Sitokaa nipende shombe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sitokaa nipende shombe

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Don, Apr 3, 2012.

 1. The Don

  The Don JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 3,455
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  Nakumbuka ilikuwa mnamo mwaka 2007 Ndipo tukio hili la kufedhehesha lilipomtokea ndugu yetu wa karibu,kwa jina mangi toka moshi(samahan cyo mangi wa jf) akiwa na umri wa miaka 26,alikuwa ndio kwanza kamaliza mwaka 1 katika kampuni fulani moro akiwa kama meneja mauzo alipoajiriwa baada ya kutoka chuo kikuu, katika kujishughulisha ndipoa alipofikia matombo na kukutana na huyu mtoto mchanganyiko wa rangi ya kibantu na kiarabu na umbo la kuvutia pasipo kasoro ya kuitwa mrembo,baada ya kuvutiwa nae ndipo alipoamua kumfunulia moyo wake kwa jinsi alivompenda,lahaula!

  Mungu si athumani bibie akamkubalia lakini kwa masharti ya kuingia kwenye ndoa na kubadili dini, mangi kwa kupenda bila hiyana akakubaliana na masharti na vigezo na taratibu za kutambulishana ili kufunga pingu za maisha zikaanza, mangi akarudi moshi na kuwaeleza ukweli lakini bahati mbaya wazazi wakawenga ngumu baada ya kuambiwa ni shombe na lazima abadili dini (watu kama hawa wanaitwa chasaka kwa chagga).

  mangi akaumiza akili ili aweze kupata lile tunda lake la maraha linalompeleka kuteseka na kuona pesa na cheo chake si thamani kitu, mangi aliamua kurudi moro na kumwelezea rafiki yake wa karibu hali halisi ndipo aliposhauriwa wacheze mchezo wa kimjini mjini ili waweze kumpata mutoto.

  Waliamua kwenda kukodi wazee wa mjini na kwenda nao huko matombo kwa mbwembwe nyingi wakitumia gharama kubwa ya msafara mkubwa wa magari na vitu vingine vya gharama kwa ajili ya wakwe, baada ya kupokelewa walitajiwa gharama ya mahari millioni 3 ambapo zilitolewa na wakaafikiana taratibu za kufunga pingu za maisha, haraka kamati iliundwa na taratibu zikaanza ambapo mangi aliulizwa mfukoni ana kianzio cha sh. Ngapi?

  Mangi alitoa kianzio cha millioni 4 pamoja na wanakamati ikafika millioni 22, hatimaye siku iliwadia ndipo msafara ukatoka moro mjini mpaka matombo kwa minajili ya kufungishwa ndoa, baada ya kufungishwa ndoa ndipo mangi alikabidhiwa mke na safari ikaanza akiwa na jina jipya la bin-mangi na mke,

  Baada ya kufika mjini na sherehe kumalizika ndipo walisindikizwa tayari kwa ajili ya mapumziko, wakiwa chumbani ndipo vituko vilipoanza pale bin-mangi alipotaka haki yake ya ndoa, mkewe alisingizia anaumwa na tumbo na hataki usumbufu, bin alivumilia na hatimaye usiku ukapita akiwa na mawazo mengi (kumbuka ndio kwanza alijua atapewa mchezo kutokana na masharti aliyopewa hapo mwanzo kuwa hadi ndoa).

  Kesho yake baada ya kuamka ndipo hali ilizidi kuwa mbaya na kuamua kwenda hospital kupima lakini hamna tatizo lililoonekana, baada ya kuzunguka sana ndipo alipopigiwa sim na wakwe zake wakimtaka mtoto wao wakamtibu kijadi wakiambatanisha na gharama ya sh. Laki saba.

  Bin alijikakamua na kuamua kuuza gari yake ili akamtibu mkewe kipenzi,wakwe walimwambia wanakwenda tanga kwa matibabu zaidi, kisicho riziki hakiliki pesa iliisha wakiwa tanga na bibie bila afadhali, mara kushtuka mangi alisimamishwa kazi na wakwe wakaamua wamrudishe matombo kwa uangalizi zaidi, hali ya mangi iliianza kuwa mbaya baada ya kuishiwa vibaya na kazi kufukuzwa.

  Bibie aliporudi hali yake ilikuwa safi na mangi alipata taarifa kuwa ni mchezo alichezewa, aliumia sana na kujutia nafsi yake ndipo alikata shauri la kurudi moshi.....

  ........*ITAENDELEA*.......
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kumbe ni hadith?
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  asiyesikia la mkuu. . .
   
 4. Kapax

  Kapax JF-Expert Member

  #4
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Summarize daa kitabu?
   
 5. toghocho

  toghocho JF-Expert Member

  #5
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 1,177
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  stori yako inatufundisha nini?
   
 6. YNNAH

  YNNAH JF-Expert Member

  #6
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,663
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  asiesikia ka mkuuuuuuuuuuuuuuu
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Apr 3, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Dah ngoja nikipata kamuda ntaipitia kwa ukaribu
   
 8. Vaislay

  Vaislay JF-Expert Member

  #8
  Apr 3, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 4,512
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  hmmm wa matombo noma alikuwa hajui?
   
 9. Kwisimla

  Kwisimla Senior Member

  #9
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  [stori yako inatufundisha nini?] Siyo kila king'aacho ni dhahabu
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  huyo lazima atavunjwa guu lake huyo..
   
 11. n

  nipos Member

  #11
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ni story nzuri inamafundisho
   
 12. MadameX

  MadameX JF-Expert Member

  #12
  Apr 3, 2012
  Joined: Dec 27, 2009
  Messages: 7,847
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  mmmh gazeti
   
 13. B

  Bigman 2012 Member

  #13
  Apr 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  its toooooooooooooooooooooooooooooooooo long!
   
 14. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  nlijua nai mangi mm ningeua mtu asee,sa ivi ungekuta nipo keko mbe.
   
 15. Purple

  Purple JF-Expert Member

  #15
  Apr 4, 2012
  Joined: Feb 9, 2012
  Messages: 2,031
  Likes Received: 228
  Trophy Points: 160
  Hongera kwa utunzi
   
 16. Vinci

  Vinci JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 2,642
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  kahadithi katamu...hakuna mchaga ambaye anaweza kufanya kitu kama hicho, mbuzi kwenye gunia aisee...hapana wako makini sana, lazima ageonjeshwa tundi tuu kabla ya ndoa.
   
 17. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  rangi huu hautupeleki popote......................nionavyo this is a case of racial stereotyping.................
   
 18. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #18
  Apr 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  ww hujielewi.sasa huowi shombo kwa ajili ya hivi vituko?kwa hyo ukikutana na mmatumbi mwenzio mwenye ujinga km huo unaoa sio
   
 19. Amyner

  Amyner JF-Expert Member

  #19
  Apr 5, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 2,404
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Si ndio hapo sasa..
   
Loading...