Sitaki!!!

Sitaki!!!

Kyachakiche

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2009
Posts
986
Reaction score
210
Ndugu mwanajf, kwenye mada hii unakaribishwa kuelezea kitu chochote unachoona hukitaki kama ambavyo mimi sitaki haya:

1.Sitaki Serikali inayosahau ahadi zake kwa wanachi kama; Maisha bora kwa kila Mtanzania, Ajira milioni moja, mahakama ya Kadhi na kumaliza mpasuko wa kisiasa Zanzibar!

2.Sitaki serikali ambayo kwa kupitia vyombo vyake vya dola kushindwa kukomesha mauaji wa Albino na Vikongwe, kubaini wezi wa Kagoda, Meremeta na Mwanachi Gold Mines!

3.Sitaki Waziri Mkuu aseme kwamba hawezi kuzungumzia tena maswala ya Meremeta hata kama ikibidi atoswe!

4.Sitaki Spika awachukulie hatua za nidhamu wabunge wa upinzani pale inaposemekana wamekwenda kinyume na kanuni kama ilivyowahi kutokea kwa Zito, Cheyo, Slaa na Ndesamburo ili hali wenzao wa CCM wakiachwa kama vile Mdhihiri, Selelii, Mhaghama na Mpendazoe!

5. Sitaki Serikali ikwepe jukumu la ulinzi huko Tarime na Rorya na kusingizia Halmashauri hadi kutishia kupeleka jeshi huko!
6.
7.
8.....
Karibuni tuendeleze
 
Sitaki Mahakama ya Kadhi iombe ridhaa ya Bunge kuanzishwa, na igharamiwe na serikali!! Sitaki kabisa!
 
7. Sitaki na sipendi kabisa jinsi Mjomba Mkuu anavyotapanya pesa za watanzania walalahoi kusafiri kila kukicha kwenda ughaibuni hasa USA
 
SITAKI:
Lugha zinazotumiwa na Watanzania wengi siku zote. Sitaki hiki, sitaki kile na nimechoshwa na hiki. Hii ni lugha ya UVIVU na UZEMBE.

Kama FUNDI MCHUNDO nasema hivi:
Tuanze na maneno machache sana ya "nilikuwa sitaki hiki/nimechoshwa na hiki na kuanzia sasa NINAANZA KUREKEBISHA HIYO HALI...."

Wanayamwezi twasema "mmulika nyoka, huanzia miguuni..." Je nyie mwaanzia wapi?

Tuanze sasa kujadili solution na si matatizo kwani hayo YANAELEWEKA.
 
Sitaki Tanzania iwe "mtazamaji" wakati nchi zingine ziki songa mbele. Nguvu tunayo, uwezo tunao lakini inaelekea tumekosa nia. Nchi yoyote maskini kusonga mbele ina hitaji kila mwananchi katika nafasi yake achangie katika maendeleo ya nchi. Work, work and more work.

Tuna hitaji viongozi wanaojua Tanzania ni nchi changa na hawa takiwi kushindanisha mishahara na marupurupu yao na nchi zingine. Tuna hitaji viongozi wasio wezi maana ina maana jasho lote la Watanzania ni la bure.

Tuna hitaji mikakati ya muda mrefu na muda mfupi. Mikakati practical & achievable at the set time frame na si ndoto za alinacha. Tuna hitaji nguvu kazi itakayo weza simamia na kushugulikia mikakati hii na kuhakikisha kila kitu kinaenda sawa.

Tuna hitaji wanawake waliosoma. Nchi yetu ina hitaji wasomi wengi iwezekanavyo.Wanaume na wanawake wote wana hitahi kuelimika.

Tuna hitaji mfumo utakao andaa vizuri watoto kuja kuchangia katika maendeleo ya nchi na kwa vijana kuwa taifa la leo badala ya la kesho. vijana wana takiwa kuwa proactive na si reactive katika kila kitu.

SITAKI TANZANIA IENDELEE KATIKA HALI ILIYO NAYO SASA. SITAKI NIFE NIIACHE NCHI KAMA NILIVYO IKUTA WAKATI NAZALIWA.
 
