Sitaki!!!

SItaki kusikia CUF wawaaambiwa wananchi wa mwanza ni maskini na kuwashangaa...wakati Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa rais mambo ya uchumi hapa awali.

Sitaki kusikia lipumba akitumia lugha ya kiuchumi kwenye mikutano yake ya kisiasa..kwa wananchi ambao hawajui uchumi nini.
 
Last edited:
- Sitaki Tanzania kuwa na Tume ya Uchaguzi inayopata maelekezo kutoka serikalini.
- Sitaki kuona wahitimu wa Ualimu wakikataa kufundisha, badala yake wanabaki kubanana na wasio na taaluma ya ualimu kwenye ajira nyingine.
- Sitaki kuona taifa lisilo la wazalishaji, badala yake wote tunakuwa wachuuzi wa bidhaa za nje.
 
Sitaki kusikia baada ya uchaguzi kuwa mtu alihama makazi alishidwa kupiga kura kwakuwa kadi yake ya kupigia kura hajaorozeshwa sehemu aliyohamia
 
Sitaki kusikia mtu anamtetea JK kuwa si FISADI wakati ameingizwa Madarakani na Mafisadi
Sitaki sitaki kabisa mtu amtetee et kwa sababu ya itikadi, imani, au tu et kwa sababu JK ni Mpole
Sitaki mtu amtete et kwa kusema alete evidence wakati anajua kabisa kuwa Yupo kwenye list ya Mwembe yanga, Anajua Kagoda aliitumia kwenye kampeni zake za urais
 
Mkuu,
Watu wa ujenzi siku zote huwa tunafahamu kuwa, dawa ya matatizo yote ni kuanza. Ukisimama na kusema uyajadili kwanza ni kwamba hutafika mbali. Ndiyo maana huwa kuna plan za kazi kwa ujumla ila zile in detail zinakuwa zinafanywa kwa kila wiki inayokuja kwa kuangalia ile plan kubwa.

Matatizo ya Tanzania yanajulikana sana sana. Kwani nani hayatambui? Labda kama hayupo Tanzania au hajawahi kufuka kabisa. Sasa kuanza kusema sitaki hiki wala kile, THEN WHAT???

Inabidi kufika sehemu tuwe kama Mwanakijiji na kuanza kupigana kuibadili hiyo hali kwa njia moja au nyingine. Ningelitegemea watu waanza kusema "pale anapokaa, ataanza kuwakusanya watu ili kujenga mazingira ya usafi, kutunza barabara, kupanda miti na mauwa nk nk". Hii SITAKI haisaidii chochote na matatizo ya Tanzania yameshasemwa sana.

Before the diagnosis there is the prognosis.
 
Sikubaliani na WaTanganyika wanavyoivamia Zanzibar kijeshi na kuiweka chini ya ubeberu na ukabaila wa mkoloni mweusi.
 
Sitaki:

Zanzibar kuwa na majimbo mengi, mikoa mingi na mfumo wenye uwakilishi mkubwa kiasi kwamba nina wasiwasi kwamba kwa kila wanzanzibar 10, watatu (3) hadi wanne (4) ni wanasiasa.
Kazi atafanya nani, kama wawili (2) hadi (3) ni vikongwe/wazee na watoto? na (1) hadi wawili (2) ni wazururaji au wafanyakazi ki-mdebwedo?
 
SITAKI ndi kuona kuna idadi kubwa ya wabunge tanzania wakati matatizo tulinayo ni commona sehemu zote. Sababu SITAKI kuona bunge limekuwa kama kijiwe cha maswali ma majibu huku hoja kama kuoneza posho za wabunge zinafanyiwa kazi lakini hoja nyingine zinapewa amjibu rahisi ya hali ua uchumi

Sitaki kuona wasomi wanakimbilia na kuteuliwa kwenye vyeo vya kisiasa badala ya kufanya chunguzi na kutoa changaaoto kwenye mambo yao ya elimu waliyosomea.

Sitaki kuona siasa (wabunge, mawaziri) ndio ajira inayolipa vizuri zaidi ya ajira nyingine huku waalimu, manesi na madaktari wakimbiwa ajira zao ni wito.
 
Sitaki kuona Waziri anakuwa pia mbunge, hivi ndivyo ufisadi wa ccm ulivyozaliwa!!!!!!
 
SItaki kusikia chadema wawaaambiwa wananchi wa mwanza ni maskini na kuwashangaa...wakati Lipumba aliwahi kuwa mshauri wa rais mambo ya uchumi hapa awali.

Sitaki kusikia lipumba akitumia lugha ya kiuchumi kwenye mikutano yake ya kisiasa..kwa wananchi ambao hawajui uchumi nini.

Buswelu ulimaanisha CUF au?
 
Sitaki:

Zanzibar kuwa na majimbo mengi, mikoa mingi na mfumo wenye uwakilishi mkubwa kiasi kwamba nina wasiwasi kwamba kwa kila wanzanzibar 10, watatu (3) hadi wanne (4) ni wanasiasa.
Kazi atafanya nani, kama wawili (2) hadi (3) ni vikongwe/wazee na watoto? na (1) hadi wawili (2) ni wazururaji au wafanyakazi ki-mdebwedo?

Hahahahahahahahahahaha, good analysis Kasheshe,

Excellent!
 
Sitaki tena kuona Raisi anamadaraka makubwa namna hii; anateua kila cheo mwenyewe bila hata kamati za kuwapitisha kwa kuwajadili wateuliwa, mawaziri, wakuu wa mikoa, ma DC, Jaji Mkuu, Majaji, mkuu wa Polisi, DPP, Mkuu wa Takukuru, mawaziri wadogo, wakuu wa mashirika makubwa, mkuu wa uhamiaji, nchi imegeuzwa genge la wacheza pata-potea!!!!
 
Ufumbuzi mnao: Amueni.... AMUENI kufa na kupona kuleta mabadiliko, mtaacha kusema SITAKI....

Maneno matupu hayavunji mfupa!
 
sitaki serikali tatu, mbili ni moja tuu ndio nataka

sitaki serikali inayoangalia mfumo mbaya wa lugha ya kufundishia TZ alafu wanakaa kimya kwa ajili wanaweza kuwapeleka watoto wao nje (mwanafunzi anasoma std 1-7 kwa kiswahili akifika form 1 anaanza kutumia kiingereza wakati kiingereza hakiwezi ni mateso haya, bora nusu ya masomo shule ya msingi yafundishwe kwa kiingereza na hii itawasaidia wakifika form1)
 
Sitaki tena sitaki kusikia kuwa watu hawataki wasicho kitaka...

Walio kuwa hawataki walisha kwenda zao na tukawazika na hizo sitaki zao...

Walizitumia hizo sitaki zao zikatuletea uhuru kutoka kwa yule tusiye mtaka...

Leo tulio baki tumebakia kama wake ndani ya nyumba, hatutaki lakini hatuchukui jitihada zozote za kuonyesha kuwa kweli hatutaki...

Hatutaki hatutaki na uku twaendelea kuwachaguwa zilipendwa wa siasa na wastaafu waendelee kututawala...

Hatutaki kitu gani na hali kila kukicha tunawakumbatia hao hao tunao jidai kuwa hatuwataki...!?

Kama kweli hatutaki mbona hatuoni hizo sitaki zikifanyakazi... kuondoa tusicho kitaka...!?

Nasema sitaki tena sitaki kuona wala kusikia kuwa hatutaki, na hali uwezo tunao wa kuifanyia kazi hiyo sitaki.

Tusio wataka wanajua kuwa hatuwataki, ila nyoyo zetu kwa kuwa zimejaa unafiki, ndio maana wanatufanya mishikaki... Wanatula uku tunaona... tumebakia kama kuku wa kisasa ndani ya banda, mie siye... mie siye... Hakuna jitihada ya kuonyesha kuwa kweli hatutaki.

Nasema tena sitaki kusikia kuwa hatutaki, uku tumejaa unafiki... Kama kweli hatutaki mbona hatuchukui hatua za kweli za sitaki tukaonyesha kweli hatutaki...!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom