Kaliua: Askari wa wanyama pori afariki

Songwe Yetu

Member
Nov 22, 2021
84
99
Askari wa wanyama pori afariki dunia wakati akijaribu kumkimbiza jangili.

Jangili huyo alikimbilia mtoni na akaaanza kuogelea ndipo askari huyo aliekuwa na wenzake nawe akaamua ajitose kimfuata mtuhumiwa.

Alioogelea lakini alipofika katikati ya mto maji yalimzidi kwani kina cha maji kilikuwa kirefu hivyo alianza kuomba msaaada kwa wenzake na walimuangalia mpaka akafariki.

Wananchi waliokuwa jirani waligoma kumuokoa na hivyo amefariki, maiti itasafirishwa na ndege kuelekea kwao, poleni familia kwa kumpoteza classmate wangu
 
Huyu askali ndio wale darasa la saba. mwenye akili timamu, why all this trouble? ameingia majini , maji mengi achana naye kwani kaiba nini chako mpaka utumbukie majini?

Peaceful arrest sawa, lakini kutumbikia kwenye maji hapana. Au alitaka kuwa kama majaliwa? Wanyama wanaouzwa Arabuni si hayo hayo! Jinga tu wacha lipate faida ya ujuha! (samahani sana kwa lugha kali)
 
Askari wa wanyama pori afariki dunia wakati akijaribu kumkimbiza jangili.Jangili huyo alikimbilia mtoni na akaaanza kuogelea ndipo askari ...

Kwa iyo askari wenzake walisimama wakamwangakia anavyo kimbizana na jangili kwenye maji wakakaa kimya tuu, na majirani nao wametulia tuuu jamaa anahangaika dimbwini kubwia ma maji hadi kaenda kwa mola!

Jangili nae vipi kapotelea majini huko au?
 
Askari wa wanyama pori afariki dunia wakati akijaribu kumkimbiza jangili.Jangili huyo alikimbilia mtoni na akaaanza kuogelea ndipo askari...
Unahakika ni jangili? Usikute mwananchi masikini alienda kujitafutia chochote akakutana na hao jamaa. Kingine kwanini wananchi walikataa kumsaidia?

Inaonyesha hao askari wanyamapori wanatesa sana wanakijiji, sivyo? Uhifadhi lazima ushirikishe communities zinazoishi kuzunguka hifadhi lakini pia kinachopatikana kwenye hiyo hifadhi wananchi nao wapate chao.

Bila hivyo askari watakufa sana mtoni.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom