Sitokaa nirudie katabia ka kutongoza demu aliyekosea namba

Sitokaa nirudie katabia ka kutongoza demu aliyekosea namba

Kitambo mwaka 2014 nilikosea number nika mpigia simu huyo mdada aka niambia wrong number bas nikaomba samahani nika potezea,kesho yake akanza ni tafuta mara ani sms mara ani call mambo yakawa hivo aka niambia yuko moro muda sio mrefu atakuja dar nika mwambia karibu maana nilikuwa nimepanga zangu geto maeneo ya pugu...siku ana kuja akasema nauli imepelea mzee mzima nika mtumia buku kumi akasema kaipata ana anza safari ,muda huo geto natoa kitu (napika) nika wambia washikaj tule kiasi chakula kingine tumwachie shemeji yenu watu sawa sawa bwana ehee akafika ubungo aka nipigia nija mwambia tukutane jeti ana sauti nzuri kwenye simu.Akili ika ni cheza sikutaka kutoka mwenyewe kuna jamaa yangu nika mwambia tuongozane wote kumpokea huyo mgeni mweheeee mweheeee.....nilicho kiona nikaishiwa pozi simu nilimpa jamaaa yangu apige ajifanye ndo mimi alafu mim nikajifanya nime msindikiz jamaaa demu akaja had hapo mdada mtu mzima sanaaa ana kwa haraka haraka ana cheza miaka 30 alikuwa na ndevu sana kifua usipime jamaaa akazuga tuna kuja kuna mzigo tunapelek kiwalan twaja tuli rudi tena demu ali maind sanaaaa kwenye simu uzuri dar alikuja kw dada yake
Dah mkuu story yako inataka fanana na yangu . hâta mie hapo ubungo karbu na tanesco stendi ya zamani ya daladala tulikutana nae nikiwa na ndugu angu ila alikuwa bonge la kimeo ila saut zaid ya Wema sepanga. Tulipiga story kidogo tukamuambia tumeagizwa sehem tutakutafta kesho. Ila ndugu angu alikuwa ananiambia ni kamkwichi kwichi hâta kama kimeo tufidie nauli yetu maana tulitoka mbagala[emoji3] [emoji3]
 
Mwaka 2009 baada ya paper la form two nilikutana na jamaa yangu aliyekuwa na simu yenye dk 60 za voda. Sasa zile kutokana na kutokuwa na wateja wa kuwapigia tukaanza mchezo wa kibuni namba. Namba ya kwanza alikuwa ni Hassani wa Tanga( huyu tulimwbia tumekosea namba). Wapili Ezdola ila alikuwa na mapozi sana( tukampiga chini). Watatu ni Atu wa Tukuyu (kisa kinaanzia hapa). Jamaa akawa kila siku wanaongea nae, anaunga bando na kuchati nae kwa SMS na kumpigia( alikuwa na saitu nzuri sana). Walifikia mpaka kutambulishana kwa ndugu na jamaa( binti anawapa simu marafiki na wazazi waongee na jamaa, na jamaa vivyo hivyo). Sasa siku moja ilikuwa binti anakuja Mbarali kijiji cha karibu na kwetu kwenye sherehe. Jamaa wakawa wanawasiliana na jamaa akamwambia binti amkute karibu na kanisa na binti alitii akatangulia. Kwakuwa hawajuani na masuala ya WhatsApp hayakuwepo kabisa, basi jamaa akanambia tuende tukamuone Shem. Kufika karibu na kanisa jamaa akampigia sim na kuiweka mfukoni. Tukamuona binti anayepokea simu maweeeeeeeeeeee ni black-bongelized women with single-mother characteristics. Jamaa alichoka, Mimi nilicheka sana na jamaa muda huo huo akazima simu na tukarudi jamaa akiwa full stressed. Siku zilizo fuata jamaa alimwambia mwenzake Mimi nilikudanganya nina mke na pia nipo Mwanza ila huko ni kwa ndugu tu, ikawa mwisho wa Wrong number relationship
Pole aisee mimi kwa njia hiyo nilipata dem mkali mpaka leo namgegeda ingawa ameshaolewa.
 
Dah mkuu story yako inataka fanana na yangu . hâta mie hapo ubungo karbu na tanesco stendi ya zamani ya daladala tulikutana nae nikiwa na ndugu angu ila alikuwa bonge la kimeo ila saut zaid ya Wema sepanga. Tulipiga story kidogo tukamuambia tumeagizwa sehem tutakutafta kesho. Ila ndugu angu alikuwa ananiambia ni kamkwichi kwichi hâta kama kimeo tufidie nauli yetu maana tulitoka mbagala[emoji3] [emoji3]
Ha ha ha ha ogopa sana kukutana na kitu kiko nje ya matarajio asume mkuu unaenda kula mzigo msichana humjui kumbe ana mapepo ana kupandishia ahaaaaa ndgu yako katisha demu uliendelea wasiliana nae
 
Ilishantokea, ikabidi nimsaksie mshikaji wangu nliekua naye tukabadilishana majina akaongea nae mi nkawa mskilizaj tuu baadae akamtema, hiv ndivo tunavoish town kwa mara ya kwaza nenda na mtu kuepusha soo lawama zkahamia kwa mshikaj wangu
 
Hahahahaha

Mimi sijawahi kuangukia pambaya aiseee!!

Kila anayekoseaga namba nikikutana nae huwaga ni kifaa
 
Habari kwenu wanajukwaa. naenda direct kwenye ajenda

Mwaka 2010, nilikuwa nasoma chuo flani Arusha. Kuna siku sms iliingia ya "tafadhali nipigie", bila hiana nikapaa hewani nikampigia.

Alipopokea nilisikia sauti nyororo ya binti nikamuuliza nani mwenzangu? Akajibu anaitwa {jina}. Katika mahojiano nilipoteza lengo la alichokuwa anakitafuta tukaanza kuchat.

Zoezi likawa la kila siku, bahati nzuri yule binti alikuwa ni wa ar palepale. Siku moja tukapanga kuonana, mambo yakaenda kama tulivyopanga. Siku hiyo ilikuwa ni wkend, sehemu tuliyopanga kuonana ilikuwa ni garden moja {jina} ambapo wanafunzi wenzangu wanapenda sana kwenda pale kurefresh.

Nilitangulia mimi kukaa, na kumsubiri kwa hamu kubwa na ikibidi nikafanye kwichi kwichi. Ikawa washkaji wakija nilipokaa nawajibu leo shemeji yenu anakuja wakakae sehemu nyingine.

Hawakuwa na kinyongo washkaji zangu. Muda ulipofika nikaenda kumpokea..... kwa kweli MUNGU ANISAMEHE,,,, SAUTI ZILIKUWA HAZIENDANI NA UHALISIA.

NILIAHIRISHA KILA KITU SIKU HIYO, Mbaya zaidi washkaji wengi walikaa kwa mbali waone kifaa,, sikuonekana chuoni wiki nzima, baadae ilibidi niwe tu muwazi kuwa nilikuwa simjui ndo nimemuona siku hiyo.

Tulikuwa tunachat tu kabla
hahahhah
 
Sasa wewe mbona issue yako ilikua ndogo sana........[emoji69] [emoji69] [emoji69]
Mwenzio haya mahusiano ya mbali na kuonana kwenye picha, yaliwahi sababisha nikaenda kumpokea mtu airport, na alipo shuka kumbe kiwete.......[emoji134] [emoji134] [emoji134] [emoji134]
Kilicho tokea naomba nisikiseme...
[emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
 
Binamu yangu aliniunganisha na huyu mkaka yuko serious anatafuta mke, nilipatiwa profile ya jamaa PhD holder ndiyo amerudi kutoka unyamwezini na ndiyo ameanza kazi mkoani. Tulianza kuchat na mkaka Ikawa kawaida kila siku lazima zile za 'morning'' na 'good night babe' si nimepata mchumba.

Baada ya miezi kama miwili ya mawasiliano akaniambia anakuja Dar na angependa kufikia k wangu. Wakati huo hakuna smart phones ikumbukwe. Siku nilifika airport kumpokea mgeni wangu miguu iliishiwa nguvu. Uchumba uliishia pale.
Tehteh kisaaa [emoji3][emoji3]. Malizia basi kwanini ulimkaushia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom