Sitaki kuolewa

Sitaki kuolewa

Rapunzel

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2012
Posts
1,079
Reaction score
600
Wasalaam wana MMU,

Yaani weekend yangu ya leo imeharibika sana . Leo nimepata simu toka kwa mama zangu wadogo wakihitaji wedding dress ya mdogo wangu ambaye anataraijia kuolewa hivi karibuni niwatumie Tz ,baada ya maongezi mada ika badilika nikapachikwa swali WE NAWE UNAOLEWA LINI?

Maana wadogo zako wote wanaolewa we bado upo tu unafikiria nini haswaa? Mwingine akadakia "Olewa basi uondoe japo mkosi", kha! This is too much... Hivi jamani kuolewa ni kutoa mkosi?

Msimamo wangu:

1. Sitaki kuolewa kwa kuondoa mkosi

2. Sitaki kuolewa kwa sababu eti umri unaenda

3. Sitaki kuolewa eti wadogo zangu wote wanaolewa

4. Sitaki kuolewa kuwalingishia watu kwa na mimi nimeolewa

5. Sitaki kuolewa ili nivae shela au pete za ndoa kama fashion (ndoa sio fashion)

6. Sitaki kuolewa eti umri unakwenda kwa hiyo yoyote atake kuja mbele yangu anioe tu kisa naingia 30 ....Nope

Ladies haya ni makosa makubwa sana ukiyaamua kwa kufuata maneno ya watu kisa hujaolewa....matokeo yake unaolewa mchana usiku unaachika ni kutojiamiani na maisha yako.

XoXo
 
enh nilishtuuuuka!
nkajua mke wetu unapeperusha zile ahadi za kaka!
usinishtue hivo siku nyingine wiwi!
ngoja nipumue kwanza af ntarudi kuchangia content!maana hiyo heading ilinipandisha sukari mwenzio!
 
Wasalaam wana MMU,

Yaani weekend yangu ya leo imeharibika sana ...

Leo nimepata simu toka kwa mama zangu wadogo wakihitaji wedding dress ya mdogo wangu ambaye anataraijia kuolewa hivi karibuni niwatumie Tz ,baada ya maongezi mada ika badilika nikapachikwa swali WE NAWE UNAOLEWA LINI?
Maana wadogo zako wote wanaolewa we bado upo tu unafikiria nini haswaa?
Mwingine akadakia "Olewa basi uondoe japo mkosi",
kha! This is too much... Hivi jamani kuolewa ni kutoa mkosi???

Msimamo wangu:
1. Sitaki kuolewa kwa kuondoa mkosi

2.Sitaki kuolewa kwa sababu eti umri unaenda

3. Sitaki kuolewa eti wadogo zangu wote wanaolewa

4.Sitaki kuolewa kuwalingishia watu kwa na mimi nimeolewa

5.Sitaki kuolewa ili nivae shela au pete za ndoa kama fashion
( ndoa sio fashion)

6. Sitaki kuolewa eti umri unakwenda kwa hiyo yoyote atake kuja mbele yangu anioe tu kisa naingia 30 ....Nop

Ladies haya ni makosa makubwa sana ukiyaamua kwa kufuata maneno ya watu kisa hujaolewa....matokeo yake unaolewa mchana usiku unaachika ni kutojiamiani na maisha yako.

XoXo

Good. Be yourself never be carried away by the wind. Kama ipo, itakuwepo tu. GOD will bless you to get what is appropriate for you and at the most appropriate time.
 
Good. Be yourself never be carried away by the wind. Kama ipo, itakuwepo tu. GOD will bless you to get what is appropriate for you and at the most appropriate time.

by the way kuoa au kuolewa siyo lazima. mitanzania badala ya kusaidiana economic status yenyewe yanaulizia yaje kukata mauno kwenye sherehe tu.
 
kweli kabisa kuoa au kuolewa ni kipendeleo cha mtu lakini wabongo tunavyoshadadia utafikiri tutaishi na huyo mtu kwenye hiyo ndoa,tunachofikiria ni kupata ujiko mtaani bila kujali ugumu wa ndoa yenyewe...........muwawache wapumuwe
 
Lisemwalo lipo!

Sioni kama kuna tatizo kuulizwa eti unaolewa lini, kumbuka na wewe ungeweza kuwatumia kiusahihi kwa huo muda waliokuuliza hilo swali...

Ina maana huna malengo yoyote/huna mchumba mpaka dakika hii?
 
Mmmmmmmh! Narudi kutoa sitaki zangu nikimaliza kisa cha Mlokole!
 
Good or bad ts ya thinking capacity and ur courageous. .congrats my lady. .we girls needs uelewa wa hal ya juu about ourselves. .
 
kama haya ulioandika hapa yanatoka moyoni mwako na unamaanisha basi wewe unajitambuwa na ni mke bora kabisa hapa duniani. nimependa brain yako kudos.

I mean it toka moyoni kabisa...wananikwaza sana hawa wanafamilia
Ukiama kuolewa, mkisalimiana kinachofuata utaolewa lini? Wananichosha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom