Sitarudia kuitetea tena CCM. Nimechoka

GJHariohay

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,026
2,000
Wanabodi habari za jioni,Poleni sana na Majukumu

Awali ya yote naomba kudeclear interest, mimi ni CCM , Damu yangu ya kijani kibichi kabisa, mzalendo wa hali ya juu.

Najitokeza rasmi mbele yenu leo hii kuonesha hisia zangu kuhusu uteuzi wa Mh. Anna ambae ni Mwenyekiti na Chama cha upinzani.

Nimesikitika sana, nimenyong'onyea sana, nimejisikia vibaya mno.
Nimekuwa nikifanya vema kazi za chama changu cha CCM kwa ufanisi wa hali ya juu na uzalendo, nimekuwa nikipambana na kila anaejaribu kukashfu chama changu ama kiongozi wangu hasa Rais wetu Mtukufu , nimepambana pia muda mwingine kupindisha hata ukweli ili mradi tu chama kisipate kashfa yeyote.

Nimefanya kazi hii kwenye mitandao yote ya kijamii, nimepambana vilivyo na mtu anaeitwa Mange Kimambi kwenye mtambo wa Instagram, hii yote ni kwa sababu ya kulinda chama ili chama nacho kinilinde.

Nimesikitika sana wazalendo wa chama tunaachwa, wanachukuliwa watu ambao hawajui machungu na mateso tuliyoyapata sisi wengine ambao muda mwingine tumepambana kupindisha ukweli ili walau tukumbukwe siku moja.

Nimejiuliza sana, huyu mama kipindi cha kampeni alinadi sera zake, sisi tulinadi pia sera zetu, leo hii anaenda kutekeleza ilani ya chama ipi?? Otherwise tunaomba viongozi wetu watuweke wazi kama hawa walikuwa mapacha wetu ama walikuwa sehemu ya mkakati wetu kudhoofisha wapinzani wetu kipindi hicho.

BTW,
Mimi ni mtu mwenye vyeti vyangu halali , sina waswasi wowote , nimeachwa , Mheshimiwa katika hili amenisikitisha sana, sasa naangalia utaratibu mwingine, vijana wenzangu wa upinzani nakuja mtaani naomba msinitenge, nimechoka kuitesa dhamira yangu.

Najiunga rasmi na nyie wazalendo wenzangu, naomba mnipokee .....

Wasalaam!!!!!!!
 

wise123

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
1,369
2,000
ndo nyie mlikuwehuka nakuanza kutusi watu kisa iyo vaccancy ya Kilimanjaro eeeh alijisemea yericko Nyerere mnaweza kuhari***a mtu kichwani kisa iyo post
 

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,139
2,000
Pole sana sisi na akina Lizaboni, Le mutuz na Pasco wa JF tumekubali yaishe tumebaki kushikilia mapembe tu maisha yanakwenda, chama kina wenyewe ndugu yangu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom