Sisi wake zetu hawatongozwi??

Sisi wake zetu hawatongozwi??

Huwa lengo la kutongoza ni nini?
Ukitongoza akakubali (kwa maelezo yako huwa unatongoza kutania) inakuwaje?
Halafu we Mpitagwa gwalamsha sebho!
cc: Baba V
Hakuna anaye tania katika kutongoza, ukitania na akakubari si lazima umtafune?
 
Nilishaambiwa au kusikia mara kadhaa kwamba Mwanamke kashtaki kwa Mmewe kwamba kuna Mwanamme anamfuatilia/anamtongoza, matukio haya yapo ya aina kadhaa:-

1. Mwanamke kulalamika kwa Mmewe kwamba katongozwa na mtu anayemfahamu huyu mwanamke kaolewa na kaolewa na nani.

2. Mwanamke kulalamika kwa Mmewe kwamba katongozwa na Mwanamme asiyefahamu kwamba huyu Mwanamke kaolewa.

Kwa sisi ambao wake zetu hawajawahi kutuambia kama huwa wanatongozwa tubaki na picha gani?

1.Wake zetu hawatongozwi?
2.Wanatongozwa wanakataa lakini Wanapuuzia kutuambia?
3.Wanatongozwa wanakubali na kuifanya iwe siri?

Najaribu kuwaza tu kwasababu mimi mke wangu hajawahi kuniambia kwamba ametongozwa na mtu yeyote.
keep_your_mouth_shut_t_shirt-rcd9df959aecd439596d461a76cba2aba_wigms_512.jpg

 
...haambiwi kila kitu...kuna vya kusema na vingine sio bwana,siku ya siku vinakurudi...akhaa

Lakini ukumbuke nyie ni kitu kimoja, unapopata changamoto ni vizuri kumwambia mwenzako ili aviweke katika maombi
 
Kwa mila na desturi zetu, kabla ya mwanamke hajaolewa na au mara tu anapovunja ungo hupewa mafunzo maalumu
yanayojulikana kama unyago, msondo, nk. Katika mafunzo haya mwanamke anafundishwa namna ya kuishi na mume,
kumtunza mume na watoto, nakadhalika. Mwanamke hatarajiwi kuwa sababu ya fadhaa, wasiwasi, au hasira ya mumewe, hivyo hatarajiwi kumwelezea mumewe juu ya yeyote anayemtongoza au mahusiano yake ya siku za nyuma. Kikubwa anachotarajiwa ni kuwa mwaminifu kumkataa yeyote anayemtongoza na kutokujiweka katika mazingira ya kutongozwa kwani mwaname hutongoza anapoona kuna mwanya/dalili za kufanikiwa kama akijaribu. Mwanamke ambaye kila kukicha anamueleza mumewe kuwa fulani kamtongoza basi hajafuzu mafunzo ya unyago, atamfanya mumewe kuwa na wasiwasi wakati wote na kushindwa kufanya kazi, pia atamgombanisha na marafiki, jamaa na ndugu zake. Mwanamke ukijiweka katika mazingira ya kutongozwa, mfano kujichekeshachekesha, kuombaomba ofa, kukubali mialiko isiyo ya kazi wala biashara, kupenda sana kusifiwa kuhusu sura na umbile lake,kupenda sana kuwaelezea watu kuhusu madhaifu ya mumewe, na kugawa ovyo namba yake ya simu ni baadhi tu mazingira yanayotoa mwanya wa kutongozwa.
Wanaume tunajua kuwa kuna mwanamke ambaye hata kama unamtamani kiasi gani lakini kila ukimwangalia usoni huoni uwezekano/nafasi ya kukubaliwa, hivyo hujikuta ukiahirisha kila mara wazo la kumtongoza.

Umenena sana! Hapa ngoja niongezee kama mkeo yuko facebook au instagram kazi kuweka picha kageuka aonekane kwa nyuma huku amejibedua lazma atongozwe na HAJAFUZU.

Mwanamke aliyefuzu anamtunzia mumewe na ana heshma mbele ya jamii.
 
mkeo anatongozwa tena sana hasa kwa sababu na wewe ulimtongoza na mkafika mahali mkakubaliana kuwa mke na mume. Pia ukumbuke kwamba kuna baadhi ya wanaume ambao kwao ni mwiko kupitwa na kiumbe anayeitwa mwanamke bila kumsumbua kwa kumtongoza.

Hivyo ndugu nikuhakikishie bila kuacha shaka kwamba mkeo anatongozwa tu tena narudia anatongozwa sana na anamalizana na watongozaji wake huko huko bila kukuletea taarifa. Sasa anamalizana nao vipi: hilo linabaki kuwa ni la kwake na Mungu wake.
 
...kuna mwanamke ambaye hata kama unamtamani kiasi gani lakini kila ukimwangalia usoni huoni uwezekano/nafasi ya kukubaliwa, hivyo hujikuta ukiahirisha kila mara wazo la kumtongoza

hii ni kweli kabisa, mi imenitokea sana, mwanamke kutoa uzazi anakuwa amependa mwenyewe tu, wanaume huwa tunapima kwanza kina kama kinaingilika.
 
mkeo anatongozwa tena sana hasa kwa sababu na wewe ulimtongoza na mkafika mahali mkakubaliana kuwa mke na mume. Pia ukumbuke kwamba kuna baadhi ya wanaume ambao kwao ni mwiko kupitwa na kiumbe anayeitwa mwanamke bila kumsumbua kwa kumtongoza.

Hivyo ndugu nikuhakikishie bila kuacha shaka kwamba mkeo anatongozwa tu tena narudia anatongozwa sana na anamalizana na watongozaji wake huko huko bila kukuletea taarifa. Sasa anamalizana nao vipi: hilo linabaki kuwa ni la kwake na Mungu wake.

Ooooh God!!!!
 
labda mkeo sio mzuri. umeoa polygob hakuna anayevutiwa naye
 
unadhani kweli nakaa miaka yote hii sitongozwi?

Na unapotongozwa huwa unarespond kivipi?

Je, kuna ambao huwa unawapenda na kuwapa walau kanafasi kakuongea na ku flirt nao?

Na wale ambao huwafeel je? Huwa unawatolea nje papo hapo au?

Je, kuna ambao wamewahi kukutongoza na ukawakubalia? Hapa kama vile najua jibu lake lakini potelea mbali....I'll ask anyway....
 
Wanaume tunajua kuwa kuna mwanamke ambaye hata kama unamtamani kiasi gani lakini kila ukimwangalia usoni huoni uwezekano/nafasi ya kukubaliwa, hivyo hujikuta ukiahirisha kila mara wazo la kumtongoza.

Usipende kutumia uwingi pasipo na ukweli usijidanganye hakuna mwanamke hata awe serious vp hatongozwi?? kila mwanamke ana level yake wewe ndo unaona huyu hawez nikubalia ukijilinganisha lakini wapo watu wanaona kabisa wakienda wana nafasi na kweli wanakubaliwa na wanapewa na haijalishi uyo ni mke wa mtu au la!!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom