Sitaki dawa

Sitaki dawa

Deception
Nimegundua majority wanakupuuza so you may change course of your facts, they are either not believed, encouraged or pipo don't want to duscuss them

It's better to be feared than ignored- 48 laws of power

be blessed.....
Ukiishi kwa kuangalia watu wanakufikiriaje utakuwa mtumwa katika maisha yako yote,hali hiyo inaweza ku dictate hata maamuzi muhimu utakayoweza kufanya katika maisha yako au ya wengine.Kamwe usiruhusu hali hiyo ikutawale.Kumbuka kila mtu ana uhuru wa kufanya jambo analolipenda,mada kama hizi si za kulazimishana hata kama ni muhimu katika maisha ya watu.
Kumbuka pia kuna watu wengi wanasoma uzi huu hata kama hawachangii humu.Hivyo sikulenga hadhira ya humu peke yake,kuna hadhira ya nje ya hapa pia wanasoma uzi huu.Kati ya watu 100 ukiokoa hata mmoja nayo ni step kubwa,yule mmoja ataokoa wengine na chain itaendelea.Mabadiliko yoyote yale huwa hayatokei ghafla,huja taratibu na kuna changamoto zake pia.

Ninapokuwa najadili mada kama hizi huwa siangalii watu kama wanapuuza au la,hata kama atatokea mmoja tu anayehitaji msaada nitakwenda na huyo mmoja hadi mwisho.
 
2.Kuhusu watoto wako kinga kushuka;ni rahisi sana,kama ni kweli kinga za watoto wako zinashuka,kunaweza kuwa na matatizo yafuatayo;

-Huwapi chakula bora-mboga za majani,ulezi,mtama,dona,soy,matunda nk
-Inawezekana watoto hao unawapa sana dawa fulani fulani za hospitali mara kwa mara
-Mazingira wanayoishi si masafi,hivyo hushambuliwa na maradhi mara kwa mara
-Inawezekana pia chakula na vinywaji wanavyotumia si vizuri kutokana na umri wao.Wape juisi za matunda halisi,usiwape juisi za viwandani,wape supu ya mboga za majani,wape uji/ugali wa dona/ulezi/mtama au soy.

Mambo mengine ningeweza kukushauri vizuri kama ningewaona watoto wenyewe na kujua mazingira wanayoishi.
Jibu zuri lakini vipi kuhusu watoto wa familia moja unakuta mmoja yuko HIV+ na mwingine yuko HIV- ila huyu mwenye + anapoteza afya kudhoofu na kufa kwa magonjwa yanashambulia mwili usio na kinga ya kutosha. Haya yanatokea wakati ambapo watoto wote hawa wawili wanalelewa katika mazingira yaleyale ikimaanisha kuwa lishe na mazingira yanafanana kwa 99.9%. Huoni kuwa kuna uwezekano HIV inaongeza uwezekano wa kupunguza nguvu ya kinga kwa haraka katika mazingira kama haya?
 
Jibu zuri lakini vipi kuhusu watoto wa familia moja unakuta mmoja yuko HIV+ na mwingine yuko HIV- ila huyu mwenye + anapoteza afya kudhoofu na kufa kwa magonjwa yanashambulia mwili usio na kinga ya kutosha. Haya yanatokea wakati ambapo watoto wote hawa wawili wanalelewa katika mazingira yaleyale ikimaanisha kuwa lishe na mazingira yanafanana kwa 99.9%. Huoni kuwa kuna uwezekano HIV inaongeza uwezekano wa kupunguza nguvu ya kinga kwa haraka katika mazingira kama haya?

Kama huo mfano ulioutoa ni hai/upo yaani umeushuhudia wewe mwenyewe,basi naomba unijibu maswali yafuatayo:
1.Je hao watoto wamezaliwa na mama aliyepimwa HIV+ au HIV-?Hapa sina maana ya kwamba nakubaliana kwamba kuna HIV,la hasha bali kuna jambo nataka kujua.Jambo hili lina tricks nyingi sana,unahitaji utulivu kidogo ili uelewe.Nataka ufahamu kwamba vipimo ndio tatizo kubwa sana.

2.Ni sababu zipi zilizofanya hao watoto wakapimwe huyo HIV?

3.Wakati wanapimwa walikuwa katika hali gani kiafya?Walikuwa wanaumwa au walikuwa na afya njema?Kama walikuwa wanaumwa,basi taja walikuwa wanaumwa nini?

4.Je,huyo ambaye alipimwa HIV+ alianza kutumia ARVs?Kama alianza,alitumia ARVs kwa muda gani?Nitajie jina la ARVs aliyokuwa anaitumia kama alianza.

5.Huyo ambaye alikuwa ni HIV+ unasema alikuwa amedhoofu na alikuwa na magonjwa.Tafadhali,naomba unitajie magonjwa yote yaliyokuwa yanamsumbua.Kuna jambo nataka kujua hapo.

Sasa ili tuwe realistic zaidi,naomba usifoji majibu,kama hujui/umesahau niambie.Nijibu kitu ambacho una uhakika nacho,usitunge au kudhania kwa maana tutaharibu uhalisia wa jibu nitakalokupa.Ndio maana mwanzo nilisema kwamba kama ningewaona hao watoto ningejua sababu halisi kwani mimi mwenyewe ndio ningefanya uchunguzi kwa kuuliza maswali papo hapo na vitu vingine ningeviona kwa macho.Sasa nijibu kwa ufasaha kabisa ili jibu nitakalokupa liwe na uhalisia.Jibu kwa mtiririko wa namba kama nilivyokuuliza.
 
SITAKI DAWA

Jumamosi, 25/06/2016

Nawaza nianzie wapi kuelezea kilichonikuta nashindwa, lakini hasa ni kukosa maneno ya kukielezea. Nimetamani nikae kimya, nisiseme, maana ninafahamika na wengi na itaniharibia picha yangu kwenye jamii. Nimetafakari sana kuchukua maamuzi magumu lakini nfasi yangu haikuumbwa hivo, nimeshindwa. Labda ningezaliwa Mhehe, lakini mchagga mimi hata vidonge vya piriton vilikuwa shida kumeza.

Lakini nimeamua nitasema. Sijui baada ya kusema nini kitatokea, sijui jamii itanichukuliaje, ndugu jamaa na marafiki watasemaje au labda watanitenga…lakini nitasema.

Wazazi wangu – MNISAMEHE! Zaidi ya yeyote yule nimewaangusha. Mlikuwa na mategemeo makubwa juu yangu. Mmenisomesha kwa gharama kubwa na mlikuwa na matumaini ya mimi kufika mbali.

Mlioniita Mentor – MNISAMEHE! Najua ni wengi walioniona kama kijana wa mfano, kaka na ndugu…mnisamehe kwa kuwaangusha. Sitamsingizia shetani wala mtu mwingine yeyote kwa kosa langu.

NIMEATHIRIKA! Na sijivunii…

July, 2015

Naamini ni wakati huu. Kulitangazwa nafasi za masomo nchini Uingereza chini ya ufadhili wa Commonwealth (Common wealth Scholarships 2015). Nami nilikuwa nimejiwekea malengo kuwa hadi mwaka 2016 ni lazima nikasome masomo yangu ya Uzamili (masters) hata ikibidi kwa kujilipia. Nilitembelea tovuti tofauti tofauti nikitafuta ufadhili kwa ajili ya masomo yangu. Hakuna tangazo lililotolewa ambalo sikuliomba. Fulbright, Mwalimu Nyerere, DAAD, World Bank, IMF, n.k n.k niliomba zote. Nilikuwa na malengo ya kwenda kusoma masomo ya usimamizi wa miradi au utungaji sera. Ndoto yangu ilikuwa moja tu: SIKU MOJA NIWE KATI YA WAFANYA MAAMUZI KATIKA NCHI HII.

Nilichoka kuwa mtu wa kuandika programs kila siku halafu aidha fedha zinaliwa au miradi inawekwa kwenye shelfu. Nilichoka kuhusishwa kwenye miradi isiyo na kichwa na miguu, miradi isiyoangalia vipaumbele vya taasisi au nchi. Nilichoka! Nikasema nitaachana na masomo yangu ya sayansi ya kompyuta nikasome masomo yatakayonifanya niwe mtunga sera na mtoa maamuzi. **** ME!!!! (mnisamehe am so mad at me)

Wakati huu ndipo kulipotangazwa nafasi hii ya Commonwealth. Nakumbuka nililiona tangazo kupitia tovuti ya TCU na ilikuwa imebaki wiki moja au mbili hivi kabla ya tarehe ya mwisho kwa hapa kwetu. Nilijipinda ofisini kuandika insha kama tatu kuelezea kwa nini mimi niipate nafasi hii na si mwingine. Niliandika kutoka moyoni. Nilifanikiwa kumaliza mapema nikatoa nakala kama walivyoelekeza; za kupeleka wizara ya elimu na za kutuma kwa barua pepe.

Siku, wiki na miezi vilipita nami nikaitwa kwenye usaili, nikaenda kufanya mitihani ya Kiingereza ya IELTS pale ubalozi wa Uingereza, nikafaulu vizuri.

Alhamisi, 23 Juni 2016 - Juzi

Nilipewa majibu kuwa nimechaguliwa pamoja na wenzangu wawili kwenda Uingereza (chuo sitokitaja) kwa ajili ya masomo ya Uzamili katika Usimamizi wa Miradi kuanzia mwezi wa tisa. Nilifurahi sana, nikapiga magoti ofisini nikamshukuru Mungu kuwa mwaminifu kwangu. Nilimuomba mwaka huu niende shule na amenijibu. Tena kaniongezea baraka kwa kuwa ninapewa ufadhili wa 100%. Hakuna hata senti yangu nitakayotumia katika maosomo yangu hayo.

Jana asubuhi nilitumiwa mkataba wangu pamoja na fomu za afya ambazo nilitakiwa kuzijaza na kuzirudisha ubalozi wao Jumatatu kwa ajili ya mipango mingine; visa na kuomba ruhusa kwa Katibu Mkuu Kiongozi (serikali ya tano hii!).

Kwa ile hamu niliyokuwa nayo wala sikuweza kubaki tena ofisini nikajiondoa kuelekea mnazi mmoja maana nilijua hilo sio suala gumu. Nilishazoea kibongobongo hakuna kufanya vipimo na kwa kuwa nilishaulizia kuhusu visa za Uingerea nilifahamu huwa hawafanyi vipimo vya afya vingine zaidi ya kile kilichoandikwa kwenye ile fomu. Hivyo niliamini wala lile zoezi lisingechukua zaidi ya nusu saa. Niliingia kwenye ATM ya bwana Kimei pale posta nikachukua fedha ya kutosha kwa ajili ya kumshukuru daktari atakayenisainia fomu zangu.

Nilimkuta mmama mmoja!dah nikamsalimia na kumueleza kilichonipeleka pale. Nilishangaa alipochukua kikaratasi chake na kuanza kujaza vipimo ambavyo nilitakiwa kwenda maabara kupima kabla hajanijazia fomu yangu. Nilitamani kuondoka lakini nikakumbuka ameshaichukua fomu yangu na alijua ninataka kuondoka akaiweka kwenye droo na kunikabidhi kile kikaratasi nielekee maabara. Nilijaribu kumuomba kwamba nimetoroka kazini anisainie tu na kupiga muhiri nami ningemshukuru vizuri tu. Alikataa na kunitaka niende kupima.

Niliondoka huku nikisoma kile kikaratasi ila nilipofika kwenye hili neno PITC nikashtuka kidogo. Ufadhili (scholarship) nautaka na vipimo sivitaki nifanyeje sasa, ikanibidi nielekee maabara. Nikaelekezwa kwenye dirisha la kulipia nikalipa (nilisahau kabisa kwamba nina bima ya afya hiyo jana). Nikarudi kwenye kiti changu kusubiri wakati wangu wa kuitwa.

Palikuwa na makelele na kulikuwa na nesi mmoja anaita watu majina. Namkumbuka kwa kuwa alikuwa na sauti kubwa kuliko mwili wake.

MAGRETH! MAGRETH!” aliita kwa nguvu. –kimya

Akaendelea kuita jina lingine, “JACKLINE!” “JACKLINE!

Mh! Haya majina mawili kwa pamoja yakanikumbusha Changanyikeni.

Sikumbuki siku kamili!

Nilikuwa na rafiki yangu tuliyeshibana sana toka utotoni, Arnold. Huyu jamaa ndiye aliyenifundisha ule msemo wa KUPATA UKIMWI MPAKA UWE UMELOGWA. Nami niliuamini maana michezo niliyoicheza ujanani tena pekupeku sikuwa nimeathirika, kweli mpaka uathirike ni lazima ulogwe.

Ndiyo, kuna nyakati nilijua sijaathirika kabisa kwa kuwa mara nyingi mabinti niliokuwa nao kwenye mahusiano walikuwa wakiniambia. Nakumbuka huyu mmoja ambaye alinifuma nikiwa choo cha klabu na mwanamke mwingine ambaye hata jina sikuwa nikimfahamu. Alinikuta nikifanya naye mapenzi pasi na kinga. Nilikuwa nimeshazoea.

Huyu ndo alinifumbua macho siku moja miezi michache baada ya kuachana nami kuwa kitu cha kwanza alichoenda kufanya baada ya usiku ule ni kwenda kupima ambapo alipojikuta hakuathirika alishukuru sana. Ndipo nami nikagundua kumbe sikuathirika. Niliifanya kama mchezo kwamba kila binti niliyeachana naye; kumuacha au mara nyingi yeye kuniacha, baada ya miezi michache nitamuuliza kama amepima na mara ningi huniambia wako poa. Nami hujua niko vizuri.

Ah! Jacky na Mage

Nakumbuka ilikuwa siku niliyotoka ubalozi wa Uingereza ambapo niliambiwa nimepita usaili na nijiandae tu kwa ajili ya mitihani ya kiingereza. Baada ya kufanya utafiti mfupi niligundua mitihani ile si migumu na kwa watu wote tuliopita usaili mimi nisingeweza kukosa ufadhili ule kwa kamtihani kale karahisi ka kiingereza.

Nilimpigia simu Arnold na kumuambia tukasherehekee. Tulienda Samaki samaki ambapo tulikutana na Jacky na Mage, tulisoma nao o-level huko Moshi. Tulipiga stori sana na kwa kuwa nilikuwa nasherehekea mimi ndo nilikuwa mnunuzi. Walikunywa vya kutosha kiasi kwamba wakati wa kuondoka wale mabinti hawakuweza kwenda peke yao. Ilikuwa kazi rahisi sana kuwashawishi twende kwangu Changanyikeni kwa kuwa pia ilikuwa ni siku ya Ijumaa. Tuliingia kwenye kausafiri changu hao mpaka Changanyikeni. Safari moja ikapelekea nyingine na yaliyotokea kule – sijivunii – na sitayaelezea na hatukuwa na kinga yoyote. Na wala siwezi kusingizia ulevi maana mimi huwa situmii kilevi chochote.

Mentor! Mentor!”

Sauti ya nesi yule ikiniita ilinishtua kutoka kwenye dimbwi la mawazo. Ulikuwa ni wakati wangu kwenda kwenye vipimo.

Nilinyanyuka na kuelekezwa kwenye chumba kingine ambapo nilipoingia sikukuta hata dalili za sindano. Kumbe ilikuwa kwa ajili ya vipimo vingine vilivyokuwa kwenye karatasi ile. Nilipima uzito, urefu, pressure, na mengine kama hayo kisha nesi akaniambia nirudi kukaa kwenye benchi.

Hapo akili yangu ikaniambia kuwa kinachofuata sasa ni ukimwi. Nilikaa nikitafakari kama kweli ninaweza kuwa nimeathirika. Akili yangu ikakataa.

Usiku wa Mwaka mpya 2016

Najua wengi mnaonifahamu hamtaamini mkisoma hapa – MNISAMEHE! Wengi walinifahamu kama kijana Mkristo safi ninayeenda kanisani kila Jumapili. Hata kanisani kwangu ni mmoja wa viongozi wa vijana – nafasi ambayo niliitumia vibaya kuendeleza tabia yangu mbaya chini ya kapeti.

Nilienda kwenye mkesha wa mwaka mpya. Tuliimba na kusherehekea sana na moyoni mwangu nilijiwekea malengo kuwa mwaka huu mpya nimtafute binti mmoja nitakayempenda na kutulia naye maana umri nao haunisubiri.

Nilidhamiria kupunguza kwa kiasi kikubwa tabia zangu mbaya hasa ukizingatia mema mengi ambayo Mungu amekuwa akinifanyia bila kustahili kwangu. Ni katika kuwaza huku ndipo macho yangu yalipodondoka juu ya msharika mmoja. Hadi wakati tunatoka ibada usiku ule tulikuwa tumeshafahamiana vya kutosha.

Itoshe kusema tu kuwa hatukufanikiwa kwenda kwenye ibada asubuhi ya tarehe 01/01/2016 kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu. Na hatukutumia kinga. Ni katika kuwaza huku ndipo nilipokumbuka kuwa juzi juzi tu alikuwa akiumwa na hakutaka kuniambia anaugua nini. “Atakuwa ameathirika?” nilijiuliza. Lakini nikajifariji kuwa KUPATA UKIMWI NI HADI ULOGWE. Ni nani wa kuniloga mimi Mentor, mtu wa watu, kwa kosa lipi nililomfanyia?

Jina langu lilitwa tena na kwenda kwa ajili ya vipimo vingine vilivyohusisha damu kuchukuliwa.

Nilitamani kuondoka pale kwani sikuwa nimeomba ruhusa ofisini lakini pia nilitakiwa kuondoka na fomu zile. Ilinibidi kusubiria.

Akili yangu ilikuwa ikisafiri mbali. Nilijiuliza maswali mengi kuhusu afya yangu ambayo sikuwa nimewahi kujiuliza kabla. Nilifanya mambo yangu mengi kwa siri kiasi kwamba ni vigumu mtu yeyote akihadithiwa haya kuyaamini. Lakini kwani UKIMWI unawapata waliofanya kwa wazi? Lakini hapana mimi siwezi kuwa nimeathirika. Kutoka kwa nani labda?

Nikamkumbuka Amina, huyu alikuwa mdada wa usafi ofisini. Kama tabia yangu nimezoea kusalimia kila mtu na huyu dada tulikuwa tukikutana asubuhi wakati naingia ofisini hakukosa salamu yangu.

Pamoja na tabia yangu ya kupenda kuwahi ofisini hakuna siku niliyowahi kwenda ofisini nisikute ameshafika. Tukazoeana sana. Nami kidogo kidogo nikaanza kumzoea na kumchokoza kwa vimaneno vya hapa na pale.

Kuna zile siku unaamka mapema, unajisikia vizuri, unaoga unavaa unaingia kwenye gari unaondoka kwenda kazini mapema ukitegemea kutakuwa na foleni kubwa kumbe unapofika barabarani unatumia robo saa tu kufika ofisini. Hii siku ilikuwa hivyo. Na nilipofika saa kumi na mbili kasoro bado nilikuta Amina amekwishafika. Na kwa bahati zaidi alikuwa akifanya usafi ofisini kwangu. Sitaki kuelezea zaidi lakini itoshe kusema usafi uliishia palepale. Na hatukutumia kinga. Baadaye Amina alikuja kuzushiwa maneno kuwa anatembea na mabosi wangu wengine na eti ameathirika hivyo akafukuzwa na sikumuona tena. Sikuweza kumuuliza kama alipima au la!

Lakini hapana, wakati ninakutana na Amina nilikuwa na rafiki wa kike, Hamida, na Hamida tulipoachana alienda kupima na hakukutwa na virusi. Nilitabasamu kugundua kuwa niko vizuri.

Lindi hili la mawazo lilikatishwa tena na nesi yule yule aliyeniita nyakati zilizopita. Niliangalia saa yangu iliyonionesha kuwa ni saa mbili zimepita tangu nifike pale.

Niliingia kwenye chumba ambacho nilijua tu ni kwa ajili ya ushauri. Nilimwomba nesi aniandikie majibu yangu kwenye kile kikaratasi pamoja na yale majibu mengine niwahi kwa daktari maana natakiwa kurudi ofisini. *sasa ndio naelewa* maana aliniangalia kwa huruma sana huku akivikusanya vikaratasi vile na kuondoka navyo huku akiniambia nisubiri. Alienda kumuita yule daktari aliyeniandikia vipimo.

Jumamosi, 25 Juni 2016

Nimeikatisha ndoto yangu mwenyewe kwa umalaya wangu. Nakumbuka siku ya usaili yule mzungu aliangalia fomu zangu baada ya kunisikiliza na kusoma insha zangu aliniambia, “Young man! If what you have written and have just told us comes from your heart, then I wish you all the best.

Nimeikatisha ndoto yangu kwa kuishi maisha mawili. Nakosa hata ujasiri wa kutubu kwa Mungu. Nakosa ujasiri wa kwenda kanisani kesho. Ni nani aliyeniloga?

Pamoja na kupewa ushauri mwingi jana, nimeamua sitokunywa dawa! Nipo tayari kutumikia adhabu niliyojitakia.

Nilirudi ofisini na kujifanya kama hakuna kilichotokea. Baadaye jioni nilijilazimisha kwenda kuangalia filamu pale LAPF Tower (Movie Night) na kwa maumivu makubwa filamu ile ilikuja wakati wa kuchelewa sana maishani mwangu. Inaitwa ‘God’s Compass’. Baada ya kutoka na kuagana na walionialika tena tofauti na siku zote nilikataa kuwapa lift kwenye gari langu na kuwalazimu wajazane wote kwenye gari lingine la mwenzao na kurudi makwao. Nilirudi kwenye gari langu ambapo nilikaa kwa zaidi ya lisaa limoja pale nikilia jinsi maisha yangu yalivyofikia mwisho haraka.

Nimejitahidi kujifanya kama kila kitu kiko sawa kwenye maisha yangu lakini nimeshindwa, nimeishia kulia machozi siku nzima ya leo. Kwa nini Mungu ameruhusu hili linitokee mimi? Kwa nini asingeninyima scholarship na kunipa afya yangu, ningejilipia mwenyewe. Nilikuwa nimeshapanga kuwa kama ningekosa scholarship ningeenda kujilipia pale IFM nisome masomo ya jioni na kwa hakika ningemaliza Masters yangu.

Hii inaweza kuwa hadithi yangu ya mwisho – sikutaraji ingekuwa hii ndiyo hadithi yangu ya mwisho, na iwe ni ya kweli! Lakini niwaombe wote msamaha. Sikuwahi kuamini kama nami ningekuja kuathirika, walikuwa na afya zao, hawakuonekana wameathirika.

Kwa wadada wote mtakaopima na kukutwa mmeathirika kwa sababu yangu – MNISAMEHE.

Wapendwa, hiki ni kisa changu cha ukweli na ndio maana nimetaja baadhi ya vitu/sehemu za ukweli ili walau muone uhalisia. Kama yote niliyowahi kuyaandika humu yatakosa maana kutokana na nilichokifanya basi naombeni neno langu la mwisho mlizingatie…UKIMWI UPO, NAMI MENTOR NIMEATHIRIKA.

Tafadhali msifuate mfano wangu.

Wasalaam na kwaherini,

Mentor.
Kwa wale ambao sio wenyeji wa hili jukwaa na wafatiliaji wa story za mentor ..they might fall in his trap!
 
Ukiishi kwa kuangalia watu wanakufikiriaje utakuwa mtumwa katika maisha yako yote,hali hiyo inaweza ku dictate hata maamuzi muhimu utakayoweza kufanya katika maisha yako au ya wengine.Kamwe usiruhusu hali hiyo ikutawale.Kumbuka kila mtu ana uhuru wa kufanya jambo analolipenda,mada kama hizi si za kulazimishana hata kama ni muhimu katika maisha ya watu.
Kumbuka pia kuna watu wengi wanasoma uzi huu hata kama hawachangii humu.Hivyo sikulenga hadhira ya humu peke yake,kuna hadhira ya nje ya hapa pia wanasoma uzi huu.Kati ya watu 100 ukiokoa hata mmoja nayo ni step kubwa,yule mmoja ataokoa wengine na chain itaendelea.Mabadiliko yoyote yale huwa hayatokei ghafla,huja taratibu na kuna changamoto zake pia.

Ninapokuwa najadili mada kama hizi huwa siangalii watu kama wanapuuza au la,hata kama atatokea mmoja tu anayehitaji msaada nitakwenda na huyo mmoja hadi mwisho.
Mkuu me nimekusomà nimekuelewa. Watu wanaokubishia wengi wanauelewa kidogo kuhusu huu ugonjwaa ndo maana ukiwapa majibu yaliyojitosheleza wanashindwa kujitetea. Ningependa kujua zaidi. Naomba nielekeze uzi mwingiñe uliotoa darasa nijifunze
 
Kama huo mfano ulioutoa ni hai/upo yaani umeushuhudia wewe mwenyewe,basi naomba unijibu maswali yafuatayo:
1.Je hao watoto wamezaliwa na mama aliyepimwa HIV+ au HIV-?Hapa sina maana ya kwamba nakubaliana kwamba kuna HIV,la hasha bali kuna jambo nataka kujua.Jambo hili lina tricks nyingi sana,unahitaji utulivu kidogo ili uelewe.Nataka ufahamu kwamba vipimo ndio tatizo kubwa sana.

2.Ni sababu zipi zilizofanya hao watoto wakapimwe huyo HIV?

3.Wakati wanapimwa walikuwa katika hali gani kiafya?Walikuwa wanaumwa au walikuwa na afya njema?Kama walikuwa wanaumwa,basi taja walikuwa wanaumwa nini?

4.Je,huyo ambaye alipimwa HIV+ alianza kutumia ARVs?Kama alianza,alitumia ARVs kwa muda gani?Nitajie jina la ARVs aliyokuwa anaitumia kama alianza.

5.Huyo ambaye alikuwa ni HIV+ unasema alikuwa amedhoofu na alikuwa na magonjwa.Tafadhali,naomba unitajie magonjwa yote yaliyokuwa yanamsumbua.Kuna jambo nataka kujua hapo.

Sasa ili tuwe realistic zaidi,naomba usifoji majibu,kama hujui/umesahau niambie.Nijibu kitu ambacho una uhakika nacho,usitunge au kudhania kwa maana tutaharibu uhalisia wa jibu nitakalokupa.Ndio maana mwanzo nilisema kwamba kama ningewaona hao watoto ningejua sababu halisi kwani mimi mwenyewe ndio ningefanya uchunguzi kwa kuuliza maswali papo hapo na vitu vingine ningeviona kwa macho.Sasa nijibu kwa ufasaha kabisa ili jibu nitakalokupa liwe na uhalisia.Jibu kwa mtiririko wa namba kama nilivyokuuliza.
Okay, uwezo wa kujibu maswali yako yote kwa ufasaha sina. Ngoja nikatafute case mojawapo niifuatilie kwa karibu halafu tutarudi kujadili panapo majaaliwa.
 
akuu, labda unipime kinguvu

Mi nshapima. Nawe pima uishi!

20160614_134234.jpg
 
Back
Top Bottom