Sisi ni ndugu, tunaishi katika jamii moja. CHOKOCHOKO ZA UDINI ZA KAZI GANI? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sisi ni ndugu, tunaishi katika jamii moja. CHOKOCHOKO ZA UDINI ZA KAZI GANI?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jumakidogo, Jan 18, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Siku hizi choko choko za udini zimepamba sana moto mitaani na, hata katika mitandao ya kijamii mfano hapa JF. Hebu tujiulize swali moja dogo. Tukiweka udini mbele na kuacha undugu na ujirani kando tunapata maslahi gani? Tunapata faida gani? Huu ni wakati wa kila mtu kuheshimu imani ya mwenzake bila kuingiliana wala kuhoji kwa nini wewe unaingia kusali katika pango!, baada ya hapo dini zote tuishi kama jamii moja isiyobaguana. Sisi ni ndugu na marafiki na tunaishi pamoja mitaani na tunafanya kazi pamoja maofisini na tunashirikiana kuijenga nchi yetu na palipo na sherehe mbali mbali tunaalikana na wake zetu wanaishi vizuri mtaani na watoto wetu wanakwenda shule pamoja na hata sokoni tunafanya biashara huku tukishirikiana meza zetu. Tuishi kwa amani! Anayetaka kuabudu mbuzi ni hiari yake! Na Anayetaka kuabudu jua sawa tu na anayetaka kuabudu mtu yeye tu na anayetaka kuabudu treni aachwe na imani yake.. Tuishi kwa amani lakini tusilazimishane imani. Tutakalia malumbano ya dini, wakati wenzetu wanasonga mbele...Haya ni maoni tu kwa wale wapenda amani wote.
   
 2. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mimi hakuna kitu kinachoniudhi kama hizi chokochoko za kidini. Eti watu wazima mmekalia kugombania dini! Dini zenyewe si zetu. Hivi kuna mtu anadhani kuwa dunia ingekuwa nzuri zaidi endapo watu wote tungekua na dini moja? Mi sidhani..!
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  hazina tija yoyote
  ukirudi mtaani tunafahamiana kuheshimiana bila kujali dini zetu

  inaelekea kuna kikundi cha watu kwa makusudi au bil kujua wanaleta chokochoko hizi
  na wengine wanazidandia bila kufikiria, yeees bila kutumia akili na kuanza chokochoko

  chokochoko hizi zitaleta athari kubwa sana mbeleni
  tena usikute waanzilishi wa chokochoko hizi wakiona kumenuka wana uwezo wa kukwea pipa(ndege) na kusonga safari
  wenzangu na mimi washadadizi na wanaotumika kama akili za kufikiri hawana watabaki hapa kupokea stahiki yao

  watanzania akili kichwani vichwani mwenu, mtu mzima mtu atakulishaje chuki za kipuuzi zisizo na faida yoyote nawe kama huna akili(au kama umeshikiwa akili) ukamsikiliza na kuleta hoja za kidini

  Jumakidogo,
  tukatae hoja za udini tuzikatae kwa nguvu zote, yaani nakuunga mkono.
   
 4. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Dini ni imani. Narudia tena kauli yangu humu Jf: viogozi wetu wa dini zetu ambao wana uwanja na tumewapa mamlaka wazungumze. Mimi kama mimi uelewa wangu ni mdogo kwa hiyo nikitaka malumbano na muumini wa dini nyingine, nitabishana kwa ushabiki na pengine nitaonesha ufundi wangu wa matusi na kejeli na sio mtazamo wa dini yangu. Endapo viongozi wangu ni dhaifu, bora waachie ngazi.
   
 5. k

  kipinduka Senior Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 130
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  muulize mkuu wa shule ya sekondar NDANDA MTWARA
   
 6. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Najua wewe ni mwanaharakati. Hapa tunazungumza namna ya kuirejesha jamii yetu iwe moja na kuondokana na tofauti za kiitikadi za imani ya kidini. Tatizo letu waislam ni kutaka serikali itufanyie kila kitu kabla ya kujaribu kuanza kutembea wenyewe. Tuonyeshe mshikamano kwanza wenyewe kwa wenyewe kwa kujiwekea malengo katika kipindi maalumu cha mpito bila kuwanyooshea vidole watu wa imani nyingine. Kama watoto wetu wananyanyaswa huko. Tuwapeleke kwenye shule zetu za kata wakati tunafanya mchakato wa kujenga mashule yetu, kwa nguvu zetu. Mi naona kuna tatizo jingine kuhusu elimu kwa viongozi wetu wa dini. Wao wamebobea kwenye maarifa ya dini tu. Tunatikiwa tupate vijana wasomi sasa wa kutuendeshea taasisi zetu za kislamu ambao wakikaa ofisini si lazima wavae kanzu, wavae mavazi ya kazi. Tuweke mikakati ya kimya kimya bila kulalamika na kutegemea msaada kutoka serikalini. Tunazidi kuchelewa, hayo yaje baadae. Huwezi kumtaja Lowasa hapa kwa kuwa anasimamia vyema na kuchangia imani yake. Wanyooshe vidole viongozi walio serikalini ambao ni waislamu wanafanya nini? Usitegemee kuwa Lowasa mkristo atakuja kuhimiza harambee ya waislamu wakati Kikwete naye ambaye ni mwislamu hajui kinachoendelea.
   
 7. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya firauni! Nendeni NSSF mkajionee
   
 8. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,703
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  Nani anaiba rasilimali zenu? Mnarasilimali nyie zaidi ya miskiti? Acha uchochezi wa kidini ww kwani 2kisema na wakristo waandamane hapatakalika kwani wakristo ni wengi kuliko waislamu so cha muhimu kila m2 aheshishmu imani ya mwenzie na sio malumbano yasio na hoja.
   
 9. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Eti waislamu wa bara wako upande wa Zanzibar in case...? angalia mzalendo.net angalia video ya Kongamano la mfumo kristo pemba
   
 10. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,866
  Likes Received: 6,218
  Trophy Points: 280
  kutwa mnaandamana halafu mnasingizia necta. Muweke msisitizo kwa watoto wenu,wasome
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Wewe kalia udini tu na Masheikh ubwabwa wenzako sisi wenzenu tunaendesha harambee za kuongeza vyuo vikuu vingi zaidi.
   
 12. salito

  salito JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  ah ha ha ha ha ha ha nyie ni sawa na sikio la kufa,yaan hapa thread inazungumzia tuwe makini tuachane na udini,nyie mshaanza kulumbana,wapuuz kabisa..
   
 13. SILENT ACtOR

  SILENT ACtOR JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2012
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 618
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 45
  Umenena vema kaka Juma.
   
 14. m

  mfumo JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  NAOMBA KUSAHIHISHA HII; sahihi ni kusema UKISTAAJABU YA FIRAUNI UTAYAONA YA MUSA!!!!KWA SABABU YA MUSA NI MAKUBWA ZAIDI YA FIRAUNI.
   
 15. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Pole sana. With this attitude, bado ipo safari ndefu ya maendeleo.
   
 16. m

  mfumo JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  JUMAKIDOGO,

  KATIKA UDINI HUU AMBAPO WAKRISTO WANAWAONA WAISLAMU SI KATIKA WAO, SI RAHISI KUREJESHA JAMII YETU KUWA PAMOJA KAMA HIVYO UNVYOFIKIRIA JUMAKIDOGO. KWA MTAZAMO WANGU LABDA YAFUATAYO YAFANYIKE NDIO TUNAWEZA KUWA PAMOJA;
  1. WAISLAMU WARUHUSIWE KUANZISHA MAHAKAM YA KADHI KAMA ILIVYO NCHI NYINGINE (MFANO KENYA NA ZANZIBAR).
  2. WAISLAMU WARUHUSIWE KUJIUNGA NA OIC.
  3. MoU YA SERIKALI NA KANISA IFUTWE MARA MOJA. WOTE WALIOHUSIKA KATIKA KUANDAA MKATABA ULE WAKAMATWE NA KUFIKISHWA MAHAKAMANI.HII NI KWA KUWA NI MKATABA UNAOVUNJA KATIBA YA NCHI.IPIGWE HESABU NI KIWANGO GANI WAKRISTO WAMEKOMBA KATIKA MKATABA HUO KISHA WAISLAMU WALIPWE CHOTE AMBACHO WAKRISTO WAMEKIPATA KWA KIPINDI CHOTE CHA MKATABA HUU WA KIFISADI.
  4.UCHAGUZI WA MUFTI WA BAKWATA USIINGILIWE NA SERIKALI.
  5. WAISLAMU WARUHUSIWE KUFANYA IBADA ZAO KATIKA MASHULE, VYUO NA MAOFISINI BILA KUBUGHUDHIWA NA VIONGOZI WA TAASISI HIZO.
  6. MAJENGO YA SERIKALI YAKOME KUTUMIA PESA ZA UMMA KWA MAPAMBO YA SHEREHE ZA DINI YA KIKRISTO.
  7.AJIRA SERIKALINI ZISIWE NA HARUFU YA UDINI KAMA ILIVYO HIVI SASA.
  8. KATIBA IWEKE KIPENGELE AMBACHO HAKITARUHUSU KUFANYA MAAMUZI KWA KUPENDELEA DINI FULANI. ADHABU KALI IWEKWE KWA YOYOTE ATAKAEKUWA MDINI.

