Determinantor
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 61,439
- 100,731
- Thread starter
- #21
acha uchokozi
Kwamba ccm wanatumia ubwabwa.
Kwamba ccm wanatumia ubwabwa.
Morning Team
Natokea kwenye familia ya wafugaji, baba yangu alikuwa ni mwindaji mzuri sana japo rafiki zake siku zote hawakukubaliana na aina ya uwindaji wa Baba, ni kweli baba alikuwa anapata sana kwenye uwindaji wake lakini njia zake za upatikanaji wa kitoweo chake ndio ulikuwa gumzo.
Ili kuwakomoa rafiki zake na watani zake mara nyingi Baba alitumia "unga wa mtama" kuwapatia wale aliokuwa anataka kuwakamata, unga huu ulikua adimu kwa rafiki zake na hivyo rafiki zake hawa hawakuambulia "kitoweo" kikubwa kwani wao walitumia njia halali za uwindaji.
Miaka ya hivi karibuni hivi, rafiki zake hasa rafiki yake wa Karibu sana alijulikana kwa jina la Utani la "Mzee Makaki" aliamua kukusanya watoto na vijana wake wote na kuvamia kila pori kwa kila "silaha" na nikiri wazi kuwa silaha hizi kwa kweli hazikua haramu hata kidogo ukilinganisha na zile alizotumia baba yangu. Harakati za Mzee Makaki zilimzindua usingizini baba yangu baada ya kuona Mzee Makaki kila aendapo kuwinda hurudi na Gunia zima la "vitoweo". Vitoweo vingi alivyokamata Mzee Makaki karibia vyote vilifuata "mtego" vyenyewe na ukweli ni kwamba Mzee Makaki yeye alitumia Mtego rafiki, wenye sauti tamu ya ubembelezi na ilijoaa ufasaha wa maneno ndani yake, yaani ukweli mtupu.
Tena Vitoweo hivi vingi vilikua na siha njema, vyenye akili timamu na kufanya maamuzi sahihi, hivyo bidhaa zake kila alipozipeleka sokoni zilipata wateja wengi zaidi japo Baba yetu aliendelea kutumia unga ule kumuibia Mzee Makaki.
Baba yangu alihamaki sana, akatuita kwa hasira akauliza kwa jazba, mnafanya nini, hebu oneni mwenzenu anavyopata vitoweo, mimi nitaendelea kutumia "unga wa mtama" hadi lini? si mnaona unga wenyewe ulivyokuwa adimu kuupata siku hizi? Nakumbuka sana siku ile ilikua inakaribia kumbukumbu ya kuzaliwa "babu" yetu ambaye kwa sasa ni Mzee sana na hata maamuzi ya vijana yake nayo yalionekana kuzeeeka.
Kama kawaida ili kumridhisha Baba tukaamua tutumie tena "unga wa mtama" kukamata kitoweo na hatimaye kumfurahisha baba atakapokutana na Watani wenzake......Kumbe siku zote lenye mwanzo halikosi kuwa na Mwisho. Tulitega kila mtego lakini tulichoambulia kukamata ni "Simbilisi" wachache sana ambao walirandana kwa karibu sana na Sungura wengi aliokamata Mzee Makaki miezi michache alipokuwa anawinda kwenye pori hilo hilo.
Basi Jioni ya siku ile tulikaa na kujifariji kuwa Maadamu tumekamata hawa simbilisi wachache basi na kwakuwa hawa wana sifa isiyo yao ya kuiwakilisha jamii nzima ya Sungura, basi tuuiaminishe familia ya Mzee Makaki kuwa Simbilisi hawa wachache wasiozidi 20 ni Muakiso wa Sungura Maelfu na maelfu waliko huko porini, kwahio kwa kukamata hawa wachache ujue tumekamata Sungura wengi.......
Maskini weeee kumbe tulikamata "simbilisi" tukidhania ni "sungura" kama wa Mzee Makaki. Sifa kubwa ya simbilisi hawa ni kufuata upepo na harufu ya unga wa mtama, na mara unga huo unapokuwa umekwisha basi haraka hukimbilia tena porini na kufanya ufugaji wetu kuwa mgumu hasa katika utunzaji wa hawa Vitoweo. Namsikitia sana baba maana Sijui ataweka wapi sura yake kesho atakapokutana na Mzee Makaki.
Funzo: Tusitumie "unga wa Mtama" tunapokua tunawinda "vitoweo"
Alamsiki
Ha ha haaa...kama hivi visimbilisi vilivyofuata unga wa mtama huko nyanda za juu kusini!
chopa ni unga wa mtama?
Hesabu raisi sana hii:-
1.Mzee Makaki=CCM
2.Ungaa wa mtama=Pesa
3.Simbilisi=Wasanii(JB&Compan)
kama nimekosea sema nikupe mji
Kwamba ccm wanatumia ubwabwa.
Ngoja nijikumbushe 4m2 yangu Minaki with Mr.FUMBUKA japokua sikupenda hesabu....
Simultaneous Equation
By Substution
Baba yako =Lowasa
Mzee Makaki=Membe na wenzie wenye tamaa ya urais
Unga wa mtama=misaada makanisani na nyama za monduli
Familia =CCM
Sungura = CDM+wananchi
Simbilisi =akina JB
nikikosea nitupie F tuu nitakuja ku reseat