Sitawasahau Askari wa Wanyama pori

Notorious thug

JF-Expert Member
Dec 29, 2021
2,818
10,584
Nakumbuka ilikuwa tarehe 20/5/2020 nikiwa maskani nilikutana na rafiki yangu wa vidato. Tukiwa tunapiga story akaniambia anafanya mishe za kuuza asali na ni biashara inamlipa sana basi kusikia vile na hali yangu ya maisha nikamwomba tupige wote mishe. Jamaa akanikubalia trip ya kwanza ilikuwa kwenda Manyara kwenye msitu fulani(jina nalihifadhi) tulifika kule tukakutana na ndugu wengini wawili jumla tukawa wanne na yule rafiki yangu tukaanza safari ya kuingia msituni na pikipiki mbili na ndoo tano kubwa za kuweka asali.

Tuliingia msitu tukapaki pikipiki vichakani tukaanza kurina asali ya chini ghafla nilisikia mlio mkubwa sana PWAAAAH! kugeuka nlijiona nipo mwenyewe mbele kuna watu wawili wananijia na nguo za rangi ya kahawia kumbe ni askari wanyama pori, nilihisi kuzimia wakapiga risasi nyingine hewani nikabaki nimeduwaa wakafika karibu wakanipiga pingu wakanilaza kifudifudi wakatoa gloves wakaanza nichuna ngozi ya unyayo huku wapo busy hawaongei na mimi nilipiga sana kelele ila walikuwa kimya wakamwagia chumvi nilipiga sana yowe haikusaidia yule askari mmoja akasema hawa hawana silaha huyu tumtie ulemavu fisi waje wamchukue tuvunje miguu yote.

Ghafla askari mmoja akaniuliza nimetokea wapi na silaha yangu ipo wapi, nikawaambia ukweli wote huku nimefunga mikono kama nasali wakaniacha wakaondoka, shunghuli ikawa kutembea natembea vipi miguu imepiga ganzi maumivu makali.

Usiku ukaingia nimelala hoi sijitambui wale wenzangu wakarudi kunicheki sikuamini wakanitia mgongoni hadi tulipoacha pikipiki njaa kali+maumivu niliona kifo kimewadia nilifika kijiji kimoja kupata huduma kwenye zahanati kusafisha majeraha na dawa nesi alinionea huruma sana alinitibu kwa kulia sana nilikaa zahanati pale wenzangu wakafanya juu chini nikapata usafiri gari noah hadi mjini kutibiwa hospitali ya wilaya

Hakika sitasahau askari wa wanyama pori, nimepona ila najua siwezi lipiza kisasi.
 
Nakumbuka ilikua tarehe 20/5/2020 nikiwa maskani nilikutana na rafiki yangu wa vidato.Tukiwa tunapiga story akaniambia anafanya mishe za kuuza asali na ni biashara inamlipa sana basi kusikia vile na hali yangu ya maisha nikamwomba tupige wote mishe.Jamaa akanikubalia trip ya kwanza ilikua kuenda Manyara kwenye msitu flani(jina nalihifadhi) tulifika kule tukakutana na ndugu wengeni wawili jumla tukawa wanne na yule rafki yangu tukaanza safar ya kuingia msituni na piki piki mbili na ndoo tano kubwa za kuweka asali tuliingia msitu tukabak pikipiki vichakani tukaanza kurina asali ya chinii ghafla nlisikia mlio mkubwa sana PWAAAAH! kugeuka nlijiona nipo mwenyewe mbele kuna watu wawili wananijia na nguo za rangi ya kahawia kumbe ni askari wanyama pori nilihis kuzimia wakapiga risasi nyingine hewan nikabaki nmeduwaa wakafika karibu wakanipga pingu wakanilaza kifudifudi wakatoa gloves wakaanza nichuna ngoz ya unyayo huku wapo busy hawaongei na bibi nlipga sana kelele ila walikua kimya wakamwagia chumviii nilipga sana yowe haikusaidia yule askari mmoja akasema hawa hawana silaha huyu tumtie ulemavu fisi waje wamchukue tuvunje miguu yote.Ghafla askari mmoja akaniuliza nmetokea wapi na silaha yangu ipo wapi nikawaambia ukwel wote huku nmefunga mikono kama nasali wakaniacha wakaondoka shunghuli ikawa kutembea natembea vipi miguu imepiga ganzi maumivu makali.Usiku ukaingia nmelala hoi sijitambui wale wenzangu wakarudi kunicheki sikuamini wakanitia mgongoni hadi tulipoacha pkpk njaa kali+maumivu niliona kifo kimewadia nilifika kijiji kimoja kupata huduma kwenye zahanati kusafisha majeraha na dawa nesi alinionea huruma sana alinitibu kwa kulia sana nlikaa zahanati pale wenzangu wakafanya juu chini nikapata usafiri gari noah hadi mjini kutibiwa hospital ya wilaya hakika sitasahau askari wa wanyama poriii nmepona ila najua siwez lipiza kisasi!
Hizo asali mlizokuwa mnalina zilikuwa Ni zenu? Tuanzie Hapa kwanza.
 
Pole sana mkuu shukuru Mungu hawajakuua au kukutupa gerezani.

Ila nisiseme uongo nimecheka sana hapo uliposema kuwa ulijikuta mwenyewe unatazamana na maaskari pori 😂
... wale askari wakawa wanasemezana; tumvunje miguu fisi waje wambebe! Dah! ha ha ha! Na fisi wanavyobeba vibaya kila mmoja na kipande chake huku bado victim akiwa anahema!
 
... wale askari wakawa wanasemezana; tumvunje miguu fisi waje wambebe! Dah! ha ha ha! Na fisi wanavyobeba vibaya kila mmoja na kipande chake huku bado victim akiwa anahema!
Hatari sana aisee.
 
Ndio maaaana ukitembelea mapori mengi ya Hifadhi hukosi kukutana na Viungo vya Binadamu. Shukuru Mungu kwa kuachwa mzima, kwa maelezo yako hilo pori ni Msitu wa Hifadhi ulikumbana na askari wa TFS au huenda Maaskari wa Misitu ya Vijiji - VGS. Pole sana Mkuu
 
18 Reactions
Reply
Back
Top Bottom