  ANGALIZO;
  WAISLAMI HAWATAKI KUPENDELEWA WANATAKA HAKI ITENDEKE KWA WANANCHI WOTE BILA KUJALI ITIKADI ZAO.
   
 17. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bwana Mfumo. Hayo uliyoyasema ndio kigezo cha kuwa na chuki kati yetu na upande wa pili? Kati ya serikali na wakristo. Hiyo mikataba ilianzia kwa nani? Ikiwa wakristo waliomba, serikali ikakubali. Lakini sisi tunapeleka madai yetu, lakini serikali inasuasua. Nani wa kumlaumu hapa kati ya wakristo na serikali? Ni nani wa kumjengea chuki kati ya wakristo na Serikali? Mi naona kama ni madai, hasira, chuki na tuzielekeze kwa serikali ili itimize haya tunayoyataka ili tulingane na wenzetu. Haki zetu tunamdai nani kati ya serikali na wakristo? Kama tunaidai serikani, hakuna sababu ya msingi kupoteza muda kwa kujaribu kutaka kujilinganisha na wakristo. Tupoteze muda katika kudai haki zetu kwa serikali bila kuharibu uhusiano uliopo kati ya dini hizi kuu hapa nchini. Tena serikali ya sasa rais ni mwislamu, makamu ni mwislamu, tunao wabunge na mawaziri waislamu wa kutosha. Tuwashinikize hawa kuwa madai yetu yana msingi. Wakishindwa, chuki na hasira zetu ziwe juu yao, badala ya kuleta malumbano na watu wa imani nyingine.
   
 18. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Yote haya muanzilishi ni JKN - Waislam wameamka sasa. JKN alipanda mbegu ya udini imechipua sasa
   
 19. K

  Kandukamo Member

  #19
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iko wapi haki yetu sisi Watanganyika tusioamini katika imani hizi za kimapokeo? Katu maishani mwangu sitokuja sahau nilivyonyimwa kupanga chumba kisa imani yangu ni tofauti na Mama mwenye nyumba. Kwa tendo hilo ndipo nilikuja tambua imani yangu ya kiasili ni bora zaidi kuliko hizi za KIMAPOKEO ambazo malengo yake makubwa ni kutugawa katika udugu wetu.
   
 20. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mfumo you have just scraped the top of our National Relligious Disparities. Let it known by all; Islaam is a relligion of peace. Submission to the will of tne one who created all without any help from none. Since Uhuru 50 years ego, affairs of Muslims in TZ have been dictated by the church. When a christian calls Jesus god it is OK. When a muslim says Jesus is not god he could end up in Jail. Thanks to ALLAH we muslims are peacefull.

  Let it also be understood that in this country there are 2 types of muslims. Those who are practising Muslims and those who are only by name. Practising muslims are the ones who are most condemned. I pray that we could exist in harmony for the benefit of our agging nation.
  40:40 "He that works evil will not be requited but by the like thereof: and he that works a righteous deed - whether man or woman - and is a Believer- such will enter the Garden (of Bliss): Therein will they have abundance without measure.
   
Loading...