Sisi watanzania bado tuko nyuma sana ya muda

Sisi watanzania bado tuko nyuma sana ya muda

Kwahiyo akili yako umeifanya iamini huo upuuzi.!!? Yaani unaamini binadamu wote wako sawa bila kuwa na tofauti ya kimawazo.!? Inasikitisha sana

Any way mm nimetolea mfano tu, hiyo cryptocurrency ni mfano tu wa matokeo chanya ya teknolojia. Mkuu achana na mambo ya cryptocurrency tuongelee namna dunia inavyo kwenda kasi hasa kwenye suala la teknolojia, je tunaenda sawa? Ama tumekalia mambo ya kipumbavu tu
Hela huwa hazitangazwi.. ukiona mtu anakutangazia mirija yake ujue kuna namna unaenda kuwekwa kati.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ndio majibu yao,Haitatokea afrika hasa Tanzania kufikia ugunduzi na uwezo hata wa kutengeneza midoli
We umetengeneza nini au umegundua nini? Au umegundua kifo Cha mende?
 
Inaonyesha bado hatuko tayari kwa mapinduzi chanya. Sera ya hii nchi pamoja na viongozi wamesababisha kuzalisha wananchi wa ajabu sana.
Haya ndio majibu yao,Haitatokea afrika hasa Tanzania kufikia ugunduzi na uwezo hata wa kutengeneza midoli
 
Inaonyesha bado hatuko tayari kwa mapinduzi chanya. Sera ya hii nchi pamoja na viongozi wamesababisha kuzalisha wananchi wa ajabu sana.
Fikiria kitu kidogo kama maji kimeshindikana wakati tuna mito na maziwa ya kutosha,inaumiza sana
 
Sio jambo la kufurahisha wala kufurahia kwa hali tuliyo kuwa nayo kiujumla, kuanzia namna ya tunavyo ishi kila siku. Dunia ya sana iko mbali na kwa haraka sana ila sisi watanzania tunaonekana bado sana ama hatuko tayari kwenda vile dunia iliko fika ama inako elekea. Inashangaza sana

Napenda tujadili kuhusu teknolojia, teknolojia inaonekana kwetu sisi bado tuko nyuma sana tofauti na mataifa mengine.

Staili ya maisha tunayo ishi imetufanya tudumae kimawazo hasa katika kutatua matatizo. Leo hii hapa Tanzania asilimia kubwa ya wananchi mitaani mpaka maofisini wanazungumza ama kujadili mambo yasio na mantiki yoyote ile katika dunia ya sasa.

Unakuta asilimia kubwa ya wananchi kuanzia asubuhi mpka muda wa kulala ni kupigizana kelele na mambo ya usimba na uyanga, siasa, wanawake na umbea tu.

Kweli kwa dunia tunayoilekea bado tunajadili ujinga kama huo.!? Yaani tunakaa na kupoteza muda wakati wenzetu huko wanafanya makubwa kila uchwao sisi tumebaki na kejeli za kijinga huko mitandaoni.

Wapo watano sema Serikali ndio imetufikisha hapa, naam kwa asilimia kubwa ni wao na hii ni kutokana kuwepo kwa sera mbovu hasa katika sekta ya elimu.

Hawa jamaa wanajiita viongozi hawana huruma kabisa na sisi wao wanajiangalia wenyewe tu, tuachane na hao jamaa maana hawana msaada wowote kwetu.

Nauliza sisi kama sisi tumechukua hatua ipi?

Duniani kumetokea mapinduzi makubwa mno ya teknolojia ila sisi hatujui tuko wapi na tunaelekea wapi. Leo hii huko China wana barabara inapita chini ya maji ila sisi kurusha tu satellite tumeshindwa wakati Kenya na Rwanda wamemeza.

Wapo watakao sema usilinganishe China na Tanzania, naam ni sahihi kabisa ila huoni taifa lako lina rasilimali nyingi kuliko hiyo China, sasa jiulize wamefanya nn mpaka wakupite. Akili mtu wangu

Leo hii kuna ishu ya Cryptocurrency, hii kitu nadhani kwa asilimia kubwa wengi wameisikia ama kuifahamu kabisa.

Cryptocurrency hii itakuja kuwa mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kifedha hapo baadaye, je ni wangapi wana ufahamu kuhusu hii kitu na wako tayari?

Sisi watanzania tumekalia mambo ya kipumbavu na kuacha mambo ya msingi, hatujifunzi vitu vipya wala ata kusoma vitabu hatutaki tupo tupo tu yaani inauma sana.

Sisi watanzania tunaelewa kwamba ukimaliza kidato cha nne ama ukifika chuo kikuu baasi umemaliza kila kitu hatutaki tena kujifunza ama kupanua mawazo yetu.

Sipo hapa kuongelea habari za Cryptocurrency ila nitatolea mfano tu. Wapo wadau mbalimbali wameleta mada kuhusu hii kitu lakini matokeo yake wakaitwa matapeli hii inaonyesha ni kiasi gani baadhi ya sisi watanzania hatuko tayari kujifunza, kujifanya tunajua na kupinga kumbe ujinga tu.

Niliwahi kutana na maneno mazuri sana katika moja ya kitabu cha mwandishi Robert Kiyosaki nanukuu "The most successful people in the world are the most rejected people in the world". Sisi watanzania tumekalia kupinga, kejeli na kuto kutaka kujifunza.

Unapinga Cryptocurrency wakati huo huo unatumia internet kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kuelewa ama kuamini ishu ya internet leo hii tunaitumia.

Nini kinakufanya usiamini Cryptocurrency wakati hayo ni matokeo ya teknolojia, vipo vingi vitakuja kwenye masuala ya teknolojia.

Mwenyezi Mungu ametujalia akili ili itumike kutatua matatizo yetu sio kupinga na kujadili masuala yasio na manufaa kwetu sisi kwa sasa na hapo baadaye.

Yapo mengi ya kuyaandika ila nisiwachoshe ila tujitahidi kuwa tayari kwa mabadiliko ya dunia. Tutumie akili zetu kutatua changamoto zinazotukabili na pia tuwe tayari kujifunza sio kila kitu ni ubishi tu, asanteni.
Watu kutwa wanashindia michembe maharage na miwa watakuwa na akili hao?
 
Mkuu tuna changamoto nyingi sana pia tuna rasilimali nyingi sana za kutatua changamoto zetu. Ishu ni kwamba tunashindwa vipi kutatua hizo changamoto wakati kila kitu tunacho, poor Tanzania.
Fikiria kitu kidogo kama maji kimeshindikana wakati tuna mito na maziwa ya kutosha,inaumiza sana
 
Mkuu tuna changamoto nyingi sana pia tuna rasilimali nyingi sana za kutatua changamoto zetu. Ishu ni kwamba tunashindwa vipi kutatua hizo changamoto wakati kila kitu tunacho, poor Tanzania.
Tukiwasambazia maji nchi nzima kwa mara moja halafu awamu nyingine za Uchaguzi tukijawaomba kura tutawaahidi nini?
 
Sasa hivi hot topic wanajadili chupa ya mirinda,wanashindana kupost hizo chupa huko Instagram.
 
Mkuu live your life achana na sera za nchi, watanzania.
One man can't change the world.
 
Well said yaani bado wana mawazo ya miaka ya kudai Uhuru,mawazo mfu, kuabudu watu, duniani hakuna nchi yenye nyimbo za kuabudu viongozi lakini TZ kila siku zinaimbwa
 
Nini kinakufanya usiamini Cryptocurrency wakati hayo ni matokeo ya teknolojia, vipo vingi vitakuja kwenye masuala ya teknolojia.
kuamini Cryptocurrency kuijua kufahamu, kuifuatilia na kujiunga as an investment ni vitu viliwi tofauti kabisa..., unaweza ukajua stock market investments ila ukasema this is not for me..., kujua teknolojia na kuitumia na kufanya speculations ni vitu tofauti..

Watanzania kwenye teknolojia yaani wananchi wanajitahidi..., mambo ya mobile phones na digital wallets (phone transactions) ilishakuwa imetapakaa mpaka kwa vikongwe ni Serikali tu na Matozo ndio wakapunguza hio kasi....

Kwahio as a technology watanzania wako tayari kui-embrance na hata hapa tunaitumia kufanya jambo ambalo miaka kadhaa lisingewezekana... (Dunia ya Sasa inakwenda Kasi) mambo yanabadilika kwa sekunde.., ila haimaanishi kila kinachopita ukirukie..., kuna vitu only time will tell (hata kama ni vizuri au bora kiasi gani) does not mean they will pan out (especially in this world of competition and discoveries)
 
Toka Watanzania walipopitisha sheria zao za magari wanaona ni chombo cha starehe nikagundua wapo nyuma ya muda sana ndio maana tunapeana hongera kununua ist ya 2004 na usingizi hupati ukinunua wakati wapo wahuni wa kimalawi au Zambia utawakuta na Toyota GD 6 ya 2021 na kodi wao wamelipa haizidi milioni kumi ya Kitanzania..wakati Tanzania hiyo si chini ya 30m lazima tutumie vitu chakavu kwa mfumo huu..
 
Yaani tumeshindwa ata kutetea haki zetu za msingi kabisa
Well said yaani bado wana mawazo ya miaka ya kudai Uhuru,mawazo mfu, kuabudu watu, duniani hakuna nchi yenye nyimbo za kuabudu viongozi lakini TZ kila siku zinaimbwa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom