Sitasahau nilipokutana na mchumba mwenza live!!

Sitasahau nilipokutana na mchumba mwenza live!!

Halafu waume wa maana wamekwenda kutaka kuoa akakataaa, leo lawama! hebu ninyamaze mie kina mumu, shunie, zeshchriss na wenza wasije wakaninyonga
Sasa hapo ningejuaje kama angebadirika??
Ila nashukuru nimeyasema ya moyoni.Nimepata faraja.Mana mpaka kazini nikaomba ruhusa.Najifungia ndani tu.Sijui kimenikuta nini.
 
Kuna kinafasi tunakuwa tumekiacha tukijiaminisha mambo yatarudi kwenye mstari....Halafu Grace hakuwa na uhakika mpaka alipokutana na mwenzake ndio akapata kujua ukweli....

Wanaume nanyi mpunguze kucheza na nafsi zetu, mkijua hapa mnapita tu...msemage mapema.
Tuseme ili mtutose sio??
 
Ooh jamn hongera kwa ujasiri wako uliouchukua mpaka kuamua kushare na sisi hii hadithi.

Natumai utakua umepunguza uchungu kama sio kuumaliza kabisa.

Watu wengine waliwekwa kama madaraja ya kuvukia, ni vivuko tu kwenda sehemu au hatua nyingine.

Halikua fungu lako haijalishi ulimsubiri kwa muda gani lakini amini Mungu kakuepushia jambo kubwa.

Kila jambo hutokea kwa sababu na kila jaribu huwa na mlango wa kutokea. Naamini utakua umeshasahau na kusamehe mkuu.

Kila mtu atahukumiwa sawa na matendo yake...

Kwenu wanaume jifunzeni kuwa wawazi na kama humuhitaji mtu mueleze ukweli sio kumpotezea muda wake.
Lakini wadau walikwenda kutaka kumuoa ujue, peengine aliwaona mafala tu anamsubiria mtu wake wa ughaibuni. na pengine masela aliwatimua kwa nyodo za mwana uhali gani
 
Aksante Dear.Mapito niliyopitia kwa huyu kaka.
Nashindwa kuelewa
Kuna wakati Tena ilitokea sitofamu akawa Na MTU mwingine.
Nikawazaaaa nikaamua kushukuru Na kusonga mbele.
Akanijia
akijutia sana Na kusema alipoenda alipotea nimsanehe.
Nikatafakari sana sana
Nikansamehe!!!!!!
Ndo amenitenda Tena.
OK.Sijajua nimekosea wapi au maisha yangu anayachuKuliaje.
Any way.Sijajua dhumuni la Mungu kunikutanisha naye Na majaribu haya.
Why iwe hivyo.Huwa najiuliza sana.
But.Nashukuru.
Dada usije ukaona kama labda mimi nimekukazia sana! hapana najaribu tu kusimama upande wa kiumeni, naamini huyu jamaa alikuonesha dalili kadhaa wa kadhaa kwamba hakufai lakini ukajitia upofu na kumng'ang'ania. sasa sijui kwa kuwa alikuwa ughaibuni au laa, pia wana walikuja na nia za dhati ukawatimua. najaribu kujenga picha tu dada. ila pole kwa yaliyokukuta
 
Dah baada ya kusoma ujumbe wako ikaingia msg ya mkaka anayenilia mingo kitambo alafu yuko mbali

Nimemjibu "go to the fucking hell"


Mpaka saivi sijajua hilo jibu limenitokajetokaje
Usikute hata mleta mada aliwaambia wale washkaji hivyo hivyo, leo anawakumbuka
 
Lakini wadau walikwenda kutaka kumuoa ujue, peengine aliwaona mafala tu anamsubiria mtu wake wa ughaibuni. na pengine masela aliwatimua kwa nyodo za mwana uhali gani
Ahadi feki na maneno matamu huwa vinatuponza sana....kuushirikisha na kuuamini sana moyo kuliko akili vimetutia ukilema wa kufikiri mbali.
 
samahani dada kwa kukuharibia uzi wako
mwanangu ni kweli ulizingua, tena ilikuwa ndio post ya kwanza kabisa. ila niamini nikwambiayo kwamba umefanya uungwana wa hali ya juu.

Big up kwa kuona kwamba uekosea na kuamua kumuomba grace msamaha, wewe mwenyewe tu ukiangalia wadau wamekudiss ila BIG UP sana mwana wewe ni muungwana
 
Pole sana Grace.

Kama bado haujapata mwenzi, i pray that you get your perfect match.Pole sana!!
 
Ok kwa sababu hukujua nafuta kauli!
Usiwe mnyonge wala kusikitika sana wala kujilaumu ama kumlaumu huyo jamaa ! Samehe sahau endelea na maisha. Kumbuka Mume analetwa na Mungu!
Hutakiwi kufuta kauli kirahisi, alitakiwa ajue. anaingiaje kwenye mahusiano bila kujua?? hivi kila siku tukisema ukikosea kuchagua mwenza umekosa kila kitu kwenye maisha hamuelewi??
 
Back
Top Bottom