Sitokuja tena kutoa sadaka kanisani

Makanisa yanasajiliwa kama taasisi. Ili usajili kama taasisi ni lazima ufuate na kuzingatia vigezo na masharti likiwemo sharti la kuwa na bodi ya wadhamini. Kimsingi hakuna kanisa la mtu mmoja.

Kaka ...
nenda kwa lakatware au mwingira uone kama kuna kutangaziwa kuwa sadaka ya last week ilifanyiwa nn na imekwenda wapi. hiyo inaamanisha kuwa ni ya mtu mmoja na hajibu kwa mtu yyte na ndio maana hana muda wa kuwaambia jinsi alivyotumia hela zenu
 
Unafanya vyema. Naomba unioneshe mstari wa Biblia unaokufanya usitoe sadaka ila ufanye hayo. Bwana Yesu mwenyewe anasema uzeni mlivyonavyo mtoe sadaka.
 
Kuna lecturer wangu aliapa kutotoa fungu la 10 mpaka anakufa.

Ni noma.
 
Sasa hivi hatuko kwenye sheria za Musa bali za Kristo.
 
kweli kabisa wachungaji wengi ni wasanii tu wanataka sadaka ,mimi tokea 2010 niliacha kutoa sadaka najikusanya kila wiki naenda kutoa kwawazee wasiojiweza na mayatima
 
That's why i will remain a Roman Catholic for life!
Unamkuta pastor ana hummer complete with security detail (bodyguards) plus a helicopter wakati ata jengo la kanisa hana waumini mvua yao jua lao!
KWELI JAMANI???!!!!
 
 
 
toa mkuu ukianza kufatilia vifungu vya biblia vinavyozungumzia sadaka ni vi vingi unavyoambiwa utoe sadaka maneno yanatoka katika kitabu kitakatifu
 
Mchungaji ana gari hummer 3

Ana helicopter kisha bado anahimiza kutoa na wewe unatoa heri mkuu umesoma alama za nyakati
 
Toa fungu la kumi wewe, utabarikiwa!!!!

Je akiamua fungu la kumi kumpa masikini mwenye kuhitaji chakula, dawa au mavazi badala ya kupeleka kanisani ili mchungaji afanye matanuzi amekosea nini? Kwa nini upeleke fungu lako kanisani wakati jirani yako yuko mahututi na hana dawa ya kumtibu?
 

Mkuu nakupongeza sana kwa kuanza kutumia akili yako vzr
 
Mkuu huwa unatoa sh ngapi kama sadaka kila uendapo kanisani? Ni vizuri kujiridhisha kwanza chanzo cha pesa ya kununulia magari hayo!!!
 
sadaka siyo lazima umpe mchungaji,kama kuna waumini wana hali duni ukawasaidia naamini mungu ataipokea sadaka,sio umpe mchungaji alafu ndio unaomna mara kannunua gari jipya sijui sijui kanunua bajaji,hiyo unayompa ni pesa,matumizi ya pesa c unayajuwa?
 
kanisa gani hilo sadaka kubwa kiasi hicho? watu hawatoagi sadaka kubwa kiasi cha kununua magari ya thamani kama hayo kwa muda mfupi. pesa za magari hayo labda ni msaada kutoka mahali au dili fulani limechezwa ila sidhani kuwa ni sadaka.
 
Kwani hiyo sadaka unamtolea nani? Mpe kaizari ya kaizari mengine achana nayo kwani umeshatimiza wajibu wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…