yeye amekupandia vya rohoni
Lazima nawe umpandie vya mwilini

Wewe inaonekana ulikuwa mkono wa birika
Wanaojitoa tunaziona Baraka tena kubwakubwa.
 
Wewe unaenda kutoa sadaka Makanisa ya Kilokole unategemea nini..??

Makanisa yanayojielewa kama Katoliki, KKKT na Anglican ni mahala pa kutoa sadaka...Maana huko Mashule, vituo vya watoto yatima, hospitali zinajengwa..
Nao wezi tu kazi kukarabati nyumba za paroko na kununua sehemu za parking na kuanzisha frem.faida inaenda kwa papa
 
Itafika wakati itafahamika IPI ni dini yakweli na zipi ni dini za uongo na utaperi,,,,,,,tuombe mungu atupe umri tu
 
Nawe buni mradi wako ukusanye sadaka.Juzi nimemsikia jamaa yangu kawa mchungaji wqnajiita manabii.Anajaza watu balaa mie namjua in and out.Nimeshangaa kuona jamaa kakusanya watu kiasi vile ninatumaini atakuwa milionea muda si mrefu
 
Na wao huwa wanasema kuwa sadaka lazima itolewe madhabahuni, hao mayatima na ombaomba pamoja na wagonjwa hawana madhabahu hivyo hawana uwezo wa kupokea sadaka ila wanachopokea ni misaada tu,TAFAKARI.............
 
You are definitely not one among us, go to hell..and let satan serve you for dinner..so long the devils son...
 
hahaahaaa baadhi ya makanisa na wachungaji wapo kimaslahi zaidi niliwahi kushuhudia kanisa moja mchungaji anakusimamia ukatoe sadaka ole wako ubaki kwenye kiti lazima atakufukuzia nje na kunakiwango kimewekwa katika utoaji wa sadaka na zisiwe za sarafu du nikajiuliza hili ni kanisa au mradi wa mtu
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
Mnatoa sh ngapi mpaka zitoshe kununua magari yote hayo?
 
Back
Top Bottom