Sisi wake zetu hawatongozwi??

Sisi wake zetu hawatongozwi??

Kwi kwi kwi kwi lol!!!!! hahahahahaha lol!!! nilidhani umelikimbilia hili swali kumbe umelijibu kinamna lol!!!!....Chezeya JF weye!!!!! Maswali mengine huwa hayajibiki 🙂🙂

ha haaaa, hayo maswali yako yoooteeee hayajibiki....... mbaya zaidi hadharani, lol!
 
Last edited by a moderator:
Siwezi kumwambia hata siku moja mpaka naingia kaburini coz hata yeye hasemi aliowatongoza.
 
Kwa mila na desturi zetu, kabla ya mwanamke hajaolewa na au mara tu anapovunja ungo hupewa mafunzo maalumu
yanayojulikana kama unyago, msondo, nk. Katika mafunzo haya mwanamke anafundishwa namna ya kuishi na mume,
kumtunza mume na watoto, nakadhalika. Mwanamke hatarajiwi kuwa sababu ya fadhaa, wasiwasi, au hasira ya mumewe, hivyo hatarajiwi kumwelezea mumewe juu ya yeyote anayemtongoza au mahusiano yake ya siku za nyuma. Kikubwa anachotarajiwa ni kuwa mwaminifu kumkataa yeyote anayemtongoza na kutokujiweka katika mazingira ya kutongozwa kwani mwaname hutongoza anapoona kuna mwanya/dalili za kufanikiwa kama akijaribu. Mwanamke ambaye kila kukicha anamueleza mumewe kuwa fulani kamtongoza basi hajafuzu mafunzo ya unyago, atamfanya mumewe kuwa na wasiwasi wakati wote na kushindwa kufanya kazi, pia atamgombanisha na marafiki, jamaa na ndugu zake. Mwanamke ukijiweka katika mazingira ya kutongozwa, mfano kujichekeshachekesha, kuombaomba ofa, kukubali mialiko isiyo ya kazi wala biashara, kupenda sana kusifiwa kuhusu sura na umbile lake,kupenda sana kuwaelezea watu kuhusu madhaifu ya mumewe, na kugawa ovyo namba yake ya simu ni baadhi tu mazingira yanayotoa mwanya wa kutongozwa.
Wanaume tunajua kuwa kuna mwanamke ambaye hata kama unamtamani kiasi gani lakini kila ukimwangalia usoni huoni uwezekano/nafasi ya kukubaliwa, hivyo hujikuta ukiahirisha kila mara wazo la kumtongoza.

Nimejifunza kitu
 
Nilishaambiwa au kusikia mara kadhaa kwamba Mwanamke kashtaki kwa Mmewe kwamba kuna Mwanamme anamfuatilia/anamtongoza, matukio haya yapo ya aina kadhaa:-

1. Mwanamke kulalamika kwa Mmewe kwamba katongozwa na mtu anayemfahamu huyu mwanamke kaolewa na kaolewa na nani.

2. Mwanamke kulalamika kwa Mmewe kwamba katongozwa na Mwanamme asiyefahamu kwamba huyu Mwanamke kaolewa.

Kwa sisi ambao wake zetu hawajawahi kutuambia kama huwa wanatongozwa tubaki na picha gani?

1.Wake zetu hawatongozwi?
2.Wanatongozwa wanakataa lakini Wanapuuzia kutuambia?
3.Wanatongozwa wanakubali na kuifanya iwe siri?

Najaribu kuwaza tu kwasababu mimi mke wangu hajawahi kuniambia kwamba ametongozwa na mtu yeyote.

Majibu ni Mawili

"2.Wanatongozwa wanakataa lakini Wanapuuzia kutuambia?
3.Wanatongozwa wanakubali na kuifanya iwe siri?"

Wake zetu
1)wanatongozwa kama wanavyotongozwa wanawake wengine.
2) Si kila jambo mkeo akwambie, mengine anayaweka siri, siri inayolenga kuleta amani ndani ya nyumba.
3) Kwani wanaume karibu wote hatuna simile,
4) Tukiambiwa ukweli yanayo wakuta wake zetu wakiwa kazini, njiani au popote walipo mbali nasi
5) tunachukulia hamaki na kusababisha uvunjifu wa amani ndani ya familia.
6) Ni bora tubaki tukiaminiana pande zote mbili, hakuna haja ya kuchunguzana...
7)Kwa hayo tutadumu ndani ya ndoa zetu na tutakuwa wenye furaha
 
Lakini kuna wanaume wengine wanajisikia raha sana wakisikia mke wake anawasumbua watazamaji

ni wachache sana nakumbuka nikiwa mjamzito nilitoka kutembea peke yangu akatokea mtu akaanza kunitongoza..nilivyorudi home nikawa namwambia hubby kama utani"kumbe ata sisi na matumbo yetu tuna mvuto".!... Wee kilichofata Mungu ndo alikua mwamuzi...siwezi kumwambia tena ata nitongozwe na rafiki yake!
 
Nilishaambiwa au kusikia mara kadhaa kwamba Mwanamke kashtaki kwa Mmewe kwamba kuna Mwanamme anamfuatilia/anamtongoza, matukio haya yapo ya aina kadhaa:-

1. Mwanamke kulalamika kwa Mmewe kwamba katongozwa na mtu anayemfahamu huyu mwanamke kaolewa na kaolewa na nani.

2. Mwanamke kulalamika kwa Mmewe kwamba katongozwa na Mwanamme asiyefahamu kwamba huyu Mwanamke kaolewa.

Kwa sisi ambao wake zetu hawajawahi kutuambia kama huwa wanatongozwa tubaki na picha gani?

1.Wake zetu hawatongozwi?
2.Wanatongozwa wanakataa lakini Wanapuuzia kutuambia?
3.Wanatongozwa wanakubali na kuifanya iwe siri?

Najaribu kuwaza tu kwasababu mimi mke wangu hajawahi kuniambia kwamba ametongozwa na mtu yeyote.

Kaka co kutongozwa tu wanaliwa haswaa na ndio wanaoongoza kwa kutoa ndogo (0710..) Usimkanie mwanamke kamwe c. ndugu yako huyo wanadanganywa na vitu vidogo sana!!! muangalie tu then mwache la sivyo utapasuka mishipa ya moyo kaka!
 
Kwa hiyo huwenda wake zetu pia wanatongozwa lakini hawatuambii tu
Tena wanatongozwa sana tu, sema hawatuambii, wajua mke wa mtu kutokana na matunzo mazuri ya mme hunawiri, kupendeza na kuwa na mwonekana mzuri tofauti na wanawake wengine wasiokuwa na waume so longer wao wanakuwa hawana mtu anayewajibika moja kwa moja kuwatunza, naomba ieleweke kwamba, hata kama wana wazazi wanaowatunza, mwanamke huwa mwenye faraja zaidi apatapo matunzo ya mpenzi/mumewe na hivyo kumfanya awe huru na wa kuvutia zaidi mbele ya mwanamume mwingine! Hii pia inachangiwa na ukweli kwamba, mke wa mtu atakula chochote akipendacho na kwa wakati wowote, kwani anakuwa yuko kwake na hapangiwi/haamliwi cha kufanya na mtu yeyote, vyote hivi vitamfanya awe na mvuto wa kipekee! Jambo linalowavutia watongozaji.... Nimemaliza, na-log off!
 
Kwa mila na desturi zetu, kabla ya mwanamke hajaolewa na au mara tu anapovunja ungo hupewa mafunzo maalumu
yanayojulikana kama unyago, msondo, nk. Katika mafunzo haya mwanamke anafundishwa namna ya kuishi na mume,
kumtunza mume na watoto, nakadhalika. Mwanamke hatarajiwi kuwa sababu ya fadhaa, wasiwasi, au hasira ya mumewe, hivyo hatarajiwi kumwelezea mumewe juu ya yeyote anayemtongoza au mahusiano yake ya siku za nyuma. Kikubwa anachotarajiwa ni kuwa mwaminifu kumkataa yeyote anayemtongoza na kutokujiweka katika mazingira ya kutongozwa kwani mwaname hutongoza anapoona kuna mwanya/dalili za kufanikiwa kama akijaribu. Mwanamke ambaye kila kukicha anamueleza mumewe kuwa fulani kamtongoza basi hajafuzu mafunzo ya unyago, atamfanya mumewe kuwa na wasiwasi wakati wote na kushindwa kufanya kazi, pia atamgombanisha na marafiki, jamaa na ndugu zake. Mwanamke ukijiweka katika mazingira ya kutongozwa, mfano kujichekeshachekesha, kuombaomba ofa, kukubali mialiko isiyo ya kazi wala biashara, kupenda sana kusifiwa kuhusu sura na umbile lake,kupenda sana kuwaelezea watu kuhusu madhaifu ya mumewe, na kugawa ovyo namba yake ya simu ni baadhi tu mazingira yanayotoa mwanya wa kutongozwa.
Wanaume tunajua kuwa kuna mwanamke ambaye hata kama unamtamani kiasi gani lakini kila ukimwangalia usoni huoni uwezekano/nafasi ya kukubaliwa, hivyo hujikuta ukiahirisha kila mara wazo la kumtongoza.

Umesema yote mkuu. Ukiona mke ametoka nnje ya ndoa 99% ujue ni yeye amekusudia (amependa) si kingine.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom