Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini?

1 Wakorintho 9 : 11

Umeona mkuu, rudi utoe kwa moyo sasa
 
Na hizo sadaka mlitoa kwa mkupuo?
By the way, aliyeko madhabahuni atakula madhabahuni.


Na neno lipo kabisa

Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu?

1 Wakorintho 9 : 13
 
Cha msingi ni kwamba wewe endelea kumuamini mwenyezi Mungu na kutoa sadaka yako kwa kadri ya imani YAKO, na HUSIANGALIE MANUFAA YA MTU AU MCHUNGAJI KAMA ANAENDA KINYUME MWENYEZI MUNGU ATAMUADHIBU SIKU YA MWISHO KADRI YA ALIVYOITENDEA HAKI IMANI YAKE.
 
Hapo ndio nachokaga, ule msemo kuwa kila mtu atakula kwa jasho lake wote tunaukubali, pale kanisani anaetokwa na jasho wakati wa mahubiri na maombezi ni nani? Mchungaji.

Sasa mbona akila sadaka inayotokana na jasho lake mnakerekwa?

Acheni hizo aiseee.
 
Natumaini wote ni wazima wa afya tele,dukuduku langu ni kuhusu utoaji sadaka makanisani nilikuwa nafikiri % kubwa ya sadaka tunazo toa zinaenda kusaidia mayatima,wajane na wasiojiweza na kueneza neno la Mungu kumbe sivyo ninafikiri sadaka zetu sisi zinawanufaisha wachungaji uku waumini tukiwa choka mbaya,kitu kilichonisukuma nisitoe sadaka ni baada ya kumuona mchungaji wetu kununua magari 3 kwa mkupuo.

Mwezi 4 alinunua LAND CRUISER V8,mwezi 5 akanunua TOYOTA BREVIS,juzi kati mwezi huu wa saba nimemuona mtoto wa mchangaji yupo ndani ya BMW mpyaaa.Nimejiuliza sana huyu mchungaji amepata wapi pesa ya kununua magari yote kwa mkupuo hivi? Jibu nililopata ni sadaka zetu ndizo zinazomfanya mchungaji atanue anavyopenda,waumini masikini choka mbaya kumbe tunamfaidisha mchungaji na familia yake.

Kuanzia leo sitoi tena sadaka wa mchango wowote ule ni heri ni dundulize hela mwisho wa siku nikawasaidie yatima na wagonjwa mahospitalini kuliko kuzidi kuwanufaisha wachungaji.

Asanteni nawatikia EID njema
pole umechelewa kuujua ukweli.mi niliacha toka mwaka 1998 mkuu huwa ninahudumia mayatima,wazee na wajane kwa mtindo wa kipekee nilio jipangia
 
Suluhisho na wewe kasomee uchungaji upate magari au chopa kama Gwajima na Geodave ili ufidie sadaka zako kutoka kwa waimini utakaowaona wajinga kama ulivyokuwa wewe !!!
 
Ainisha kanisa lenu usilete umoja katika wingi. Unategemea kanisa lenye jina kama church of christ the king liwe na substance kwa jamii?
 
we kwani sadaka unayo toaga ina zidi 10000 hadi una lia lia apa
 
Cha msingi ni kwamba wewe endelea kumuamini mwenyezi Mungu na kutoa sadaka yako kwa kadri ya imani YAKO, na HUSIANGALIE MANUFAA YA MTU AU MCHUNGAJI KAMA ANAENDA KINYUME MWENYEZI MUNGU ATAMUADHIBU SIKU YA MWISHO KADRI YA ALIVYOITENDEA HAKI IMANI YAKE.
ni sawa na kumpa ada mtoto kisha akala, ukampa tena akala, ukaendelea kumpa kisa target yako ni shule. sadaka inatakiwa kufanya kazi ya mungu si anasa za mchungaji.
 
Sadaka ni katoliki tu ( japo nao wameanzisha sadaka ya pili )
 
Huo ndo mshahara wa mchungaji,endelea kutoa sadaka usifikirie hayo
 
Una Hoja Mleta Mada Ila Jaribu Kuchunguza Kwanza ....... Yani Ufanye Kama Research Katika Kanisa Lako Sadaka Zinaenda Wapi... Maana Makanisani Wanaingia Watu Tofauti Tofauti.. Kuna Mwingine Ni Miweka Hazina Ila Anafanya Kazi BOT huko.. so Usije Ukamuona ana Prado Ukaswma Ni Sadaka Zetu . Mchungaji Naye Mchunguze kama ana Kazi Nyingine Tofauti

Maana Taratibu za Makanisa Sadaka Huwa Zinatangazwa Na Matumizi yake sasa Labda Hilo kanisa lenu

Ingawa Sadaka Maana Yake Umetoa Htakiwi Kuangalia Nyuma.. Atajuana na Mungu wake anayeitumia Sadaka Vibaya
Mchungajia ana kazi gani nyingine ya kuweza kununu V8,BREVIS,BMW ndani ya miezi micjache hivyo?????
 
Nakuunga mkono ndugu.. Kuna baadh ya makanisa haya wanata ya wokovu mpaka sadaka unapangiwa utoe sh ngapi.. Je ndo yesu alivofanyaga?? Wenye sadaka kubwa wanakaa mbele nyie makapuku nyuma... Kumuona mchungaji mpaka ulipie kwa mfano kuna mmoja anajiita nabii et kumuona afanye maombez hapo ni 250000/= tsh na ushahid ninao.. Yan sa hv makanisa haya ya wokovu yamekua ni ujanja ujanja tu.. Rudi kwenye kanisa lako la awali ndgu.. Hawa mtume na nabii ni wengi na ni wapigaji tu.. Binafsi makanisa hayo nilishayakimbia.. Tatizo wakristo tunafuata miujiza na sio neno la Mungu.. Tunatafuta miujiza na hatumtafuti Mungu...
Japo mie muislam,ila nilishawahi kushuhudia waumini wanalalamika kuwa wamepangiwa kiasi cha sadaka niliwaza sana ila leo ndiyo nimepata jibu.

[HASHTAG]#tena[/HASHTAG] wao usikoa unakuwa upande tofauti na wasiotoa na unaulizwa nawewe unaahidi utatoa lini.
 
Kwani ulitaka hizo pesa afanyie nini wakati mnampa wenyewe kwa mapenzi yenu, au ungerizika ukimuona anazidi kupauka na sadaka mnatoa
 
Back
Top Bottom