Sitawasahau Askari wa Wanyama pori

Pole sana,Mungu awalaani hao askari waliokufanyia unyama,Mungu atawalipa ipo siku.
Nakumbuka ilikua tarehe 20/5/2020 nikiwa maskani nilikutana na rafiki yangu wa vidato.Tukiwa tunapiga story akaniambia anafanya mishe za kuuza asali na ni biashara inamlipa sana basi kusikia vile na hali yangu ya maisha nikamwomba tupige wote mishe.Jamaa akanikubalia trip ya kwanza ilikua kuenda Manyara kwenye msitu flani(jina nalihifadhi) tulifika kule tukakutana na ndugu wengeni wawili jumla tukawa wanne na yule rafki yangu tukaanza safar ya kuingia msituni na piki piki mbili na ndoo tano kubwa za kuweka asali tuliingia msitu tukabak pikipiki vichakani tukaanza kurina asali ya chinii ghafla nlisikia mlio mkubwa sana PWAAAAH! kugeuka nlijiona nipo mwenyewe mbele kuna watu wawili wananijia na nguo za rangi ya kahawia kumbe ni askari wanyama pori nilihis kuzimia wakapiga risasi nyingine hewan nikabaki nmeduwaa wakafika karibu wakanipga pingu wakanilaza kifudifudi wakatoa gloves wakaanza nichuna ngoz ya unyayo huku wapo busy hawaongei na bibi nlipga sana kelele ila walikua kimya wakamwagia chumviii nilipga sana yowe haikusaidia yule askari mmoja akasema hawa hawana silaha huyu tumtie ulemavu fisi waje wamchukue tuvunje miguu yote.Ghafla askari mmoja akaniuliza nmetokea wapi na silaha yangu ipo wapi nikawaambia ukwel wote huku nmefunga mikono kama nasali wakaniacha wakaondoka shunghuli ikawa kutembea natembea vipi miguu imepiga ganzi maumivu makali.Usiku ukaingia nmelala hoi sijitambui wale wenzangu wakarudi kunicheki sikuamini wakanitia mgongoni hadi tulipoacha pkpk njaa kali+maumivu niliona kifo kimewadia nilifika kijiji kimoja kupata huduma kwenye zahanati kusafisha majeraha na dawa nesi alinionea huruma sana alinitibu kwa kulia sana nlikaa zahanati pale wenzangu wakafanya juu chini nikapata usafiri gari noah hadi mjini kutibiwa hospital ya wilaya hakika sitasahau askari wa wanyama poriii nmepona ila najua siwez lipiza kisasi
 
Back
Top Bottom