Sitaki dawa



Your ignorance isifanye kupotosha watu.

Sasa wapi hapo huyo profesa kazungumzia kuwa kirusi cha HIV hakiexist au hakipo?

Kirusi yupo na anaonekana, omba ueleweshwe.

Hapo kwenye hiyo video huyo profesa kazungumzia nini cha zaidi ya kula vizuri, kufanya mazoezi kubadilisha life style ili kupunguza oxidants mwilini?
 
kama hayo uliyoandika ndio pekee uliyoelewa katika ile video,basi unathibitisha jinsi unavyotembea na mwili huku akili imeshikwa na wengine.Labda kiingereza ni shida kidogo,sitakulaumu kwa hilo.Ukitaka kuthibitisha kama hujaelewa hiyo video basi jaribu kumuuliza mwingine akuelezee alivyoelewa yeye,lazima atakueleza zaidi ya hayo uliyoeleza wewe kama mtu huyo anajua vizuri kiingereza na anajua pia kusikiliza.Au JF members wengine watakuelezea,mijadala hii sikuanza leo humu JF,nilishajadili hadi na madaktari humu.Sasa kama madaktari wenye fani yao walikosa point za msingi,itakuwa wewe?Sitakulaumu kwa kuwa najua uko ktk kipindi cha mpito kiuelewa,mimi nilishapita huko zamani sana.
 
Pole sana mkuu duh! Kwanzia sasa najirekebisha coz na mimi ni mchafu hamna mwanamke apite machoni mwangu nisimgegede tena kavu but niko safi lakini napoelekea si pazur aise
 
Kama ni imani inakuwaje kwa watoto wanaozaliwa na HIV? Si ingetokea kwa watu wengine.
 
Mkuu I still think this is like any other story humu. Naona pia hata diagnosis iliyoandikwa kwenye form yako ya hospital uliyo-attach inaonyesha tatizo lako ni PUD. Meaning una vidonda vya tumbo (Peptic Ulcer Disease). Ingawa inaonyesha kweli kipimo cha ukimwi kilifanyika lakini majibu umeyaficha.

Unless, daktari aliyeweka hiyo diagnosis yako ni kimeo au kilaza, ninazidi kuamini kuwa inawezekana kweli umepata hiyo scholarship na ukapima lakini majibu sio positive for HIV ila unajaribu kuelimisha na kukumbusha watu wawe makini kwenye pitapita zao kwasababu ukimwi upo.

However, vyovyote vile iwavyo, kama kweli mkuu umeathirika, nakupa pole. Lakini zaidi sana na kwa dhati kabisa nakupongeza kwa uamuzi wa kupima, japo ilikuwa coincidental. Mshukuru Mungu umejua status yako. Usijichukie. Mungu ana makusudi yake mkuu.

Hali unayoisikia sasa hivi ni reaction ya kawaida sana pale mtu unapopata taarifa mbaya kama hizo. Hasa ukizingatia kuwa ni tatizo utakaloishi nalo forever.

Nakusisitizia mkuu kuelewa kuwa huo sio mwisho wa dunia. Kuna magonjwa ya kutisha zaidi lakini sio ukimwi. Nakuomba usijiadhibu. Uamuzi wa kutokutumia dawa ni wa kujiadhibu. Sio sawa hata kidogo.

Tafadhali sana:

1. Zingatia ushauri uliopewa na utakaoendelea kupewa na madakari. Kubali kutumia dawa accordingly.

2. Endeleza mipango yako yote ya maisha. Pursue your dreams bro. Hiyo ni status tu. Sisemi hutakufa. Lahasha. Kila mtu atakufa siku yake ikifika. Unaweza kuishi na ukimwi for over 20 years. Na kwa taarifa yako ukimwi unaweza usiwe sababu ya kifo chako. Most importantly, you need the right attitude bro. Kung'uta vumbi hilo maisha yaendelee.

3. Hakikisha unabakia safe brother...to yourself and others. Jikinge mwenyewe usipate maambukizi mapya (hii ni broad subject) na jitahidi usiwaambukize wengine. Protected sex is one of the ways to go.

4. Ukihitaji rafiki na mshauri, I can always give you a hand, in any way possible, my brother. Just give me a shout.

Genuine salute to you my brother Mentor kwa kutoa mafundisho muhimu kupitia thread hii yako.
 
Pole sana ndugu yangu. Nimewahi kuwa katika wakati wa kutafakari nikiwa nasubiri majibu kutokana na nafasi ya ndoto yangu niliyoipata kwa neema ya Mungu nikatoka mzima.

Kwa ufupi unarudi kuwaza jinsi ulivyoishi katika jamii na familia. Unakumbuka njia ulizopitia na kuuona ujinga uliowahi kuufanya japo kwa wakati huo ulidhani ndo kula maisha.

Kuna mijadala mingi tunajadili humu kuhamasishana na kujivunia ngono, lkn likikutokea ndo unapogundua mchango pekee wa watu waliokuona unaweza ni POLE na hamna zaidi. Tunaishia kujuta na kuacha simanzi kwa wapendwa lakini pia kukatisha ndoto zetu.
 
Hmmmmm! Dah! Pole sana Mkuu lakini huo ugonjwa si hukumu ya kifo. Waathirika wengi ambao hutumia dawa wanaishi kwa miaka mingi tu na kuweza kufanya shughuli zao za kila siku bila matatizo yote. Sioni sababu ya wewe kuamua kutotumia dawa. Pole sana Mkuu.
 
Pole sana Mkuu ucfe moyo.. Mbona watu tumezaliwa navyo na bado tunaish ondoa hofu kabisa.. Mungu atakupa nguvu.. Kila nafs itaonja umaut so hakuna anayejua atakufaje na pia unaweza ucfe kwa ugonjwa huu na ukaja kufa na kitu kingine kabisa... Watu wanakufa hata kwa ajali.. Mshukuru Mungu kwa yote... Cjawah kujutia kuzaliwa na hali hii ila nilisikitika mama angu alipofarik nakuniacha nikiwa Mtoto sana cjielewi
 
Kinachosikitisha ni kwamba niliwahi kusoma humu kwamba baadhi ya waathirika hutoa rushwa ili waandikiwe kwamba ni wazima wa afya. Sasa kama kuna jamaa KE/ME amemuomba akapime kabla ya kupiga hatua kwenye mahusiano yao ya kimapenzi watu kama hawa ni waambukizaji wazuri kwa sababu mwenzie huamini kwamba afya yake ni njema kabisa hivyo hakuna sababu ya kutumia kinga, kumbe anaendelea kuusambaza. INATISHA SANA.

 
Yeah..? Kama mim nilianza kutumia dawa nikiwa na miaka 10 mpaka Leo na miaka kama 15 natumia ARVs na nipp fresh nafanya shughul zangu kama kawaida... Sion kama ni kitu cha ajabu na ukwel hukuweka huru na kukuondolea msongo wa mawazo coz unakuwa umeshajikubal.. HIV is conditional.
 
Pole sana Mkuu na ahsante kwa kufunguka hapa jamvini kuhusu hali yako.

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…