mgodi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 2,780
- 1,851
Wanabodi amani iwe nanyi na poleni na majukumu ya kutafuta rizki....Natangaza kugombea ubunge jimbo la KARATU......
****Njia ya muongo...... *×*
Tangu lini ulikuwa ccm wakati hapo ulitangaza nia kuwa unatangaza kugombea ubunge karatu kupitia chadema...
Jimbo la Karatu ni jimbo lenye heka heka nyingi sanaa za kisiasa, ni kiini cha mabadiliko katika nchi hii, ni kati ya maeneo yenye historia kwenye medani za kisiasa,, jimbo hili limekuwa chini ya CHADEMA toka mwaka 1995 kipindi hicho mbunge wake akiwa Mh. DR.WILLBROAD PETER SLAA.... nimeamua kujitosa kugombea jimbo la Karatu kupitia chama changu CHADEMA,, sifa zote ninazo, ntafuata taratibu zote ndani ya chama changu ,,nitayasikiliza na kuyahishimu mawazo na maoni ya viongozi wangu wa chama,, umri wangu unaniruhusu,jimbo lile kwa sasa linahitaji kijana ambaye ataweza kuendana na pilika pilika za maendeleo ya haraka kwa jimbo lile,, barabara za mji na stendi ya magari ni changamoto kubwa sanaaa kwa mji wa karatu wenye vyanzo vingi sana vya mapato ikiwemo utalii ambapo Karatu ni center ya hifadhi za NGORONGORO na MANYARA,, mji una hotel nyingi sana kitalii,rasilimali za madini nk....
Maji bado ni changamoto kubwa sana wakati mji wa karatu umezungukwa na rasilimali nyingi sana misitu ambayo ni chanzo kizuri cha maji....
Ndugu zangu wanakaratu mnahitaji kijana atakayeweza kuendana na siasa za speed kubwa kwa maendeleo ya haraka sanaaa...... Kijana wenu kamanda HARIOHAY nahitimu chuo mwaka huu mwezi June,, nakuja kujitosa ili jamii yangu inufaike na elimu yangu na nguvu yangu...
Naomba mnipokee ili tupate maendeleo ya haraka sanaa,, Mimi ni mtoto wenu nimesomea shule yenu ya kata,, sasa naomba muonje matunda ya mtoto wenu ambaye ni zao la shule zenu za kata, nazijua changamoto zilizopo kwenu, maisha yenu nayajua vizuri,, familia yangu ni kimaskini sana, naamini nitawatumikia kwa upendo na unyenyekevu wa hali ya Juu.
Ahsanteni sanaaa Mungu awe kiongozi wetu daima....
Wenu,
Gjhariohay!