Sitasahau: Baba alikamata "Simbilisi" akidhani "Sungura"

Sitasahau: Baba alikamata "Simbilisi" akidhani "Sungura"

Determinantor

Platinum Member
Joined
Mar 17, 2008
Posts
61,444
Reaction score
100,740
Morning Team
Natokea kwenye familia ya wafugaji, baba yangu alikuwa ni mwindaji mzuri sana japo rafiki zake siku zote hawakukubaliana na aina ya uwindaji wa Baba, ni kweli baba alikuwa anapata sana kwenye uwindaji wake lakini njia zake za upatikanaji wa kitoweo chake ndio ulikuwa gumzo.

Ili kuwakomoa rafiki zake na watani zake mara nyingi Baba alitumia "unga wa mtama" kuwapatia wale aliokuwa anataka kuwakamata, unga huu ulikua adimu kwa rafiki zake na hivyo rafiki zake hawa hawakuambulia "kitoweo" kikubwa kwani wao walitumia njia halali za uwindaji.

Miaka ya hivi karibuni hivi, rafiki zake hasa rafiki yake wa Karibu sana alijulikana kwa jina la Utani la "Mzee Makaki" aliamua kukusanya watoto na vijana wake wote na kuvamia kila pori kwa kila "silaha" na nikiri wazi kuwa silaha hizi kwa kweli hazikua haramu hata kidogo ukilinganisha na zile alizotumia baba yangu. Harakati za Mzee Makaki zilimzindua usingizini baba yangu baada ya kuona Mzee Makaki kila aendapo kuwinda hurudi na Gunia zima la "vitoweo". Vitoweo vingi alivyokamata Mzee Makaki karibia vyote vilifuata "mtego" vyenyewe na ukweli ni kwamba Mzee Makaki yeye alitumia Mtego rafiki, wenye sauti tamu ya ubembelezi na ilijoaa ufasaha wa maneno ndani yake, yaani ukweli mtupu.

Tena Vitoweo hivi vingi vilikua na siha njema, vyenye akili timamu na kufanya maamuzi sahihi, hivyo bidhaa zake kila alipozipeleka sokoni zilipata wateja wengi zaidi japo Baba yetu aliendelea kutumia unga ule kumuibia Mzee Makaki.

Baba yangu alihamaki sana, akatuita kwa hasira akauliza kwa jazba, mnafanya nini, hebu oneni mwenzenu anavyopata vitoweo, mimi nitaendelea kutumia "unga wa mtama" hadi lini? si mnaona unga wenyewe ulivyokuwa adimu kuupata siku hizi? Nakumbuka sana siku ile ilikua inakaribia kumbukumbu ya kuzaliwa "babu" yetu ambaye kwa sasa ni Mzee sana na hata maamuzi ya vijana yake nayo yalionekana kuzeeeka.

Kama kawaida ili kumridhisha Baba tukaamua tutumie tena "unga wa mtama" kukamata kitoweo na hatimaye kumfurahisha baba atakapokutana na Watani wenzake......Kumbe siku zote lenye mwanzo halikosi kuwa na Mwisho. Tulitega kila mtego lakini tulichoambulia kukamata ni "Simbilisi" wachache sana ambao walirandana kwa karibu sana na Sungura wengi aliokamata Mzee Makaki miezi michache alipokuwa anawinda kwenye pori hilo hilo.

Basi Jioni ya siku ile tulikaa na kujifariji kuwa Maadamu tumekamata hawa simbilisi wachache basi na kwakuwa hawa wana sifa isiyo yao ya kuiwakilisha jamii nzima ya Sungura, basi tuuiaminishe familia ya Mzee Makaki kuwa Simbilisi hawa wachache wasiozidi 20 ni Muakiso wa Sungura Maelfu na maelfu waliko huko porini, kwahio kwa kukamata hawa wachache ujue tumekamata Sungura wengi.......

Maskini weeee kumbe tulikamata "simbilisi" tukidhania ni "sungura" kama wa Mzee Makaki. Sifa kubwa ya simbilisi hawa ni kufuata upepo na harufu ya unga wa mtama, na mara unga huo unapokuwa umekwisha basi haraka hukimbilia tena porini na kufanya ufugaji wetu kuwa mgumu hasa katika utunzaji wa hawa Vitoweo. Namsikitia sana baba maana Sijui ataweka wapi sura yake kesho atakapokutana na Mzee Makaki.

Funzo: Tusitumie "unga wa Mtama" tunapokua tunawinda "vitoweo"

Alamsiki
 
Mzee Makaki ni balaa heri lile la njaa!Wengi wanamgwaya hasa wasio na haya!....endeleeni kumwaga mtama mpaka mtashika tama!
 
hahahahhahaaa Mpwa wangu Mani Hebu njoo usome hii comment hapa
Mzee Makaki ni balaa heri lile la njaa!Wengi wanamgwaya hasa wasio na haya!....endeleeni kumwaga mtama mpaka mtashika tama!
 
Last edited by a moderator:
MZEE MAKAKI NI MBUNIFU SANA , huwezi kuiga kabisa mbinu zake aisee !
 
Mpwa wangu wapi tena panakutatiza nikusaidie? Hujui uwindaji kweli?
Atakuwa alikamata Mbeva.sijaelewa kabisaaa. Nadhani huu ndio uandishi wa Great Thinker Bravo sana.
 
hahahaaa sorry Mpwa wangu hivi kuna mahali nimemtaja Dr. W.P. Slaa watakua na lao jambo hao sio bure, mimi nazungumzia uwindaji na ufugaji hahahhaaaaaaaa
I

Utaambiwa umetumwa na Dr. Slaa
 
Last edited by a moderator:
hahahaaa sorry Mpwa wangu hivi kuna mahali nimemtaja Dr. W.P. Slaa watakua na lao jambo hao sio bure, mimi nazungumzia uwindaji na ufugaji hahahhaaaaaaaa

Story yako inaeleweka ingawa kuna sehemu umejichanganya unaweza kuwachanganya wasomaji
 
itabidi baba ako abadili mbinu za kuwinda japo kashachelewa ila ana kijana mmoja ambaye ni mwindaji hodar nathani huyu nizaidi ya familia nzima ila anawaendesha kama wendawazimu na anawinda kivyake vyake.
 
hahahaaa pengine hapo ulipochanganyikiwa ndipo kwenye msingi mzima wa habari yenyewe , mie simo
Story yako inaeleweka ingawa kuna sehemu umejichanganya unaweza kuwachanganya wasomaji
 
hahahahaaaaaa kwani si pori ni hilo hilo? Ngoja atakutana na Baba huko huko
itabidi baba ako abadili mbinu za kuwinda japo kashachelewa ila ana kijana mmoja ambaye ni mwindaji hodar nathani huyu nizaidi ya familia nzima ila anawaendesha kama wendawazimu na anawinda kivyake vyake.
 
hahhaa kumbe wale wananchi wanakuja kwenye mikutano ya CHADEMA kushangaa helikopta
 
Hao sungura wanaovamiwa na kukamatwa kinguvu huko porini ipo siku watakuwa wajanja na kufuata njia sahihi ya kujificha. Ahahahaaa
 
Back
Top Bottom