You can't discuss the solutions without discussing the source of the problems.You can't get to thesource of the problem without discussing the problem. Kujua tatizo ni nini pekee haitoshi. It has to be deeper than that. Kukwepa kuya ongelea matatizo haimaanishi matatizo hayo hayapo. Je uta pangaje mikakati ya kutatua matatizo bila kujadili matatizo hayo? Tunao walipa pesa zetu za kodi ndiyo wali takiwa kufanya hivyo kwa ajili yetu, wao wameshindwa so why not do it ourselves?
 
Mkuu, haya ni maneno mazito sana!
 
Mkuu,
Watu wa ujenzi siku zote huwa tunafahamu kuwa, dawa ya matatizo yote ni kuanza. Ukisimama na kusema uyajadili kwanza ni kwamba hutafika mbali. Ndiyo maana huwa kuna plan za kazi kwa ujumla ila zile in detail zinakuwa zinafanywa kwa kila wiki inayokuja kwa kuangalia ile plan kubwa.

Matatizo ya Tanzania yanajulikana sana sana. Kwani nani hayatambui? Labda kama hayupo Tanzania au hajawahi kufuka kabisa. Sasa kuanza kusema sitaki hiki wala kile, THEN WHAT???

Inabidi kufika sehemu tuwe kama Mwanakijiji na kuanza kupigana kuibadili hiyo hali kwa njia moja au nyingine. Ningelitegemea watu waanza kusema "pale anapokaa, ataanza kuwakusanya watu ili kujenga mazingira ya usafi, kutunza barabara, kupanda miti na mauwa nk nk". Hii SITAKI haisaidii chochote na matatizo ya Tanzania yameshasemwa sana.
 
  1. Sitaki Tanzania inayowaachia wavunja haki za binadamu na wauwaji kutembea huru.Huko visiwani askari jeshi na polisi wameuwa na hakuna hata kesi waliyofunguliwa au hata serikali kusema chochote juu ya mauwaji hayo.Ikionesha kuwa walihalalisha mauwaji ya wapemba!Hii si mara ya mwanzo, kwa wapemba kuuliwa ilishafanywa kabla na kuhalalishwa kwa kuitwa mapinduzi!
  2. Serekali inayowabana wapemba siitaki, kiuchumi.Mfano mafuta ya Zanzibar, kodi za mabenki na mengi yanayoendelea kuibuka huko baraza la wawakilishi...bila ya kujibiwa na bunge, kwani yote ni kweli?🙄
  3. Sitaki serekali yenye lengo na madhumuni ya kufuta utaifa wa Zanzibar, hili ndio lengo.Iko wazi kuwa Tanganyika ni sawa na Izraili na ajenda zake za siri za kuimeza Zanzibar kwa kutanua mipaka!
I will stop there...but there is more.......😕
 
Staki kuona serikali inayokumbatia wezi na watapanyaji wa rasilimali za nchi

staki kuona serikali inayotoa ahadi za uongo za kutupima viatu kila baada ya miaka mitano.

staki kuona serikali ambayo ina kigeugeu,mwaka huu ikisema hivi mwaka kesho inabadilisha maneno
 
SITAKI KUSIKIA VISINGIZIO VYOVYOTE KUHUSU UMASKINI WA NCHI HII, midhali sababu zinajulikana tuchukue hatua. Hatua ya kwanza ccm OOOUT!
 
sitaki kusikia nyote mkizungumzia hili bila kulichulia uzito unaostahili.
NATAKA kila mtu aanze kuijenga Tanzania akianzia na Familia yake,na jirani yake wa kulia kwake,kushoto kwake mbele na yule aliye upenuni na mahali anapoishi.
SITAKI kusikia mkisema Tanzania ni NCHI MASIKINI.
 
sitaki na tena sipendi wapiga kura wanaoilaumu ccm kwa kutokuteleza ahadi inazotoa wakati wa uchaguzi lakini hao hao wanaolaumu wanawapigia kura wabunge wa ccm.

sitaki, sitaki, sitaki unafiki wa aina hii unao wapa kiburi wabunge wa ccm.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom