Sisi watanzania bado tuko nyuma sana ya muda

Sio jambo la kufurahisha wala kufurahia kwa hali tuliyo kuwa nayo kiujumla, kuanzia namna ya tunavyo ishi kila siku. Dunia ya sana iko mbali na kwa haraka sana ila sisi watanzania tunaonekana bado sana ama hatuko tayari kwenda vile dunia iliko fika ama inako elekea. Inashangaza sana

Napenda tujadili kuhusu teknolojia, teknolojia inaonekana kwetu sisi bado tuko nyuma sana tofauti na mataifa mengine.

Staili ya maisha tunayo ishi imetufanya tudumae kimawazo hasa katika kutatua matatizo. Leo hii hapa Tanzania asilimia kubwa ya wananchi mitaani mpaka maofisini wanazungumza ama kujadili mambo yasio na mantiki yoyote ile katika dunia ya sasa.

Unakuta asilimia kubwa ya wananchi kuanzia asubuhi mpka muda wa kulala ni kupigizana kelele na mambo ya usimba na uyanga, siasa, wanawake na umbea tu.

Kweli kwa dunia tunayoilekea bado tunajadili ujinga kama huo.!? Yaani tunakaa na kupoteza muda wakati wenzetu huko wanafanya makubwa kila uchwao sisi tumebaki na kejeli za kijinga huko mitandaoni.

Wapo watano sema Serikali ndio imetufikisha hapa, naam kwa asilimia kubwa ni wao na hii ni kutokana kuwepo kwa sera mbovu hasa katika sekta ya elimu.

Hawa jamaa wanajiita viongozi hawana huruma kabisa na sisi wao wanajiangalia wenyewe tu, tuachane na hao jamaa maana hawana msaada wowote kwetu.

Nauliza sisi kama sisi tumechukua hatua ipi?

Duniani kumetokea mapinduzi makubwa mno ya teknolojia ila sisi hatujui tuko wapi na tunaelekea wapi. Leo hii huko China wana barabara inapita chini ya maji ila sisi kurusha tu satellite tumeshindwa wakati Kenya na Rwanda wamemeza.

Wapo watakao sema usilinganishe China na Tanzania, naam ni sahihi kabisa ila huoni taifa lako lina rasilimali nyingi kuliko hiyo China, sasa jiulize wamefanya nn mpaka wakupite. Akili mtu wangu

Leo hii kuna ishu ya Cryptocurrency, hii kitu nadhani kwa asilimia kubwa wengi wameisikia ama kuifahamu kabisa.

Cryptocurrency hii itakuja kuwa mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kifedha hapo baadaye, je ni wangapi wana ufahamu kuhusu hii kitu na wako tayari?

Sisi watanzania tumekalia mambo ya kipumbavu na kuacha mambo ya msingi, hatujifunzi vitu vipya wala ata kusoma vitabu hatutaki tupo tupo tu yaani inauma sana.

Sisi watanzania tunaelewa kwamba ukimaliza kidato cha nne ama ukifika chuo kikuu baasi umemaliza kila kitu hatutaki tena kujifunza ama kupanua mawazo yetu.

Sipo hapa kuongelea habari za Cryptocurrency ila nitatolea mfano tu. Wapo wadau mbalimbali wameleta mada kuhusu hii kitu lakini matokeo yake wakaitwa matapeli hii inaonyesha ni kiasi gani baadhi ya sisi watanzania hatuko tayari kujifunza, kujifanya tunajua na kupinga kumbe ujinga tu.

Niliwahi kutana na maneno mazuri sana katika moja ya kitabu cha mwandishi Robert Kiyosaki nanukuu "The most successful people in the world are the most rejected people in the world". Sisi watanzania tumekalia kupinga, kejeli na kuto kutaka kujifunza.

Unapinga Cryptocurrency wakati huo huo unatumia internet kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kuelewa ama kuamini ishu ya internet leo hii tunaitumia.

Nini kinakufanya usiamini Cryptocurrency wakati hayo ni matokeo ya teknolojia, vipo vingi vitakuja kwenye masuala ya teknolojia.

Mwenyezi Mungu ametujalia akili ili itumike kutatua matatizo yetu sio kupinga na kujadili masuala yasio na manufaa kwetu sisi kwa sasa na hapo baadaye.

Yapo mengi ya kuyaandika ila nisiwachoshe ila tujitahidi kuwa tayari kwa mabadiliko ya dunia. Tutumie akili zetu kutatua changamoto zinazotukabili na pia tuwe tayari kujifunza sio kila kitu ni ubishi tu, asanteni.
Umeanza vzr ila umeharibu na haya masua la hela za kidigitali

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toka Watanzania walipopitisha sheria zao za magari wanaona ni chombo cha starehe nikagundua wapo nyuma ya muda sana ndio maana tunapeana hongera kununua ist ya 2004 na usingizi hupati ukinunua wakati wapo wahuni wa kimalawi au Zambia utawakuta na Toyota GD 6 ya 2021 na kodi wao wamelipa haizidi milioni kumi ya Kitanzania..wakati Tanzania hiyo si chini ya 30m lazima tutumie vitu chakavu kwa mfumo huu..
Watunga sheria wamepatikana kwa sheria mbovu,tena wanaendelea kutunga sheria mbovu.
Kigezo cha kumpata kiongozi wa siasa ni " kujua kusoma na kuandika" .Baada ya miaka 60 ya uhuru tumeendelea kurudi nyuma katika kutunga sheria na kanunu zenye uwezo wa kusimamia na kuinua uchumi wa taifa.
Mpaka sasa watunga sheria hawaamini kuwa ukipunguza kodi ya uagizaji magari,magari yataongezeka,matumizi ya mafuta yataongezeka,utaongeza makusanyo kupitia matumizi ya mafuta.
Kilimo mazao mapya ya biashara hayaongezeki wala kufanyiwa utafiti:
Tanzania zao la kahawa na pamba ni mazao yaliyopoteza usimamizi na soko.
Taasisi za utafiti wa kilimo haziongezi mazao mapya ya biashara kwa wakulima(mfano kokoa,zabibu na mazao mengine) ili hali nchi ina ardhi ya kutosha na wakulima wapo tayari kupokea maelezo na maelekezo kwa zao lolote litakalo waingizia kipato ili mradi uhuru uwrpo katika uuzaji katika masoko ya ndani na nje.
 
Wiki iliyopita nimeona tangazo lingine la kuwepo kwa Tozo mpya kwa magari ya mizigo kuanzia tani moja kuendelea kwa Kinondoni pekee sasa kila sehemu wakianzisha hiyo kodi ya maroli ya mafuta eti elfu hamsini yaani wao wanakaa kuongeza Tozo kila kukicha sijui wanafikiri nini maana hawajui kuwa wanaongeza inflation kwenye bidhaa bila wao kujua yaani kila mtu anakaa na kutoa mawazo bila kushirikisha bodi ya Uchumi sijui hata kama ipo maana nao wakiwepo watakua kama Latra na Ewura tu.
 
Wiki iliyopita nimeona tangazo lingine la kuwepo kwa Tozo mpya kwa magari ya mizigo kuanzia tani moja kuendelea roli la mafuta elfu hamsini yaani wao wanakaa kuongeza Tozo kila kukicha sijui wanafikiri nini..
Wenye mamlaka wamekosa ubunifu,hakuna tathimini inayofanyika namna ya kupunguza kodi.
Kama nchi tumeshindwa kujifunza kwa mataifa mengine jirani,eti tuna bandari,lakini nchi ambazo hazina bandari kodi zao zipo chini.?!!
 
Nadhani tuna roho mbaya tu sio bure na ubinafsi haiwezekani bei ya mafuta Brantire ikawa ina tofauti ndogo na Arusha na wenzetu hawana kodi kero kwa Wananchi wao kutwa kutumia magari ya kisasa hata magari ya mizigo kwa Zambia na Malawi hayazidi 10M kama kodi miaka miwili iliyopita ilikua kama 6M magari mengi tunayoyaona yanayokuja Tanzania ni ya Watanzania wengi walioshindwa kulipa kodi kubwa za Nchi yao wanasajili kwa Nchi nyingine maisha yanaenda..harafu hizo hela ni ufisadi kila mwaka ukisoma report ya CAG sasa kwa nini waweke kodi kubwa ili kuumiza tu Wananchi...
 
Sio jambo la kufurahisha wala kufurahia kwa hali tuliyo kuwa nayo kiujumla, kuanzia namna ya tunavyo ishi kila siku. Dunia ya sana iko mbali na kwa haraka sana ila sisi watanzania tunaonekana bado sana ama hatuko tayari kwenda vile dunia iliko fika ama inako elekea. Inashangaza sana

Napenda tujadili kuhusu teknolojia, teknolojia inaonekana kwetu sisi bado tuko nyuma sana tofauti na mataifa mengine.

Staili ya maisha tunayo ishi imetufanya tudumae kimawazo hasa katika kutatua matatizo. Leo hii hapa Tanzania asilimia kubwa ya wananchi mitaani mpaka maofisini wanazungumza ama kujadili mambo yasio na mantiki yoyote ile katika dunia ya sasa.

Unakuta asilimia kubwa ya wananchi kuanzia asubuhi mpka muda wa kulala ni kupigizana kelele na mambo ya usimba na uyanga, siasa, wanawake na umbea tu.

Kweli kwa dunia tunayoilekea bado tunajadili ujinga kama huo? Yaani tunakaa na kupoteza muda wakati wenzetu huko wanafanya makubwa kila uchwao sisi tumebaki na kejeli za kijinga huko mitandaoni.

Wapo watano sema Serikali ndio imetufikisha hapa, naam kwa asilimia kubwa ni wao na hii ni kutokana kuwepo kwa sera mbovu hasa katika sekta ya elimu.

Hawa jamaa wanajiita viongozi hawana huruma kabisa na sisi wao wanajiangalia wenyewe tu, tuachane na hao jamaa maana hawana msaada wowote kwetu.

Nauliza sisi kama sisi tumechukua hatua ipi?

Duniani kumetokea mapinduzi makubwa mno ya teknolojia ila sisi hatujui tuko wapi na tunaelekea wapi. Leo hii huko China wana barabara inapita chini ya maji ila sisi kurusha tu satellite tumeshindwa wakati Kenya na Rwanda wamemeza.

Wapo watakao sema usilinganishe China na Tanzania, naam ni sahihi kabisa ila huoni taifa lako lina rasilimali nyingi kuliko hiyo China, sasa jiulize wamefanya nn mpaka wakupite. Akili mtu wangu

Leo hii kuna ishu ya Cryptocurrency, hii kitu nadhani kwa asilimia kubwa wengi wameisikia ama kuifahamu kabisa.

Cryptocurrency hii itakuja kuwa mapinduzi makubwa kwenye masuala ya kifedha hapo baadaye, je ni wangapi wana ufahamu kuhusu hii kitu na wako tayari?

Sisi Watanzania tumekalia mambo ya kipumbavu na kuacha mambo ya msingi, hatujifunzi vitu vipya wala ata kusoma vitabu hatutaki tupo tupo tu yaani inauma sana.

Sisi watanzania tunaelewa kwamba ukimaliza kidato cha nne ama ukifika chuo kikuu baasi umemaliza kila kitu hatutaki tena kujifunza ama kupanua mawazo yetu.

Sipo hapa kuongelea habari za Cryptocurrency ila nitatolea mfano tu. Wapo wadau mbalimbali wameleta mada kuhusu hii kitu lakini matokeo yake wakaitwa matapeli hii inaonyesha ni kiasi gani baadhi ya sisi watanzania hatuko tayari kujifunza, kujifanya tunajua na kupinga kumbe ujinga tu.

Niliwahi kutana na maneno mazuri sana katika moja ya kitabu cha mwandishi Robert Kiyosaki nanukuu "The most successful people in the world are the most rejected people in the world". Sisi watanzania tumekalia kupinga, kejeli na kuto kutaka kujifunza.

Unapinga Cryptocurrency wakati huo huo unatumia internet kwa miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kuelewa ama kuamini ishu ya internet leo hii tunaitumia.

Nini kinakufanya usiamini Cryptocurrency wakati hayo ni matokeo ya teknolojia, vipo vingi vitakuja kwenye masuala ya teknolojia.

Mwenyezi Mungu ametujalia akili ili itumike kutatua matatizo yetu sio kupinga na kujadili masuala yasio na manufaa kwetu sisi kwa sasa na hapo baadaye.

Yapo mengi ya kuyaandika ila nisiwachoshe ila tujitahidi kuwa tayari kwa mabadiliko ya dunia. Tutumie akili zetu kutatua changamoto zinazotukabili na pia tuwe tayari kujifunza sio kila kitu ni ubishi tu, asanteni.
Mkuu umeongea point sana. Kikubwa tusichoke kuwapa elimu. Hata ukiitwa tapeli usivunjike moyo.
 
Kuna wakati unakuwa na fursa lakini unaogopa kuwapa watu kwa kujua watanzania tunaishi kwa mazoea na ukigusia issue ya mtandao mtu anaona kashaibiwa tayari. Unabaki kuona huruma na maisha yanaendelea.
 
Nilikuwa Kenya kwenye matatu (daladala) vijana fulani waliokuwa wanajadili kuhusu "Archimedes principle" ni kwa nini meli inaelea? Kila mtu alitoa wazo lake. Ila Tz ni usimba na uyanga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nitoe mtazamo wangu: Mara nyingi hizi teknolojia zinakuja bila kuwa na watu wa kuchuja na kui-customize iendane na tamaduni au imani za watu. Mfano kwa muislam riba hata 0.000001% ni haramu. Pia muamala wenye kubahatisha mfano udalali wa hizi biashara za mitandaoni, kama (ordergo), Amazon-wish, na nyenginezo kwa nini? Maana siyo tu unalazimishwa utoe pesa kwa matumaini kuwa huenda ukapata pesa zaidi ya ulizotoa, bali unaweza vile vile usipate chochote cha ziada. Ni Kamari hiyo. Na wakati huo huo, kukosekana uhakika wa malipo ya udalali wako, ni wizi uliokubuhu kwa kazi ulioifanya bila ya kuwa na uhakika wa malipo .

Lakini bado nafasi ipo ya kucostomize ili ukienda kwa wamasai ibebe masai value, ikienda kwa waislam iepuke riba au kamari features.

NI USHAURI TU
 
Back
Top Bottom