Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,502
- 51,098
Tangu Rais Samia aingie madarakani amefanya teuzi nyingi tu na katika teuzi hizo wapo watu wamekaa standby kuangalia majina ya Kizungu (isomeke Kikristo) na Kiarabu (isomeke Kiislamu) ili waone kuwa watu wanaoendana nao kiimani "wameula" zaidi au la!
Nataka nieleze sababu za hivyo:
1. Mosi, kuna sense of entitlement.
Kwa miaka mingi sana nchini tangu Uhuru mpaka leo hii, nafasi za Utumishi wa Umma na Serikali zimekaliwa zaidi na Wakiristo kuliko Waislamu. Teuzi nyingi kuanzia Nyerere hadi leo hii Rais Samia, teuzi nyingi zinakwenda kwa Wakiristo.
Hali hii imelalamikiwa sana na Waislamu kwa miaka mingi, kuwa, hili jambo lina ukakasi. Iweje teuzi ziende kwa watu wa mrengo mmoja tu kila wakati wakati nchi hii ni yetu sote, na watu wenye vigezo wapo pande zote? Majibu ambayo watu hawa wamekuwa wakipata ni kejeli, kuwa nyie hamjasoma, kuwa nyie mnaendekeza elimu ahera, lakini hoja yao hiyo siku hizi imekuwa proven wrong.
Hata ikafikia hatua hadi Sheikh Khalifa kutoa orodha ya Waislamu wasomi mamia kwa mamia ili kufuta propaganda kuwa waislamu wenye vigezo vya kutosha kuhudumu katika teuzi mbalimbali hawapo, lakini licha ya hivyo hoja hiyo imekuwa ikifumbiwa macho. Sasa leo, Samia licha ya bado kuendelea kuteua Wakiristo wengi zaidi kuliko waislamu lakini angalau kidooogo waislamu nao wanaonekanaonekana kwa mbali.
Hili limeshtua wale waliozoea kuona teuzi za mrengo mmoja, wanahaha, wamepandwa na ghadhabu, wanataka waendelee kuteuliwa watu wa imani yao kwa wingi uleule (over representation) kama zamani.
2. Sababu ya pili ni kuwa, Siyo kweli kuwa baadhi ya hawa wanaolalamikia udini katika teuzi hawajui kuwa Samia bado anateua Wakiristo wengi zaidi kuliko Waislamu.
Bali wanataka kumblackmail ili asije akazoea kuteuateua Waislamu. Wanampa meseji kuwa, ukijaribu kubadili status quo katika nchi hii na kuwapa nafasi watu wa imani nyingine katika Utumishi wa Serikali kwa wingi kama sisi basi tutakusagia kunguni kwa watu wa imani yetu ili upate wakati mgumu kisiasa.
Kwa hiyo hizi kelele kimsingi ni fitina ya kumchonganisha Rais na Wakiristo ili Rais aogope kuwapa Waislamu nafasi na kwa hiyo Status quo ya Wakiristo kuendelea kudominate Utumishi wa Umma na Serikali, uendelee kama ilivyokuwa tangu Serikali ya Awamu ya Kwanza hadi leo.
3. Sababu ya tatu ni chuki tu, na ufia dini.
Islamophobia is real, kuna watu wanaamini kuwa, kwa kuwabagua watu wa dini nyingine na kuwapendelea watu wa dini yao ni kumfanyia Mungu Ibada!
Wapo watu makazini wakiona kuna wafanyakazi wanavaa hijabu, muda wa swala umefika wanaenda kuswali, au Salamu ya "Assalam Aleikum" imekuwa nyingi katika korido za ofisi wanaanza kuchukia, wanajenga hila mioyoni mwao na kibaya zaidi kuna baadhi wanakwenda mbali hadi ku collude na like minded people ili kuwaletea fitina wenzao n.k.
Enzi hizo wakati nasoma katika chuo kikuu kimoja hapa nchini, wanafunzi Waislamu waliomba chumba kimoja kilicho idle ili wafanye ibada wakazunguushwa mno, wengine wakawa wanapewa vitisho vya siri kuwa wawe makini na ajenda yao hiyo kwamba wachague chuo au dini (yaani ni kitisho cha kupigwa fitina hadi wafukuzwe chuo).
Lakini at the same time, kila siku jioni na siku za Jumamosi na Jumapili madarasa ya chuo hichohicho Wakiristo wameruhusiwa kuyatumia kusali na kuabudu. Umeona aina hii ya chuki, choyo na roho mbaya?
Ushauri wangu:
1. Watanzania tuachane na habari za kutaka upendeleo katika ajira na teuzi. Hii nchi ni yetu sote. Si vizuri kunung'unika watu wa imani nyingine pia wakipata fursa za kuhudumu katika nchi.
2. Lakini kama tunaona upendeleo wa dhahiri katika teuzi, hapo kweli tuseme na tupige kelele. Kuna wakati nchi hii Rais mmoja aliunda Baraza la Mawaziri la watu zaidi ya 20 akaweka Waislamu watatu. Sasa katika situation kama hiyo kweli hapo jamii nzima haipaswi kukaa kimya.
Hivyo hivyo leo hii Samia akiunda Baraza la Mawaziri akaweka Wakiristo watatu tu hata mimi sitokaa kimya. Tusiwe na double standard, kwamba teuzi zikifavour watu wetu tunanyuti, ila wengine wakianza kuchomoza basi tunakuja hapa JF kuanzisha nyuzi lukuki za udini. Hiyo siyo fair.
3. Tuzidi kuimarisha, Umoja, Amani na Mshikamano. Nchi hii Wakiristo are here to stay, Waislamu are here to stay. Yesu hakuoni mfuasi wake bora kwa kuwa mbaguzi na wala Mtume Muhammad hakuoni mfuasi wake bora kwa kuvunja amana za watu wote. Tupendeane mazuri.
Nawasilisha.